Jumatatu, 9 Aprili 2012

KANUMBA KUZIKWA KESHO JUMANNE MAKABURI YA KINONDONI BAADA YA KUAGWA VIWANJA VYA LEADERS. MAMA MZAZI AMEBARIKI WAZO HILO.


Mama mzazi wa Steven Kanumba anayeitwa Flora Mtegoa (katikati aliyeshika tama), akiwa amezungukwa na ndugu,jamaa na waombolezaji wengine mara baada ya kuwasili nyumbani kwa Marehemu Sinza-Vatican.Picha kwa hisani ya Shamim Mwasha at 8020 Fashions Blog
Steven Kanumba, muigizaji ambaye bila shaka tunaweza kusema ndiye alikuwa maarufu zaidi miongoni mwa waigizaji wa filamu za kitanzania(Bongo Movies) alifariki majuzi alfajiri kuamkia Jumamosi katika mazingira ambayo bado yanatatanisha na bado polisi wanaendelea na uchunguzi ingawa taarifa ya uchunguzi wao wa awali, iliyotolewa na RPC wa Kinondoni,Charles Kenyela, inaonyesha kwamba huenda marehemu amefariki kutokana na matumizi mabaya (alcohol abuse) ya pombe kali aina ya Jack Daniels.
Taarifa hiyo inafuatia mahojiano kati ya Polisi na muigizaji mwingine Elizabeth Michael “Lulu” ambaye inaaminika ndiye alikuwa na Marehemu ambapo awali kabla mauti hayajamkuta palitokea kutoelewana baina yao.Kwa mujibu wa maelezo ya Lulu, Kanumba alikuwa ametumia kinywaji hicho kwa wingi ana wakati wakiendelea na malumbano, alianguka na kujigonga katika ukuta wa chumbani hapo.
Hata hivyo, taarifa ya kitabibu(Post Mortem) kuchunguza chanzo cha kifo chake  bado haijawekwa wazi na  inatarajiwa kufanyika hivi leo(Jumatatu) na ukimalizika basi ndipo taarifa rasmi itatolewa na hivyo kubariki rasmi kuendelea kwa shughuli za mazishi hapo kesho
Read more: BongoCelebrity

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni