MWANAMKE mmoja amejikuta akilazimika kulia isivyo kawaida katika msiba wa jirani yake baada ya ndugu wa marehemu kumshambulia na kumtuhumu kwa maneno kuwa alihusika kutengeneza kifo cha ndugu yao huyo
Msiba huo ambao ulihudhuriwa na mwandishi wa mtandaio huu, huko maeneo ya Tabata Kimanga jijini Dar es Salaam jana
Awali mtandao huu ulifahamishwa kuwa, marehemu aliwahi kutupiana viswahili vikali yaani kugombana miezi minne iliyopita huku kila mmoja akimtupia maneno makali mwenzie na kudaiwa Anastazia alitamka maneno ambayo yalikaririwa kuwa “UTANIJUA MIMI NANI”na maneno hayo ndiyo yaliyomuingiza matatani baada ya kutokea kifo hicho
Imedaiwa kuwa wawili hao walikuwa na ugomvi ambapo ilidaiwa marehemu alikuwa akijihusisha na mapenzi na mume wa Anastazia na kuthibitishwa hilo na mwenye mali na ndipo ugomvi kati yao ulianza
Imedaiwa mwenye mali aligundua hilo kupitia ujumbe mfupi wa maneno kwenye simu ya mkononi ya mume wake na kugundua na alipombana mume wake alikiri kuwa na mahusiano na marehemu huyo na kudaiwa Anastazia kumfata ana kwa ana binti huyo akiwa na Shangazi yake mlezi kumuealeza bayana kuwa aachane na mume huyo na marehemu kudaiwa alikana na kuanza kumtukana matusi ya nguoni hadharani Anastazia na kupelekea kukua kwa ugomvi huo
Imedaiwa na mmoja wa majirani wa karibu na familia ya marehemu kuwa, ugomvi huo ulikuwa na kupelekea sakata hilo kuonekana kushabikiwa na hata baadhi ya ndugu wa marehemu kuwa kumtetea ndugu huyo ili hali wanafahamu kuwa anatenda makosa
Imedaiwa kuwa, marehemu alikuwa ni mwanafunzi aliyekuwa akichukua Shahada ya Uchumi na alifariki mwishoni mwa juma lililopita kwa ajali wakati alipokuwa akirudi kutokea mkoani Pwani akiwa na gari dogo na kugongana uso kwa uso na gari nyingine na kupoteza maisha akiwa hospitalini kwa matibabu
Hivyo kutokana na kifo cha ghafla cha marehemu huyo, anastazia anatuhumiwa kuhusika na vitendo vya ushirikina kusababisha ajali hiyo na ndugu kumshambulia kwa maneno na kumtuhumu uchawi licha ya kuwa yeye mwenyewe anakana kuhusika na kifo hicho
Imedaiwa kuwa Anastazia ni mfanyakazi wa Shirika binafsi nchini na mume wake akiwa ni mfanyakazi wa Benki ya Exim ni majirani wa karibu na familia ya marehemu
Hadi NIFAHAMISHE inaiondoka eneo la tukio majira ya saa 2 usiku iliacha mwanamke huyo akiwa msiba hapo kama kawaida huku akifarijiwa na baadhi ya majirani na kubaki na hudhuni na kujilaumu kutokana na kauli yake hiyo ya hasira aliyoitoa awali na kudai hakuhusika kwa namna yoyote kusababisha kifo hicho
“Kwani mimi nilishapuuzia ugomvi huo, toka mume wangu akiri kuwa alishirikia mara moja mapenzi na binti huyo na kuniomba msamaha mara kadhaa, nilishamsamehe marehemu siku nyingi, japo yeye alikuwa akinionyesha shari kwangu, sijahusika kwa kweli kifo chake ni mipango ya Mungu tu, siwezi kabisa ushirikina kwani nimempokea YESU siku nyingi ndiye anayeniongoza” alidai Anastazia wakati akizungumza na NIFAHAMISHE
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni