Michezo ya Olimpiki
Michezo ya Olimpiki ni mashindano ya michezo makubwa duniani inayofanyika kila baada ya miaka minne.
Michezo ya Olimpiki imekuwa na historia ndefu katika vipindi viwili:
- Michezo ya Olimpiki ya Kale ilifanyika tangu tarehe isiyojulikana lakini kwa uhakika kuanzia mwaka 776 KK hadi mwaka 393 BK katika mtaa wa mahekalu wa Olimpia kwenye rasi ya Peloponesi nchini Ugiriki.
- Michezo ya Olimpiki ya Kisasa ya kwanza ilitokea mwaka 1896 mjini Athens (Ugiriki). Mwanzishilishaji alikuwa Mfaransa Pierre de Coubertin alitaka kutumia kielelezo cha michezo ya kale kwa kujenga uhusiano mzuri kati ya vijana wa nchi mbalimbali na kuwapatia nafasi ya kushindana kwenye uwanja wa michezo badala ya uwanja wa vita. Coubertin alianzisha Kamati ya Kimataifa ya Olimpiki (International Olympic Committee - IOC).
Michezo ya kisasa hufanyika katika mji mwingine kila safari. Michezo ya 2004 ilifanyika Athens, ya 2008 huko Beijing na ya 2012 itafanyika London.
Kuna tofauti kati ya michezo ya kiangazi na michezo ya majira ya baridi.
Washindi watatu wa kwanza wa kila mashindano hupewa medali ya dhahabu, fedha au shaba.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni