Baadhi ya wahitimu wa sekondari ambao huomba kujiunga na Elimu ya Juu kila mwaka na idadi yao hukua kila mwaka, serikali iafanye jitihada za kuwakopesha vijana kama hawa bila upendeleo.
WANAFUNZI wanaotarajia kujiunga na vyuo vya elimu ya juu wameandamana hadi ofisi za Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, wakilalamikia kukosa mikopo ikiwa wana vigezo vyote vya kupewa mikopo hiyo.
Jana wanafunzi hao walifika eneo la Wizara hiyo majira ya saa 5 asubuhi wakitokea Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu iliyopo eneo la Msasani jijini Dar es Salaam
Wanafunzi hao walidai wamechukua uamuzi wa kuja wizarani hapo baada ya kutoridhishwa na majibu waliyopata katika ofisi hiyo na kufika hapo kwa lengo la kutaka kuonana na waziri mwenye dhamana hiyo ili awasaidie.
Wakilalama mbele ya vyombo vya habari wanafunzi hao walilalamikia hatua ya bodi hiyo kutowapa mikopo ikiwa wengi wao wanatokea kwenye familia duni na watoto wa wakulima na kusikitishwa kunyimwa mikopo hiyo ikiwa wanavigezo vyote vya kupewa mikopo hiyo .
Wakizungumza na mtandao hjuu wanafunzi watatu ambao waliomba wasichapishwe majina yao walisema, wao wana sifa zote kwa kuwa walifaulu kiwango cha juu kwa kupata daraja la kwanza katika mitihani ya kidato cha sita na wamechaguliwa kujiunga na chuo kikuuu cha Dar es Salaam na endapo watakosa mikopo hiyo watashindwa kusoma kwa kuwa wazazi wao wana kipato duni kabisa
Kwa upande wa pili, Msemaji wa bodi hiyo, Cosmas Mwaisobwa, alisema ugawaji mikopo kwa mwaka huu ulizingatia mahitaji ya mwanafunzi na si ufaulu kama ilivyozoeleka.
Alisema serikali iliweka vipaumbele watakaosoma masomo ya elimu ya afya, sayansi ya kilimo, ualimu wa masomo ya sayansi, hisabati na uhandisi hao watapata mikopo kwa asilimia 100
Vilevile alisema imezingtia wanafunzi wenye mahitaji maalum kwa kuangalia vigezo kama mayatima na wale kweli waliothibitishwa kuwa wanatoka kwenye familia duni kwa kutibitishwa kwa kuambatanisha vielelezo kwenye barua ya mtendaji wa serikali ya mtaa kwenye barua ya mkopo
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni