Kikosi cha Simba S C
Kikosi cha Yanga AFC
KARIBU KATIKA BLOGU HII YA KUELIMISHA, KUBURUDISHA NA KUONYA KUPITIA MADA MBALIMBALI NA HATA PICHA. ONGEZA MAHUSIANO KWA KUJUMUIKA NA WENZIO HAPA.UNAWEZA TUMA PICHA NA MAELEZO KWA ANUANI HII;mkuu74@gmail.com



| Mrembo Kusaula Nguo Kushangilia Ushindi wa Timu ya Taifa | ||
![]() Larissa Riquelme | Tuesday, July 19, 2011 1:10 AMMacho ya washabiki wa soka wa nchini Paraguay yameelekezwa kwa mrembo maarufu nchini humo ambaye aliahidi kusaula nguo zake zote iwapo timu yake ya taifa ingevuka hatua ya robo fainali ya kombe la Copa America. | |
| Mrembo wa nchini Paraguay, Larissa Riquelme aliahidi kumwaga radhi hadharani katika kushangilia timu yake ya taifa iwapo timu hiyo itavuka hatua ya robo fainali ya kombe la Copa America. Hivi sasa macho ya washabiki wa soka wa nchini Paraguay yameelekezwa kwa Larissa kwani timu ya taifa ya Paraguay imeweza kuvuka hatua ya robo fainali baada ya kuibugiza Brazil mabao 2-0 kwa penalti na kuitupa nje ya mashindano ya Copa America. Katika mechi hiyo iliyoamuliwa kwa penalti baada ya mechi kuisha sare ya 0-0, Brazil ilikosa penalti zote nne ilizopiga wakati Paraguay iliweza kuzamisha kimiani penalti mbili kati ya tatu ilizopiga. Wakati Paraguay ikijiandaa kupambana na Venezuela siku ya jumatano kwenye mechi ya nusu fainali, washabiki wa soka wanasubiri kuona kama Larissa atatimiza ahadi yake. Larissa aliwahi kutoa ahadi kama hiyo wakati wa kombe la dunia nchini Afrika Kusini mwaka jana, lakini kwakuwa Paraguay haikufika mbali hakulazimika kuitimiza ahadi yake. | ||



| Kisasi cha Kumuua Kaka wa Rais, Maiti Yatundikwa Sokoni | ||
![]() Maiti ya Sardar Muhammad ikiwa imetundikwa | Friday, July 15, 2011 3:43 AMMaiti ya mzee wa Afghanistan ambaye aliuliwa baada ya kumuua kwa kumpiga risasi kaka yake rais wa Afghanistan,Hamid Karzai, ilitundikwa sokoni kama kisasi kwa mauaji aliyoyafanya. | |
| Sardar Muhammad alikuwa mtu aliyeaminika sana kwenye familia ya rais wa Afghanistan, Hamid Karzai. Sardar kutokana na ukaribu wake kwa kaka yake na rais Karzai, bwana Ahmad Wali Karzai, alikuwa miongoni mwa wazee wa kikabila ambao walikuwa wakikutana na Wali Karzai muda wowote ule kujadili masuala mbalimbali. Siku ya jumanne, Sardar mwenye umri wa miaka 40, alifika kwenye nyumba ya Wali Karzai pamoja na wazee wengine na alikuwa na faili ambalo alimtaka Wali Karzai aliangalie. Walienda chumba cha pili wakiwa peke yao ili waweze kuliangalia faili hilo lakini hazikupata dakika nyingi Sardar alichomoa bastola yake na kumpiga risasi mbili Wali Karzai. Walinzi wa Wali Karzai waliwahi kufika kwenye chumba hicho na kumuua kwa kumpiga risasi Sardar ambaye alikuwa akijiandaa kumpiga risasi ya tatu bwana Wali Karzai. Walinzi hao kwa hasira na kulipa kisasi cha kuuliwa kwa bosi wao, waliitundika maiti ya Sardar kwenye mojawapo ya majengo yaliyopo kwenye soko lililopo katikati ya mji wa Kandahar. Maiti hiyo iliachwa ikining'ia hapo juu ya ukuta kwa zaidi ya dakika 20 kabla ya kuondolewa. Jana yalikuwa mazishi ya Wali Karzai ambayo yaliongozwa na rais wa Afghanistan, Hamid Karzai. Maelfu ya watu walijitokeza kumzika Wali Karzai lakini mazishi yake yaliingia dosari wakati mtu mmoja alipojilipua ndani ya msikiti na kuwaua watu watatu akiwemo mmoja wa maimamu wakuu wa Afghanistan, watu wengine 15 walijeruhiwa. Taarifa zaidi zilisema kwamba mwanaume huyo aliingia msikitini wakati wa sala ya kuisalia maiti akiwa amevaa kilemba ambacho ndani yake alificha bomu alilolitumia kujilipua. Taarifa hizo ziliongeza kuwa mwanaume huyo alifanikiwa kuingia na bomu hilo msikitini kwa kujiingiza na kujifanya yupo katika msafara mmoja na maimamu kwakuwa maimamu huwa hawasachiwi. "Huwa tunawaheshimu watu wanaovaa vilemba, hatukukisachi kilemba chake kutokana na heshima zetu kwa watu wanaovaa vilemba, ameisaliti heshima hii kwa kuficha bomu kwenye kilemba", alisema Afisa Usalama mkuu wa Kandahar, Jenerali Mohammed Naim Momin. Naye rais wa Afghanistan, Hamid Karzai akiombeleza kifo cha kaka yake aliwataka Waafghanistan waache kuwaua ndugu zao. "Ni rahisi kuua na kila mtu anaweza, lakini mwanaume wa kweli ni yule anayeokoa maisha ya watu", alisema rais Karzai | ||
![]() Kieu Becker | Wednesday, July 13, 2011 10:52 PMStaili ya wanawake kuwaadhibu wapenzi wao kwa kuzikata sehemu zao za siri imeendelea nchini Marekani ambapo mwanamke mmoja nchini humo amejikuta akitupwa rumande kwa kuukata kwa kisu uume wa mume wake na kisha kuusagasaga kwa mashine. | |
| Mwanamke mmoja wa California nchini Marekani amejikuta akitupwa rumande baada ya kumlisha madawa ya kulevya mumewe, kumfunga kwa kamba na kisha kuukata uume wake kwa kisu na ili kuhakikisha kipande hicho cha uume hakitaungwa tena na madaktari alikidumbukiza kipande hicho cha uume kwenye mashine ya kusaga uchafu. Taarifa ya polisi ilisema kwamba siku ya jumatatu usiku, mwanamke huyo aliyetajwa kwa jina la Kieu Becker mwenye umri wa miaka 48, alimuandalia mumewe chakula ambacho alikiwekea madawa ya kulevya. Mumewe mwenye umri wa miaka 51 ambaye jina lake halikutajwa, alijihisi vibaya baada ya kula chakula hicho na haukupita muda mrefu alipoteza fahamu. Kieu alimburuza mumewe na kumlaza kitandani ambapo alimvua nguo zake zote na kisha kuifunga mikono na miguu yake kwenye kitanda. Kieu alisubiri mumewe apate fahamu kabla ya kuanza kumshambulia kwa kisu chenye urefu wa sentimita 25.4. "Alikuwa ameishazinduka wakati uume wake ulipokatwa", alisema msemaji wa polisi. Taarifa ya polisi ilisema kwamba Kieu alikichukua kipande cha uume wa mumewe na kukiweka kwenye mashine ya umeme ya kusaga taka ambayo huwekwa chini ya sinki la maji kwenye majumba mengi ya Marekani. Baada ya kuhakikisha kipande hicho cha uume kimesagwasagwa sana kiasi cha kuwa vipande vidogo vidogo, Kieu alipiga simu polisi na kuwajulisha kilichojiri. Polisi walipofika walimkuta mumewe akiwa bado kitandani mikono na miguu yake ikiwa imefungwa kwa kamba, alikuwa akivuja damu sana. Kieu alitupwa rumande akifunguliwa mashtaka ya kufanya ukatili, kuteka mtu na kumlewesha mtu kwa madawa ya kulevya ili kufanya kosa la jinai. Ili aachiwe huru kwa dhamana, Kieu alitakiwa kutoa dola milioni moja. Mume wa Kieu aliwahishwa hospitali ambapo alifanyiwa operesheni ili kuokoa maisha yake. Ingawa hali yake bado ni mbaya sana, madaktari wanaamini mwanaume huyo atapona. Kieu hakuleta upinzani wowote wakati alipokuwa akitiwa mbaroni na atapandishwa kizimbani siku ya jumatano. Taarifa zaidi zilisema kwamba Kieu na mumewe walifunga ndoa mwezi disemba mwaka jana na walikuwa kwenye harakati za kuivunja ndoa yao ingawa sababu ya mgogoro kwenye ndoa yao haikujulikana. | ||
![]() Baadhi ya wasanii wa kundi la Fish Group | Wednesday, July 13, 2011 5:01 AMKUNDI la sanaa za maigizo na filamu nchini la Fish Group linasaka wadhamini ili kuendelea kukuza vipaji vya wasanii wachanga na kuinua tasnia ya filamu nchini. | |
| Wakiongea na Kalimanzila wa Nifahamishe.Com ofisini kwao Magomeni jijini Dar es Salaam, jana viongozi wa kundi hilo, Hamis Yusuph na Juma Mwamwindi ‘Stopa’ walisema kuwa wanasaka wadhamini hao kwa kuwa mpaka sasa tayari wameishawaandaa vijana kwa kiwango kikubwa kwenye sanaa. Viongozi hao walisema kwamba kundi hilo limefanikiwa kuwaokoa baadhi ya vijana wa mtaani toka kwenye matendo mbalimbali ya uhalifu. “Lengo letu ni kukuza vipaji na kuendeleza sanaa hivyo tunaomba wadau kujitokeza na kutupa tafu ya kuendeleza gurudumu hili mpaka sasa tunajiendesha wenyewe bila wadhamini” alisema Mwamwindi ‘Stopa’. Mpaka sasa kundi hilo linawasanii 64 na linanolewa na walimu wazoefu wakiwemo Hamad Abdala ‘Mr.Eddo na Mode ambao ni wasanii wazoefu kwenye tasnia hiyo. Aidha waliongeza kuwa, malengo yao zaidi ni kuhakikisha mbali na sanaa ya maigizo na filamu pia wanataka kuwa na kundi la ngoma na sarakasi. Kwa upande wake mkuu wa nidhamu wa kundi hilo, Ramadhan Shaban ‘Max well’ alisema kuwa wamepata faraja kwa wazazi wa wasanii waliojiunga na kundi hilo kuwaunga mkono kwa kuwaruhusu watoto wao kufanya sanaa tofauti na zamani ambapo sanaa ilionekana kama uhuni. “Tunajisikia faraja wazazi kuikubali sanaa hivyo Tanzania tunakoelekea soko litakuwa zaidi ni kushirikiana kwa pamoja” alisema Max. Max aliongeza kuwa kama mtu atakuwa tayari kulidhamini kundi hilo basi anaweza kuwasiliana nao kwa simu hizi 0652513951 au 0719302000 ama anaweza kufika ofisini kwao Magomeni Mapipa, kituo cha mabasi cha Mapipa mkabala na Shibam Restaurant | ||
TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) Mkoa wa Temeke, imeanza kutoa mafunzo ya rushwa kwa walimu ikiwa ni maandalizi ya kufundisha somo hilo shule za sekondari. Hatua hiyo inafuatia mpango wa serikali kuliweka somo la rushwa kwenye mitaala ya sekondari, ili kufanya jamii kuwa na maadili mema ya kuchukia rushwa. Hata hivyo, walimu hao walisema licha ya kufundisha somo hilo shuleni, rushwa itaendelea iwapo mishahara itaendelea kuwa midogo. Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Temeke, Beutoz Mbwiga, alisema mafunzo hayo yatawasaidia walimu wanaofundisha somo la uraia kuwajenga wanafunzi wao kwa maadili, hivyo kuchukia rushwa. “Wanafunzi wakifundishwa kuhusu madhara ya rushwa wakiwa shuleni, wataichukia na kupambana nayo maishani mwao,” alisema Mbwiga. Mbwiga alisema athari za rushwa kwa sekta ya elimu, zimekuwa zikisababisha kushuka kwa kiwango cha elimu nchini. “Kiwango cha elimu kinashuka kwa sababu mitihani inaweza kuvuja kutokana na watendaji kupewa rushwa,” alisema Mbwiga. Aliongeza kuwa vurugu na migomo ya wanafunzi inayotokea kwa baadhi ya shule, ni mojawapo ya athari za rushwa. Mbwiga alisema sababu za kuwapo rushwa ni mmomonyoko wa maadili, kupenda kuishi maisha ya kifahari, kipato duni na kukosekana kwa utashi wa kisiasa. Kwa upande wake, Mwalimu wa Sekondari ya Temeke, Hilde Mchomba, alisema watu hawataacha kuchukua rushwa kama mishahara itaendelea kuwa midogo. “Hata kama tutawafundisha wanafunzi kuwa na maadili mema na kuchukia rushwa, lakini kama mishahara yao itakuwa haitoshelezi mahitaji watalazimika kuchukua ili kujikimu,” alisema mwalimu huyo. Mwalimu Mchomba alisema mafunzo hayo yanatakiwa kwenda sanjari na serikali kupanga viwango vya mishahara itakayowezesha wafanyakazi kujikimu kwa mwezi mzima, vinginevyo mapambano hayo hayatafanikiwa. Naye Mkuu wa Dawati la Elimu kwa Umma wa Takukuru Mkoa wa Temeke, Esther Mkokota, alisema wameanza kutoa mafunzo hayo kwa walimu 25. |
![]() Mbwa kama huyu alitumika kufanya mapenzi na mwanamke | Mwanamke mwenye umri wa miaka 43 wa nchini Ireland amefariki dunia baada ya kufanya mapenzi na mbwa. | |
| Taarifa zilizotolewa zilisema kwamba mwanamke huyo ambaye alikuwa ni mama wa watoto wa wanne ambaye jina lake halikutajwa alikutana na mwanaume mwenye umri wa miaka 57, Sean McDonnell kwenye mtandao wa Zoofili ambako walichati kuhusiana na kufanya mapenzi na mbwa. Baada ya wawili hao kukutana, mwanamke huyo alifanya mapenzi na mbwa wa McDonnell mwenye asili ya Ujerumani lakini muda mfupi baada ya kukamilika kwa tendo hilo mwanamke huyo alifariki dunia. Taarifa zaidi zilisema kwamba, mwanamke huyo alifariki dunia kutokana na aleji aliyoipata kutokana na mbegu za kiume za mbwa kuingia ndani ya mwili wake. Ingawa polisi walithibitisha kuwa tendo hilo lilifanyika kwa ridhaa ya mwanamke huyo, Sean McDonnell,amekamatwa na anashikiliwa na polisi kwa kosa la ukatili wa wanyama kwa kumlazimisha mbwa wake afanye mapenzi na mwanamke huyo. McDonnell huenda akahukumiwa kifungo cha maisha iwapo atapatikana na hatia | ||