Ijumaa, 12 Agosti 2011

HATI YA MASHTAKA YA WAKILI MAARUFU YAREKEBISHWA, POLISI BADO WAENDELEA KUMSHIKILIA.

Wakili Median Mwalle

Peter Saramba, Arusha
UPANDE wa mashtaka tayari imefanyia marekebisho na kuwasilisha mahakamani hati ya mashtaka dhidi ya wakili maarufu nchini, Mediam Mwale, anayekabiliwa na madai ya kujihusisha na uingizaji zaidi ya Sh18 bilioni nchini kinyume cha taratibu.Hati hiyo ilirejeshwa na kupokelewa kwenye masjala ya mahakama juzi, lakini haikuweza kusomwa mbele ya hakimu kutokana na mshtakiwa kutofikishwa mahakamani baada ya kulazwa hospitalini.

Hakimu Mkazi Mfawidhi Mahakama ya Mkoa wa Arusha, Charles Magesa, Agosti 9, mwaka huu alikataa kupokea hati ya awali iliyokuwa na mashtaka 13 iliyosomwa na Wakili wa Serikali, Velitas Mlau, kutokana na kujaa makosa ya kisheria.

Miongoni mwa makosa ya kisheria yaliyotajwa na Wakili wa utetezi, Loomu Ojare, ni hati hiyo kutotaja wazi wazi jina la kampuni, taasisi, shirika wala mtu aliyetoa au kumpa mshtakiwa fedha zinazodaiwa kuingizwa nchini kinyume cha sheria.

Wakati huohuo, habari za uhakika zilizothibitishwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Thobias Andengenye, zinasema wakili huyo alipelekwa hospitali baada ya kulalamika kujisikia vibaya.

“Ingawa sijajua kwa usahihi nini tatizo linalomkabili hadi niwasiliane na mamlaka husika hospitali ya serikali alipolazwa, lakini ni kweli tulimpeleka Mount Meru baada ya kusema anajisikia vibaya,” alisema Andengenye.

Andengenye lisema hadi jana alikuwa hajapata taarifa iwapo wakili huyo bado yupo hospitali au ameruhusiwa na kuahidi kufuatilia.
Juhudi za kupata taarifa rasmi za tatizo linalomsumbua Mwale kutoka kwa madaktari wa Hospitali ya Mount Meru, zilikwama baada ya wahusika kugoma kulizungumzia, huku akitupa suala hilo kwa polisi.

“Kweli tumempokea na kumpa huduma ya afya mtu huyo unayemtaja. Lakini siwezi kuzungumzia zaidi suala hilo kwa sababu liko mikononi mwa polisi. Pia, siwezi kueleza tatizo linalomkabili kwa sababu ni kinyume cha taratibu na sheria za kitabibu kutaja siri ya mgonjwa, labda kama yeye atakuwa tayari kusema,” alisema mmoja wa madaktari kwa sharti la kutotajwa.


Polisi aliyekuwa zamu kumlinda Wakili Mwale hospitalini hapo aligoma kumruhusu mwandishi wa habari hizi, kumwona au kuzungumza naye huku akisisitiza lazima kipatikane kibali kutoka kwa Kamanda wa Polisi Wilaya (OCD) au mkoa (RPC

Alhamisi, 11 Agosti 2011

PICHA YA LEO; COROLLA YA NG'OMBE.

Corolla  ya kienyeji huko nchi za wenzetu.

MAKAMPUNI YA MAFUTA YASALIMU AMRI KWA SERIKALI

UPATIKANAJI wa bidhaa ya petroli kwa jana ulikuwa bado mgumu kutokana na baadhi ya kampuni kuendelea na msimamo wa kugoma kusambaza bidhaa hizo.

Msimamo huo ulionesha kuwa mgomo uliokuwapo ni wa kujaribu kutengeneza mazingira ya uhaba wa nishati hiyo kwa kuchelewesha utoaji wake kwa sababu mbalimbali.

Katika maghala ya kampuni zinazosambaza mafuta zilizoko Kurasini, Dar es Salaam, gazeti hili lilishuhudia kampuni mbili ambazo licha ya kuagizwa na Serikali kusambaza bidhaa yake ya petroli lakini hazikutii agizo hilo.

Kampuni ya Engen na BP maghala yake hayakuwa na hekaheka za magari kama ilivyokuwa kwenye maghala ya kampuni zingine, ambako jana malori yalijazana kusomba bidhaa hiyo.

Gazeti hili lilitaka kujua sababu ya Engen kutotoa huduma, lakini walinzi waliokuwa getini walimwonesha mwandishi jina la Duncan Malashika, kuwa ndiye atazungumza na wanahabari juu ya suala hilo.

“Sisi watu wa Utawala wametuachia jina hili, kuwa mkija wanahabari, tuwaeleze kuwa huyo ndiye Meneja wa Kampuni na amekuja nchini na ataitisha kikao cha wanahabari,” alisema askari aliyekuwa getini.

Kwa upande wa kampuni ya BP Tanzania Limited ambayo ni mbia wa Serikali ya Tanzania yenye hisa asilimia 51, licha ya kuwapo malori ya petroli za kampuni hiyo, lakini hadi saa nane mchana hakukuwa na gari ambalo lilikuwa limetoka na mzigo.

Hakuna Ofisa wa Kampuni hiyo aliyekuwa tayari kuzungumza, huku walinzi wa kampuni hiyo wakidai kuwa wahusika walikuwa kwenye kikao na wakatoa namba ya simu ya mhusika ambaye hata ilipopigwa haikupatikana.

Kwa upande wa maghala ya Oil Com, magari yalikuwa yanapakia mzigo na kutoka, lakini mengi yalionekana ni ambayo yanapeleka mzigo nje ya nchi. Baadhi ya madereva wa magari yanayosambaza mafuta nchini ambao wananunua bidhaa hiyo kutoka Oil Com walilalamika kuwa tangu Alhamisi wiki jana wako hapo lakini hawajapata mzigo.

“Leo wanatoa mafuta lakini wanatoa kipaumbele kwa magari yanayopeleka mzigo nje, mimi niko hapa tangu Alhamisi sijapata mzigo,” alisema Hemed Said ambaye ametoka Singida.

Malalamiko kama hayo pia yalitolewa na dereva Ramadhan Ali aliyetoka Mbeya ambaye alisema Oil Com licha ya kutoa mzigo, lakini magari yanayosambaza mzigo ndani ya nchi si mengi yanayopewa mzigo.

Lakini kwa upande wa maghala ya GBP, Orxy na CamelOil, magari yote ya ndani na nje yalikuwa yanatoa mzigo hali iliyoonesha kuwa hawakuwa na tatizo. Mkurugenzi Mtendaji wa CamelOil, Abdallah Nahd, alisema walianza kutoa huduma hiyo tangu saa 12 asubuhi jana.

Nahd alisema walisitisha kutoa huduma hiyo baada ya kutofautiana kwa kiasi fulani na Serikali, lakini kutokana na hatua iliyofikiwa, walisitisha mgomo kwa kuwa wako chini ya Serikali, hivyo hawana mamlaka yoyote.

Alisema kutokana na hali hiyo, walianza kutoa mafuta hayo ambapo kwa muda huo alipokuwa akizungumza na vyombo vya habari (saa 8.30 mchana), zaidi ya malori 100 yalikuwa yamepakia na kuondoka na mafuta.

Hali ilivyokuwa vituoni Magari na watu wengi waliokuwa na vidumu, bado walionekana wakigombea kupata mafuta hayo katika baadhi ya vituo vilivyoanza kuuza.

Baadhi ya vituo vililazimika kuomba ulinzi wa polisi ambao walisimamia uuzaji wa huku wengi wakipewa masharti ya kununua lita zisizozidi tano ili angalau kila mtu apate.

Gazeti hili lilipita katika kituo cha CamelOil Manzese na kukuta msongamano huo uliowalazimu walinzi wa kituo hicho kuingilia kati na kuweka utaratibu wa kuuziwa.

Kituo cha OilCom cha Big Brother Manzese, hali ilikuwa mbaya zaidi na kusababisha msongamano wa magari hadi eneo la barabara ya Morogoro na kusababisha foleni kutokana na eneo hilo kuwa makutano na barabara ya Mabibo. GAPCO eneo la Posta Mpya, magari mengi yalikuwa kwenye foleni yakisubiri kupata huduma hiyo.

Vituo ambavyo jana vilianza kutoa huduma ni vya kampuni za CamelOil, Orxy, Gapco, Lake Oil, Kobil na baadhi ya vile vya OilCom ambavyo watu wenye vidumu walijazana huku foleni za magari nazo zikiongezeka.

Kutokana na nishati ya mafuta kuendelea kuwa haba, baadhi ya vijana ambao walikuwa wanauza mafuta hayo uchochoroni, waliyauza kwa Sh 4,000 badala ya Sh 2004 kwa lita.

Mwandishi wa habari hizi, alishuhudia wafanyabiashara wa bodaboda wakinunua mafuta hayo katika eneo la Kipawa kando ya kituo cha mafuta cha OilCom. “Sisi tutaendelea kuwa na mafuta hayo si unaona tuko kando ya kituo, tunajua namna ya kuyapata,” alisema muuzaji wa mafuta hayo.

Mgomo huo unatokana na hatua ya Serikali kupitia kwa Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji (Ewura) kutangaza kushusha bei hiyo baada ya Serikali kuondoa baadhi ya tozo na kodi kwa bidhaa hizo.

Katika agizo la Ewura, bei ya petroli kwa bei elekezi ni Sh 2,004 wakati dizeli ni Sh 1,911 na mafuta ya taa bei kikomo ni Sh 1,890. Bei hizo zinatokana na Serikali kupunguza zaidi ya Sh 200 kwa lita. Hatua hiyo ya Serikali iligomewa na wafanyabiashara wa mafuta na wengi wao kuamua kufunga vituo vya kuuzia mafuta kwa kisingizio kuwa hawana bidhaa hiyo muhimu kwa uchumi wa Taifa.

Mkuu wa Mawasiliano wa Ewura, Titus Kaguo alipoulizwa kuhusu hali ya jana, alisema walikuwa bado wanafanya tathmini kujua ni nani wanaendeleza nmgomo ili hatua zichukuliwe. Kuhusu mafuta yaliyiodaiwa kuwa yanapelekwa nje, alisema si kweli kwani mafuta yaliyotolewa jana ambayo aliyatolea mchanganuo yalikuwa ni yaliyowekwa vinasaba ili yauzwe ndani ya nchi.

Mchanganuo Kwa mujibu wa Kaguo, hadi saa 10 jioni, tayari jumla ya lita 5,401,600 za mafuta mbalimbali jamii ya petroli zilishapakuliwa kutoka maghalani na kupelekwa katika vituo mbalimbali vya kuuza kwa reja reja. Alisema hadi wakati huo, lita 1,821,600 za petroli zilishapakiwa.

Alisema lita 3,309,500 za dizeli zilipakuliwa huku matumizi ya siku yakiwa ni lita milioni tatu, wakati huo za mafuta ya taa zikiwa ni lita 270,500 na matumizi ya siku yakiwa lita 615,000.

Kwa mujibu wa mchanganuo huo, kampuni ya BP ilichukua mafuta lita 402,000 za dizeli na petroli lita 48,000; CamelOil lita 416,500 za petroli na 629,000 dizeli. 0ilCom ilichukua lita 382,000 za dizeli na 353,000 za petroli, huku Total ikiwa na lita 163,000 za dizeli na 0ryx lita 91,000 za dizeli na lita 44,000 za petroli. Mchanganuo huo ulionesha pia kwamba kampuni ya Gulf Bulk ilikuwa na lita 272,000 za dizeli na 86,000 za petroli wakati Engen ikichukua lita 175,000 za dizeli na 64,000 za petroli.

Kampuni ya MGS International ilichukua mafuta lita 116,000 za petroli na 232,000 za mafuta ya taa wakati NatOil ilichukua lita 79,000za dizeli, 55,000 za petroli na 4,000 za mafuta ya taa. LakeOil ilikuwa na lita 279,000 za dizeli na 65,000 za dizeli huku Gapco wakiwa na lita 418,100 za petroli, 348,000 za dizeli na 34,500 za mafuta ya taa na Kobil ikiwa na lita 37,000 za petroli na 431,000 za dizeli.
Harakati za kupata mafuta.
Camel Oil



Kampuni ya Hass ilichukua lita 37,000 za petroli na lita 431,000 za dizeli. Wakati huo huo, Kaguo alisema meli mbili za mafuta zilikuwa zimetia nanga bandarini Dar es Salaam, ambapo moja ilipakua lita milioni 15 za dizeli na nyingine hadi jana alasiri ilikuwa ikiendelea kupakua lita milioni 16 za dizeli na milioni 19 za mafuta ya ndege

Jumatano, 10 Agosti 2011

WAKILI MAARUFU ARUSHA ASOMEWA MASHTAKA YA KUTAKATISHA FEDHA-MONEY LAUNDERING.

 Wakili Maarufu jijini Arusha Medium Mwalle amefikishwa mbele ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha na kusomewa mashitaka 13 yanayodaiwa kumkabili likiwamo la kukutwa na kiasi kikubwa cha fedha kwenye kaunti zake zisizo na maelezo sahihi (Money Laundering).
Wakili Median Mwalle wa nne toka kushoto mwenye suti nyeupe akiwa na Askofu Simon Makundi wa kanisa la Anglikan Arusha wa kwanza kushoto na Wakili Ezra Mwaluko wa pili toka kushoto wakati wa misa ya mapatano ya mgogoro wa kanisa mwaka jana, Mwalle alimwakilisha Askofu na Mwaluko aliwawakilisha waumini mahakamani.


Mwale alisomewa mashitaka hayo 13 jana mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Arusha, Charles Magessa na Mwendesha Mashitaka wa Serikali aliyejulikana kwa jina moja la Mallya.

Mara baada ya kusikiliza hoja za pande zote mbili katika shauri hilo Hakimu Magessa alitupilia mbali hoja za upande wa Mashitaka akidai maelezo katika hati hiyo hayakueleza wazi. Akisoma uamuzi mdogo baada ya kuahirisha kwa muda kesi hiyo, Magessa alidai, hundi zinazodaiwa kutumika kutoa na kuingiza fedha kwenye akaunti za mtuhumiwa hazikuelezwa zimetoka wapi na kwa nani, “Hati ya Mashitaka inatakiwa ieleze au itoe maelezo mafupi kulingana na mashitaka na vipengele husika. Kama haitafanyika hivyo ni wazi mwisho wa siku nguvu ya Mahakama hupotea bure,” alidai Magessa na kuongeza, “Lakini sheria inasema lazima hati ya mashitaka iwataje au imtaje mtu ili ajulikane ni nani. Hatua hii inasaidia mlalamikaji kujua nani anayemlalamikia.”

Alidai kutokana na hatua hiyo Hakimu Magessa alidai, kwamba Mahakama yake haitayapokea mashitaka hayo kuanzia la tatu hadi la 11 kutokana na makosa yalijitokeza, “Mashitaka haya kuwa ni makubwa, hivyo napendekeza yarudishwe yaandaliwe upya ili kusiwapo na mashaka kwenye hatui mpya itakayoletwa siku yoyote skutoka upande wa Serikali. “Sasa basi haitakuwa busara kuendelea na mashitaka ya haya hivyo naamuru mashitaka ya kwanza hadi la pili nayo yarudishwe yaje pamoja. Mtuhumiwa arudishwe mikononi mwa polisi kwani wao ndio wanataratibu za kumshikilia,” alidai Magessa.

Mwalle moja ya Mawakili waliojijengea umaarufu mkubwa anadaiwa kukamatwa Agosti 2, 2011 na polisi wa kimataifa wa Interpol, ambapo hadi jana tayari alikuwa amefikisha wiki moja akiwa anashikiliwa na polisi.

Aidha, hati ya mashitaka haikuweza kupatika kwa ajili ya kuandika kwa usahihi mashitaka hayo 13 kutokana na madai kwamba kulihitajika marekebisho.

Nje ya Mahakama

Hali ya hewa ilionekana kuwa nzito zaidi kwa baadhi ya mawakili waliokuwa kwenye viwanja hivyo kwa ajili ya kujua hatima ya wakili mwenzao. Baada ya kutoka nje ya jengo la mahakama, wakili huyo alishindwa kuficha sura yake baada ya kukutana na kamera ya televisheni moja hapa nchini. Hatua hiyo ilimfanya Mwalle kuomba mpiga picha asiendelee kupiga picha kwa madai kuwa "atamharibia". Alilazimika kusimama kwa kuipa mgongo camera huku akiwa amezungukwa na maofisa wa polisi na usalama wa Taifa. Mara baada ya kuona wanacheleweshwa maofisa hao walimwamuru kuanza kutembea licha ya kamera hiyo kummulika.

WAUZA MAFUTA WABANWA, WAPEWA MASAA 24 WATOE HUDUMA.

Mussa Juma, Dodoma
na Boniface Meena na Claud Mshana, Dar
MAMLAKA ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (Ewura), imetoa amri kwa kampuni nne kubwa zinazosambaza mafuta kurejesha huduma hiyo mara moja huku ikizitaka kujieleza, kwa nini zisichukuliwe hatua za kinidhamu kwa kushindwa kutimiza wajibu wao kwa mujibu wa leseni zao
za biashara.Kampuni hizo ni pamoja na BP ambayo Serikali inamiliki nusu ya hisa pamoja na Engen, Oil Com na Camel. Mbali ya maagizo hayo mawili, Ewura pia imezitaka kampuni hizo kuhakikisha kwamba zinaendelea kutoa huduma hiyo bila kubughudhi mfumo wa usambazaji mafuta nchini.

Aidha, Ewura pia imetoa leseni kwa Shirika la Taifa la Maendeleo ya Petroli (TPDC) kuingiza mafuta kuanzia jana ikisema ombi lake la kupatiwa leseni ya kuuza ndani ya nchi litashughulikiwa baada ya kubainisha miundombinu yake.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Dar es Salaam jana, Mkurugenzi Mkuu wa Ewura, Haruna Masebu alisema kisheria, amri hiyo (Compliance Order) ni sawa na agizo la Mahakama Kuu na kwamba wahusika hawana budi kutii. Mbali na kampuni hizo, Masebu alisema pia kwamba kampuni nyingine ndogo za mafuta zinachunguzwa na zitakazothibitika kuhusika katika mgomo wa kutoa huduma hiyo muhimu ya nishati, zitachukuliwa hatua.

Agizo la Ewura limekuja sambamba na hatua ya Bunge kusitisha shughuli yake kawaida jana ambayo ilikuwa ni mjadala wa hotuba ya makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Viwanda na Biashara na kujadili mgomo wa wafanyabiashara ya mafuta ambao mpaka jana, walikuwa wamesitisha uuzaji wa bidhaa hiyo katika vituo mbalimbali nchini na kusababisha kusimama kwa shughuli mbalimbali za kiuchumi na kijamii. Ombi la kujadili suala hilo liliwasilishwa bungeni na Mwenyekiti wa Kamati ya bunge ya Nishati na Madini, January Makamba.

Baada ya mjadala uliochukua sehemu kubwa ya shughuli zake za jana, Bunge liliazimia kwa kauli moja kwamba Serikali ihakikishe amri hiyo ya Ewura kama ilivyowasilishwa kwake na Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja inatekelezwa.

Akihitimisha hoja yake, Makamba alitoa hoja kwamba sheria ifuate mkondo wake na kuitaka Serikali kuchukua hatua kwa kampuni zitakayokaidi agizo hilo mara baada ya muda uliotolewa kumalizika. Pia alisema: “Kwa sababu tatizo hili ni la nchi nzima na watakaoanza kunufaika ni wakazi wa Dar es Salaam, Serikali ihakikishe kuwa na mikoani mafuta yanapatikana kama kawaida.”

Michango ya wabunge
Awali, akichangia hoja hiyo, Makamba alisema tangu Ewura ilipotangaza kushuka kwa bei ya mafuta, hali imekuwa mbaya lakini kabla ya hapo mafuta yalikuwa yanatosha. Alisema hatua ya kushuka bei ya mafuta ililenga kuwapunguzia wananchi mzigo na ni suala lililopitishwa na wabunge na kuelezea kushangazwa kwake na jinsi usimamizi wa sheria ulivyochelewa kutekelezwa.

Makamba alisema nchi imekuwa kwenye mgawo wa umeme kwa muda mrefu lakini nishati ya mafuta ni muhimu zaidi kuliko umeme: “Hili ni tatizo kubwa, lazima Serikali ionyeshe ipo na ina uwezo wa kusimamia, watu sasa wananunua kwa mfano, Korogwe lita moja ya mafuta ni Sh3,000, Handeni Sh4, 000 naambiwa Tabora hakuna kabisa mafuta... hili ni jambo la hatari kwa usalama wa nchi,” alisema Makamba na kuongeza:

“Tunataka kuiona hali ya mafuta inarejea kama ilivyokuwa awali, kama tutashindwa kufanya uamuzi, nchi itasimama, wananchi hawatuelewi. Chama Cha Mapinduzi (CCM), ndicho kimeunda Serikali, lakini suala hili la mafuta linavyofanyika sivyo wananchi walivyotegemea. Mheshimiwa Waziri sema kitu, Mheshimiwa Waziri Mkuu sema kitu, kwa sababu ipo Ewura lakini Serikali ipo, haiwezekani siku saba nzima hatujasikia Waziri Mkuu amesema kitu, wala Waziri amesema kitu kwa nini? Hili jambo baya, tunaomba muonyeshe mpo na mnafanya kazi.”

Akichangia hoja hiyo ya mafuta, Naibu Kiongozi wa Upinzani Bungeni, Zitto Kabwe alitaka wafanyabiashara hao waagizwe kufungua vituo vya mafuta na kuendelea kutoa huduma mara moja na kwamba kama hawatafanya hivyo hadi jana saa 12:00 jioni, Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), livifungue na kuyauza kwa nguvu.

Alisema katika hali ya kawaida imezoeleka kuona wanaogoma ni wafanyakazi na hajawahi kutokea wafanyabiashara wakagoma: “Hatujasikia wafanyabiashara wamekata rufani tangu kushushwa bei au wamekwenda Tume ya Ushindani (FCC) kukata rufani. Wanataka kutuonyesha ubabe wao, wanataka kutumia jeuri ya fedha, Watanzania siku zote ni maskini jeuri, leo mafuta yatoke, Ewura waagize yatoke ikifika saa 12 jioni wamegoma basi wanyang’anywe leseni mara moja na JWTZ liingie na wafungue vituo mafuta yatoke.”

Zitto ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma (POAC), alisema bado Serikali ina haki ya kulinda maslahi ya raia wake akisema wafanyabiashara kwa kutumia umoja wao, wameamua kukiuka maagizo la Ewura.

Mbunge wa Mkanyageni (CUF), Habib Mnyaa alisema tatizo hilo linatokana na makosa yaliyoanzia bungeni akisema chombo hicho kimeshindwa kuisimamia Serikali ipasavyo: “Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini katika Bunge la Tisa, iliwahi kupendekeza kuwa Serikali kupitia TPDC, ianze kusimamia biashara ya mafuta, lakini haijatekeleza.”

Alisema umefika wakati Serikali ijue kwamba siyo kila wakati maagizo ya Benki ya Dunia (WB) na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), yana manufaa kwa nchi kama Tanzania, kwani Serikali kujitoa kwa asilimia 100 katika biashara ni makosa.

Mbunge wa Muleba Kaskazini, Charles Mwijage ambaye alijinasibu kuwa ni mtaalam katika sekta ya mafuta, alisema tatizo kubwa lililopo ni kanuni inayopanga bei. “Serikali imepotoshwa, siku ambayo tulipandisha bei ya mafuta ya taa niliwaambia Ewura wapime akiba ya mafuta ya taa iliyopo na watu ambao walipandisha siku ya pili tu walikuwa ni watu wa kukamatwa.”

Mbunge wa Ubungo, John Mnyika alisema ana ushahidi vigogo wa Serikali kuhongwa katika sakata la mafuta na kwamba hilo pia limefikia hapo kutokana na udhaifu wa Serikali: “Tusiiadhibu Ewura, kwani walitekeleza wajibu wao, lakini pia katika hili Takukuru wanapaswa kuchukua hatua ya kuchunguza kwani nina ushahidi viongozi na maofisa wa Serikali kuhongwa katika jambo hili.”

Alisema inashangaza kuona kwamba, Serikali ina hisa asilimia 50 katika Shirika la BP lakini pia shirika hilo linagoma kuuza mafuta wakati ni mali ya Serikali: “Tunamiliki asilimia 50 BP, tunamiliki asilimia 50 katika Tipper halafu tunaambiwa mafuta hakuna, Serikali yetu ipo wapi, nashauri Serikali kuchukuwa hatua.”

Mbunge wa Kibakwe, George Simbachawene aliitaka Serikali kuwafungulia mashtaka wauzaji hao kwa kuwa wamekiuka Sheria ya Ushindani wa Kibiashara (FCC). Alisema kuwa wametishia usalama wa nchi hivyo ni muhimu Watanzania wakasimama pamoja na kuonyesha uzalendo kwenye suala hilo.

"Tuchukue hatua zozote kwa kuwa tuko tayari kwa lolote. Lazima tuonyeshe ukakamavu kwenye hili kwani usalama wa nchi si kulinda tu, bali hata kumiliki nishati," alisema Simbachawene.

Mbunge wa Gando, Khalifa Suleiman Khalifa alisema kuwa uhuru waliopewa wauzaji wa mafuta wanautumia vibaya na hiyo ni changamoto kwa Serikali na kwamba inapaswa kulishughulikia suala hilo bila kuyumba kwa kuwa wananchi wana shida na ndiyo inayoweza kuwasaidia.

Mbunge wa Busega, Dk Titus Kamani alisema wafanyabiashara hao wanaiyumbisha Serikali na ndiyo maana wiki nzima wananchi wameteseka. Alisema vyombo vya dola vilipaswa kuhakikisha vina taarifa za kutosha kuhusu kiasi cha mafuta kilichopo ikiwepo kwenye maghala ili kutoa taarifa kamili ya hali ilivyo: “Hata mawasiliano yao vyombo vya dola vilipaswa kuyajua katika kipindi hiki.”

Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu alisema kampuni za mafuta zimepewa fursa ya kufanya biashara hiyo lakini si haki yao... “Ndiyo maana wanaweza kunyang'anywa leseni wakati wowote ule." Alitaka zinyang'anywe fursa hiyo kwa kuwa zinataka kuathiri uchumi wa nchi.

Mbunge wa Kigamboni, Dk Faustine Ndugulile alisema ni muhimu Serikali ikachukua hatua ndani ya saa 24 na kuhakikisha wananchi wanapata mafuta: “Tuwakague na tukikuta mafuta tuyachukue na tuwafutie leseni.”

Kwa upande wake, Mbunge wa Kinondoni, Idd Azzan alisema kama si Makamba kuomba suala hilo lijadiliwe, Serikali ilikuwa imelala: “Serikali ichukue hatua na mpaka kesho tatizo liwe limekwisha na kama itashindikana mawaziri waondoke kwa kuwa hawana kazi ni waoga.”

Mbunge wa Mbarali, Modestus Kilufi alisema kilichofanywa na kampuni hizo ni usaliti kwa taifa na kitawaharibia biashara yao: “Serikali ichukue hatua na kuwanyang'anya leseni kisha ichukue mafuta na kuyauza.”

Mbunge wa Musoma Mjini, Vincent Nyerere alisema katika suala hilo ndiyo sehemu Serikali inapotakiwa kujisafisha: “Tunahitaji hatua zichukuliwe. Tunahitaji kuona makali ya Serikali ili kuondoa dhana ya kuonekana kuwa ni legelege”.

Mbunge wa Tabora Mjini, Ismail Aden Rage alitaka sheria ya kuweka watu kizuizini irudishwe ili watu waache kuichezea Serikali kama mpira.

CHANZO; Gazeti la Mwananchi.

Jumatatu, 8 Agosti 2011

MUIGIZAJI MAARUFU NIGERIA SAM LOCO-EFE AMEFARIKI DUNIA, CHANZO CHA KIFO BADO HAKIJAJULIKANA.


Sam Loco-Efe is dead!
Veteran actor and comedian, Sam Loco-Efe was found dead in his hotel room in Imo State. The cause of his death has not been disclosed.


Sam Loco Efe


NIGERIAN popular actor and comedian, Sam Loco-Efe is dead. Efe was found dead in his hotel room on Orlu Road, Owerri, capital of Imo State, on Sunday August 7.

The Imo State Commissioner of Police, Mohammed Jingiri Abubakar, confirmed the death to journalists looking for clarification on the incident. He said the famous actor had been ill for sometime and had only come to the hotel to recuperate before continuing his entertainment business, before he suddenly died.

Abubakar said: “It is true. He died in Rapour Hotel in Owerri. We are in the process of going to mortuary now. We heard he had been sick for one week and he had just been discharged. He died last night. We will give you other details latter,” the police commissioner said.

The death was also confirmed by the Actors guild of Nigeria (AGN). The Guild’s president, Segun Arinze said in an interview: “Yes, it is true that Sam Loco passed away tragically in his hotel room. I will be making a statement on Monday, (August 8). I can’t say much now because I want to verify the detail.”

National Secretary of the AGN Chuma Onwudiwe also confirmed Efe’s death, saying: “Today is indeed a very sad day in Nollywood. I can confirm that the great Sam Loco is dead.”

A versatile actor and a polyglot, the late Efe spoke Igbo, Yoruba and Hausa fluently even though he hailed from Benin, Edo State in South-South geo-political zone.


Efe had performed in several movies, on stage and television for more than four decades. He was part of the Nigerian troupe at FESTAC 77, when Nigeria hosted the world in arts and culture at the National Theatre, Iganmu, Lagos.

The death of Efe marks another deplection in the ranks Nollywood family. A few months ago, one the veteran actors, Ashley Nwosu, who had been for sometime died, and about a month ago, another legendary entertainer Christy Essien-Igbokwe died.


The body of the deceased was removed and taken to the morgue of the Federal Medical Centre, Owerri, he said

IJUE MOCHWARI YA MAZAO GHALA LA MAZAO LINDI FARMERS NACHINGWEA

Sehemu ya ghala la kuhifadhia mazao Lindi Farmers, mazao mbalimbali ya msimu hupokelewa hapa kama korosho, ufuta na mbaazi. Mazao ambayo hayakuandaliwa vizuri kwa kufuata ubora wa kimataifa kuhusu kiwango cha unyevu au mchanganyiko usio zao husika, hupelekwa sehemu iitwayo mochwari kwa kuandaliwa upya. 

Hapa ni mochwari, wafanyakazi wakipepeta ufuta ili kuondoa vitu visivyotakiwa(reject)

Baadhi ya vitendea kazi vya mochwari.

Kushoto ni mashine ya kupimia unyevu wa zao husika, mfano ufuta unyevu husizidi asilimia 6.5, kulia ni mzani unaoweza pima uzito hata ule mdogo kabisa(micro scale).

Jengo la mochwari kwa nje mbele.

WAISLAM WAFIKISHA CHUNGU CHA NANE RAMADHAN HUKU BEI YA BIDHAA IKIWA JUU, WAFANYABIASHARA TUWE NA UTU MWEZI UPITE.

Waislam wakiwa kwenye sala ya Ijumaa.
Wakinamama wakichagua mafungu ya viazi huko soko la Mwanakwerekwe Zanzibar, fungu moja linauzwa shilingi elfu mbili, ndizi aina ya mkono wa Tembo inasemekana zimefikia shilingi elfu nne kila moja, tutafika kweli jamani!!!?


TAMWA, TGNP MPO!? MWANAUME AJINYONGA KUTOKANA NA MATESO YA MKE, HATARI!!!!!

Mkazi mmoja katika Mtaa wa NHC katika Mji wa Mugumu wilaya ya Serengeti wilayani Mara, Samson Kitoshi (32) amejinyonga hadi kufariki dunia kwa kamba chumbani kwake kwa kile alichodai kuwa: “Amechoka kupigwa na mkewe kila wakati.”
Mkurugenzi wa TAMWA Bi. Ananilea Nkya.
Tukio hilo lililovuta umati mkubwa wa watu, linadaiwa kutokea jana saa tano asubuhi. Akisimulia mkasa huo, mtoto wa marehemu (jina tunalihifadhi) alisema kabla ya kutokea kwa tukio hilo, mama yao alimpa Shilingi 1,000 akanunue sukari na vitafunwa, lakini asimpe baba yao chai... "Mama aliaga kuwa anakwenda Hospitali DDH kwa kuwa anaumwa. Baba akasema hatakunywa chai hiyo na kutuambia kuwa hatutamwona tena anatuaga na tusiingie ndani."

Marehemu baada ya kuingia chumbani kwake anadaiwa kuwa alifunga kamba juu ya dari na kujining'iniza hadi alipokata roho. Mtoto huyo wa darasa la tatu ambaye ana umri wa miaka 10 alisema hawakuweza kuingia ndani kama walivyoambiwa na baba yao, lakini baadaye aliamua kumwamsha akidhani kuwa amelala ili anywe chai ndipo alipokuta amening'inia. Alipiga kelele kuomba msaada.

"Baba alikuwa amevua shati akawa amening'inia chini kuna meza nikaweka stuli ili nifungue kamba sikuweza nikapiga yowe majirani wakafika wakasema ameshakufa," alisema.

Kuhusu migogoro ya ndani, mtoto huyo alisema kumekuwa na ugomvi wa mara kwa mara hasa ukisababishwa na mama yao ambaye anauza pombe ya kienyeji ya wanzuki anaporudi akiwa amelewa kwani humfanyia vurugu baba yao.

"Hivi karibuni baba alifikia hatua ya kumtaka mama aondoke amechoka na mateso anayomfanyia, lakini mama alikataa kuwa hawezi kutoka na kudai yeye ndiye atakayetoka," alisema. Ndugu wa Kitoshi ambaye anaishi katika Kijiji cha Morotonga alisema kuwa marehemu aliyekuwa akifanya kazi ya kusaga nafaka alikuwa akilalamika kupigwa na mkewe mara kwa mara.

"Huyu ni ndugu yangu hata leo amefika kwangu na akanikosa na kurudi nadhani alitaka kuniambia kitu. Baada ya muda nikapigiwa simu kuwa amekufa kwa kujinyonga, amechoshwa na kupigwa," alisema.

Kamanda wa Polisi Wilaya ya Serengeti, Paulo Mng'ong'o alijaribu kumtafuta mwanamke huyo kwa simu lakini mara baada ya kujitambulisha kuwa yeye ni OCD, mama huyo alikata simu.

Baada ya muda mama huyo alifika nyumbani na kumkuta mume wake akining'inia kwenye kamba. Huko alipokewa kwa maneno makali kutoka kwa wanawake wenzake waliokuwa na hasira baadhi wakisema: “Ulitaka afe ujitawale sasa amekufa tanua... unadanganya ulikuwa hospitali mbona umelewa..."

Maneno hayo makali yalimwingia mwanamke huyo kwani alikaa chini kisha akalala chali na kupoteza fahamu. Hakuweza kunyanyuka hadi alipopakiwa kwenye gari la polisi pamoja na mwili wa mumewe na kupelekwa hospitali.

Akizungumzia tukio hilo, Kamanda Mng'ong'o alisema polisi inalifanyia uchunguzi na kwamba itatoa taarifa kwa umma. Alisema wangefanya mahojiano na mke huyo wa marehemu baada ya kuzinduka kujua chanzo cha kifo hicho.Mwenyekiti wa Mtaa wa NHC, Elias Nyamraba alisema kuwa wanasubiri ndugu wa marehemu kwa ajili ya hatua nyingine ikiwemo ya mipango ya mazishi akisema Kitoshi ni mzaliwa wa Kijiji cha Issenye


source:wavuti.com

Jumamosi, 6 Agosti 2011

AL SHABAAB WAUHAMA MJI WA MOGADISHU.

Kikundi cha wapiganaji wa Kiislamu wa Somalia, al Shabaab, kinasema kuwa kimeondoka katika vituo vyake kadha ndani ya mji mkuu, Mogadishu.
Mogadishu, Somalia


Wakaazi wameiambia BBC kwamba waliona misafara ya wapiganaji ikiondoka katika mji huo.
Kuhama huko kunafuatia mapigano makali jana usiku.
Kikosi cha Umoja wa Mataifa kinachoisaidia serikali ya Somalia kimekuwa kikipigana na al Shabaab mjini Mogadishu katika siku za karibuni; ili kuweza kufikisha msaada wa chakula kwa wale walioathirika na ukame nchini Somalia.
Haijulikani kama wapiganaji hao wameondoka kabisa.
Msemaji wa serikali alielezea huo kuwa "ushindi wa dhahabu" kwa watu wa Somalia.
Lakini al Shabaab, ambayo inadhibiti sehemu kubwa ya kusini mwa nchi, ilisema wameondoka kufwatana na mikakati yao na iliahidi kufanya shambulio la kulipiza.
Baadhi ya wadadisi wanafikiri al Shabaab imepungukiwa na fedha kwa sababu wafadhili wao wa Arabuni wamewapunguzia msaada tangu al Shabaab kudhoofika kijeshi.
Wadadisi wanasema al Shabaab imewahi kuwahamisha wapiganaji wake mjini Mogadishu siku za nyuma, lakini safari hii inaonesha kuondoka kwao ni ushindi mkubwa kwa serikali

TIDO MHANDO NA JOSEPH WARUNGU WAULA AL JAZIIRA, KWELI MWENYE BAHATI HABAHATISHI.

Giant Arab Satellite television Al Jazeera has deployed former BBC editors Tido Mhando and Joseph Warungu to steer its Swahili Service Channel set to launch in 2012, a move set to create a seismic effect on the regional media landscape.
Mr.Tiddo Mhando.

The new satellite channel to be based in Nairobi, will target viewers mainly in East Africa and Great Lakes regions, where majority are Swahili speakers. There are more than 150 million Swahili speakers in the two regions, but the channel will target a few millions at its launch.Mhando and Warungu are household names in the region and the only ones to have held senior editorial management jobs at the BBC headquarters in London. “Mhando and Warungu are top names in journalism from the region, their presence in Al Jazeera Swahili will be going to be a vote of confidence for the channel,” said a top official familiar with the plans.

Officials in the media giant said the reaction in East And Central Africa on the news about the launch of the Swahili channel "has been great."

At the top of his BBC career, Mhando was the head of the Swahili Service, while Warungu was leading English to Africa Service at the station, and directly responsible for flagship radio Focus on Africa programme and Focus on Africa Magazine. Mhando started his careers as a radio DJ at the government-run Tanzania Broadcasting Corporation (TBC) in Dar es Salaam in early1980s. At the same times, he also reported for a number of broadcasters including Deutsche Welle, Voice of America and Kenya Broadcasting Corporation, known at that time as the Voice of Kenya.

Joseph Warungu (photo: BBC @ flickr)In 1985, he moved to BBC Swahili Service in Nairobi and 14 years later, he moved to London and became the first African to head the service, a job he excelled in. But he first gained his real field reputation during Kenya’s first multiparty elections in 1992 with his solid reporting and command of the language. Notably, Mhando interviewed all presidents in the East and Central Africa region.

In1990, Mhando fame reached its apex after he became the first journalist to report the disappearance and eventual death of the then Kenyan foreign minister, Dr Robert Ouko, and in January 2001 he was the last journalist to interview President Laurent Kabila of DR Congo. Their long and revealing discussion took place just weeks before his assassination.

In 2006, he retired from the BBC and joined TBC as the managing director, but four years later the government refused to renew his contract largely because of fallout with the politburo in the powerful ruling party Chama Cha Mapinduzi(Revolutionary Party) over TBC’s coverage of the 2010 elections.

On his part, Warungu, trained as high school Kiswahili teacher, worked his way up after working for government-owned Kenya Broadcasting Corporation and private Kenya Television Network.

In 1992, he joined BBC Swahili Service and 11 years later, he was appointed the head of the station’s African Service, replacing legendary African hand Robin White.

On his appointment, he said: "This is one of the most challenging and responsible jobs in the whole of African journalism. More than 20 million listeners all over Africa rely on the BBC to keep them in touch with the continent. I intend to build on the formidable reputation which Robin White has established for both programmes, strengthening our reporting of Africa and our links with partner stations."

Warungu has toured dozens of countries, including reporting from South Africa upon the release of Nelson Mandela in 1991 and United States when Barack Obama won US presidential race as well as covering several warzones.

This is not the first time the Arab channel is employing experienced BBC hands. With closure of BBC Arabic service in the 1990s, more than 250 journalists switched to the newly created Al Jazeera. Its English service has also hired a couple from the BBC, including Mohamed Addow and Yvonne Ndege who report from east and west Africa respectively


EWURA KUPIGA FAINI MILIONI 3 KWA WAFANYABIASHARA YA MAFUTA WAKOROFI.

 Mgomo uliofanywa na kampuni za mafuta kupinga kushushwa kwa bei ya bidhaa hiyo, umeibua hasira za serikali, ambapo sasa Mamlaka ya Udhibiti Huduma za Nishati na Maji (EWURA), imetangaza kumchunguza Mkurugenzi wa Kampuni ya Engen, Selan Naidoo, ili kumchukulia hatua iwapo atabainika kuendelea kutoa matamshi yanayolenga kuchochea mgomo huo.

EWURA imesema hatua hizo zitachukuliwa dhidi ya Naidoo, ikiwa ni pamoja na kumnyang’anya leseni ya biashara ya mafuta, kwa vile yeyote anayechochea wenzake kugoma anavunja sheria za nchi.

Kauli hiyo ilitolewa na Mkurugenzi Mkuu wa EWURA, Haruna Masebu, alipozungumza na waandishi wa habari ikiwa ni siku moja baada ya Naidoo kuipa serikali saa 24 kuangalia namna ya kufidia hasara watakayopata pindi wanapouza mafuta kwa bei elekezi la sivyo ataachana na biashara hiyo.

Masebu alisema mchakato ulioifikisha serikali kufikia maamuzi ya kushusha bei ya mafuta, ulifanywa kitaalamu na ulikuwa sahihi kwani ulizingatia sheria, ikiwa ni pamoja na kuwashirikisha wadau wote wa bidhaa hiyo. Kutokana na hilo, alisema kamwe hawawezi kumvumilia mtu yeyote anayechochea wenzake kuvunja sheria za nchi, “Tutaangalia kwa undani tabia ya kiongozi wa Engen. Akiendelea na matamshi ya kuvunja sheria za nchi, sheria itachukua mkondo wake, ikibidi tutamnyang’anya leseni,” alisema Masebu.

Pia alisema kampuni yoyote itakayobainika kuendelea kuuza mafuta kwa bei ya zamani, kila moja itatozwa faini ya Shilingi milioni 3 kwa kila siku hadi hapo itakaporekebisha bei hiyo.

Alisema pia wanazichunguza kampuni zote zinazoendelea kugoma kuuza mafuta na kwamba, kwa sasa wanajielekeza katika mikoa ya Mwanza na Manyara, ambako kunadaiwa kuwapo na mgomo baridi.

Vilevile, alisema watatembelea vituo vya kuuza mafuta kuhakikisha vinauza nishati hiyo kwa bei elekezi.

Alisema kwa mujibu wa Sheria ya Ushindani, ni marufuku kwa wafanyabiashara ya mafuta kukaa na kupanga bei, hivyo iwapo itathibitika jana walifanya kitendo hicho, watachukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria.

Masebu alisema katika kujibu malalamiko ya kampuni za mafuta, Bodi ya EWURA imeamua kufanya marekebisho kuhusu gharama anazotozwa mfanyabiashara kwa kuchelewa kupakua mafuta kutoka kwenye meli bandarini. Katika marekebisho hayo, sasa gharama za meli kukaa bandarini kwa ajili ya kupakua mafuta kutoka siku 3-15, hatalipa mfanyabiashara, badala yake, zitalipwa na serikali kupitia Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).



source: http://www.wavuti.com/habari.html#ixzz1UH8ZpSBJ

Ijumaa, 5 Agosti 2011

SEMINA YA UTAWALA BORA NDANI YA GHALA LA LINDI FARMERS NACHINGWEA JANA.

Mdau wa blogu yetu Hansom akiwa na meneja wa Lindi Farmers Ltd Danford Nguata wakijiandaa kutoa semina ya utawala bora kwa wadau wa mazao wilayani Nachingwea jana.
Afisa Ushirika wa wilaya kushoto. Mbaraka store keeper wa Lindi Farmers na Meneja wa kampuni ya Ulinzi ya SAJ mwenye kilemba. 
Mwenyekiti wa semina ndg Zablon, mwenye shati jeusi na tai.
Washiriki semina wakichangia mada.
Wadau wakisubiri semina ianze.

Alhamisi, 4 Agosti 2011

NYOTA WA SOKA WA JAPAN AFARIKI DUNIA.

Mcheza kandanda wa Japan Naoki Matsuda amefariki dunia siku mbili baada ya kupoteza fahamu uwanjani akiwa mazoezini ikidhaniwa ni matatizo ya moyo.
Naoki Matsuda
Naoki Matsuda


Matsuda aliyekuwa na umri wa miaka 34, aliyeiwakilisha Japan katika fainali za Kombe la Dunia za mwaka 2002, siku ya Jumanne alikimbizwa.
Alianguka na kuzimia akifanya mazoezi na klabu yake ya Matsumoto Yamaga, na tangu wakati huo hakuweza kurejewa na fahamu.
Meneja wa zamani wa timu ya taifa ya Japan, Philippe Troussier akitoa rambirambi zake kwa familia ya mchezaji huyo, alisema alikuwa mchezaji muhimu katika kikosi cha nchi hiyo kilichoshiriki Kombe la Dunia.
"Inasikitisha sana kuona mtu anafariki dunia akiwa na umri mdogo kama wake," Bw Troussier alieleza Shirika la Reuters.
"Ni pigo kubwa. Alikuwa kijana mzuri sana na nilikuwa karibu naye. Niko pamoja na jamaa zake katika msiba huu mkubwa."
Mashabiki, marafiki na wachezaji wenzake wa zamani, walikusanyika katika hospitali ya Matsumoto kumtakia apone haraka alipokuwa amepoteza fahamu.
Matsuda aliichezea Japan mara 40 na kushinda mataji mara mbili katika Ligi ya nchi hiyo katika kipindi cha miaka 15 cha uchezaji wake na timu ya Yokohama F-Marinos.
Mapema mwaka huu alijiunga na timu ya Matsumoto inayocheza ligi ya chini

RAIS WA ZAMANI WA MISRI AFIKISHWA KIZIMBANI AKIWA TAABANI KITANDANI.



Aliyekuwa rais wa Misri, Hosni Mubarak
Thursday, August 04, 2011 4:30 AMHata kama utakuwa madarakani na kwa kutumia nguvu zako madarakani kufanya ufisadi kwa kuiba pesa za wananchi na kutumia rushwa kuwanyima wananchi haki zao, ipo siku yote yataisha na utaanguka na kuwa mtu mwenye kudharauliwa na pesa zote ulizo nazo hazitatosha kunusuru maisha yako.
Hapa nazungumzia kesi ya aliyekuwa rais wa Misri, Hosni Mubarak ambaye enzi za utawala wake alikuwa ni mtu mwenye maguvu mwenye kuogopewa na kila mtu nchini Misri kutokana na ubabe wake, lakini jana aliingizwa mahakamani akiwa mdogo kama sisimizi akiwa hoi bin taabani akishindwa hata kusimama na kupelekea asomewe mashtaka akiwa kwenye kitanda cha hospitali.

Katika hali ambayo wananchi wa Misri waliifurahia ni kumuona kiongozi wao huyo wa zamani akiwa amevalishwa sare nyeupe ya magereza akiwa kwenye kizimba kilichozungushiwa machuma pamoja na wanae ambao wote wanatuhumiwa kwa makosa mbali mbali.

Kwa mara ya kwanza katika historia ya nchi za kiarabu kiongozi wa nchi amepandishwa kizimbani na wananchi wake, tukiacha mfano wa Saddam Hussein wa Irak ambaye alinyongwa baada ya kupatikana na hatia ya makosa yaliyokuwa yakimkabili.

Mubarak maisha yake yako hatarini kwani anatuhumiwa kwa mauaji ya watu zaidi ya 800 waliouliwa wakati wa maandamano ya kuuong'oa utawala wake. Mubarak anatuhumiwa kuamuru silaha za moto zitumike kukomesha maandamano ya wananchi waliouchoka utawala wake.

Mubarak huenda akahukumiwa kunyongwa iwapo atapatikana na hatia.

Mamilioni ya wananchi wa Misri walishuhudia LIVE kwenye luninga kubwa zilizowekwa mitaani, wakati mbabe huyo wa zamani akiwa mbele ya sheria.

Mubarak mwenye umri wa miaka 83 alikanusha mashtaka yote aliyosomewa mahakamani yakiwemo mashtaka ya mauaji na rushwa.

Kesi hii iliahirishwa hadi tarehe 15 mwezi huu ambapo Mubarak atarudi tena kizimbani.

Kesi hii ni somo zuri kwa wanasiasa mafisadi wa barani Afrika, Mubarak ananyea debe hivi sasa jela sio kwasababu ya shinikizo la mataifa ya nje bali ni nguvu za wananchi wale waliosema "Tumechoka sasa basi".

Mubarak ingawa anadaiwa kuwa na mamilioni ya dola kwenye mabenki ya nje ya nchi yake, hawezi tena kuyafaidi mamilioni hayo aliyodaiwa kuyaiba nchini kwake akiwaacha wananchi wake wa hali za chini wakiteseka.

Utawala wa Mubarak ulikuwa ni miaka 30, hivyo mafisadi jifunzeni kuwa ingawa mtatesa sana madarakani mkiyarudisha nyuma maisha ya wananchi wenu, ipo siku moja sheria itashika mkondo wake na dhamana ambayo mlipewa na wananchi lakini mkaitumia ndiyo itakayowatokea mbele zenu na kuwaangamiza

Jumanne, 2 Agosti 2011

WAHAMIAJI LIBYA WAKUTWA WAMEKUFA KWENYE MASHUA.

Wakimbizi wa Libya
Walinzi wa pwani huko Italia wamekuta miili ya watu 25 katika boti iliyokuwa imejaa wakimbizi wanaokimbia kutoka Libya.
Boti hiyo yenye mita 15 ilifunga gati katika kisiwa cha Lampedusa kusini mwa Italia iliyokuwa imebeba watu 271 waliookoka, shirika la habari la AFP liliripoti.
Miili ya watu hao 25 ilikutwa kwenye chumba chenye injini ya boti.
Maafisa walisema watu hao wameonekana kufariki dunia kutokana na kukosa hewa ya kutosha.
Maelfu ya wakimbizi kutoka Afrika magharibi wamewasili kwenye kisiwa hicho katika wiki za hivi karibuni.
Walinzi hao wa pwani waliingia katika boti hiyo siku ya Jumatatu na kugundua miili ya watu hao.
Vyombo vya habari vya Italia vimeripoti kuwa watu waliokuwa katika chumba hicho chenye injini walijaribu kutoka lakini walikwama kutokana na idadi ya watu waliokuwemo na huenda wakawa wamekabwa na harufu kali ya moshi kutoka kwenye injini.

MWANAUME AKUTWA NA VIA VYA UZAZI VYA KIKE.



Mkulima mmoja wa nchini India ambaye pia ni baba wa watoto wawili amewashangaza madakatri baada ya kugundulika mbali ya kuwa ni mwanaume rijali tumboni mwake ana viungo vyote vya kike vya kumuwezesha mwanamke kupata ujauzito.
Mkulima huyo aliyetambulika kwa jina la Ryalu aliwahishwa hospitali baada ya kusumbuliwa na maumivu ya tumbo.

Wakati madaktari wakimfanyia upasuaji wakidhani anasumbuliwa na ugonjwa wa kidole cha tumbo, walipigwa na butwaa walipogunudua mwanaume huyo ana mfumo kamili wa uzazi wa kike.

Tumboni mwake mbali ya kwamba kulikuwa na mfumo kamili wa uzazi wa kiume pia kuligundulika kuna mfumo kamili wa uzazi wa kike kukiwa na mji wa mimba, mayai ya uzazi ya kike, nyonga, mirija ya fallopian na tishu za sehemu ya siri ya kike.

Madaktari wa hospitali katika mji wa Bhopal, Madhya Pradesh, walishangazwa kugundua viungo hivyo vya uzazi vya kike vikiwa kwenye sehemu ya chini ya tumbo la Ryalu.

Daktari Pramod Kumar Shrivastava, wa hospitali hiyo alisema kwamba Ryalu kwa nje hana tofauti na wanaume wengine, alikuwa na viungo vyote vya uzazi vya kiume na alikuwa akiishi maisha ya kawaida kama mkulima.

"Tumeviondoa viungo vyote vya uzazi vya kike na hivi sasa anaendelea vizuri", alisema daktari Shrivastava.

Taarifa zaidi ziliongeza kwamba Ryalu hakuwahi kusumbuliwa na matatizo yoyote ya tumbo hadi hivi karibuni alipokumbwa na maumivu makali tumboni na kuwahishwa hospitali.

"Hana matatizo yoyote ya kijinsia, homoni zake zote ni za kiume na hana matiti kwenye kifua chake", aliongeza dakati mwingine wa hospitali hiyo

TUNAWATAKIA MFUNGO MWEMA WA MWEZI MTUKUFU WA RAMADHAN

RAMADHAN KARIM.

Jumatatu, 1 Agosti 2011

POMBE ZA HARUSI ZAMUUA MZAMBIA

Wahudumu wa Afya wakitoa mwili wa marehemu ndani ya hoteli.

RAIA wa Zambia amekutwa amekufa ndani ya Hoteli ya Southern Sun jijini Dar es Salaam, huku watu wengine watatu wakiwa katika hali mbaya kwa kile kinachosemekana kuzidiwa na ulevi.

Wanaume hao wanne walikutwa katika chumba namba 425 ghorofa ya nne ndani ya hoteli hiyo iliyoko katikati ya Jiji, watatu wakiwa hawajitambui.

Aliyefariki ametambuliwa kwa jina moja la Baster. Mwandishi wa gazeti hili alifika hotelini hapo saa saba mchana na kukuta Askari wa Upelelezi wa Mkoa wa Kipolisi wa Ilala, wakiendelea na kazi yao huku wafanyakazi wa hoteli hiyo wakionesha wasiwasi kutokana na tukio hilo.

Katika mlango wa nyuma wa hoteli hiyo, maiti ya Mzambia huyo ilitolewa na wahudumu wa afya wa kampuni binafsi na kuiingiza katika gari la kampuni hiyo kisha kuondoka nayo chini ya ulinzi wa Polisi.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, Faustine Shilogile alithibitisha kifo hicho na kusema Polisi wanaendelea na uchunguzi.

Wanaume watatu waliokuwa hai walifikishwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili wakiwa mahututi, lakini baada ya kuwekewa maji, mmoja wao, Eliud Sikwabi ambaye ni Muingereza, alizinduka na kuhojiwa na kuwataja wenzake Ikbar Bahabur wa Zambia na Mtanzania aliyetajwa kwa jina moja la Omari, ambaye anayeaminika alishiriki katika harusi iliyofanyika usiku wa kuamkia jana ambako alitumbuiza.

Kamanda Shilogile alisema kinachoonekana kuwa watu hao walikunywa sana pombe kali, ndiyo sababu ya hali hiyo ambazo walianza kunywa pombe hizo katika sherehe ya harusi ya mtoto wa Jaji Mark Bomani.

Aliyekuwa amepanga katika chumba hicho cha Hoteli ya Southern Sun ni Sikwabi.

“Inasemekana watu hawa baada ya kutoka kwenye harusi hiyo, waliendelea kunywa pombe hizo chumbani na hata Polisi wamekuta mabaki ya pombe hizo chumbani na uchunguzi wa pombe hizo unaendelea,” alisema Kamanda Shilogile.

Akizungumza na gazeti hili jana, Jaji Bomani alikiri watu hao kuwepo katika harusi ya mwanawe, Clement Bomani iliyofungwa juzi asubuhi katika Kanisa la Mtakatifu Joseph na baadaye walipata chakula cha mchana katika Ukumbi wa Mlimani City.

Jaji Bomani alikiri kuwa watatu waliolazwa katika Hospitali ya Muhimbili ni marafiki wa mtoto wake huyo, lakini alisema aliyefariki dunia hawamtambui, bali alifika na rafiki zake hao.

Alisema baada ya chakula cha mchana, vijana walikuwa na sherehe yao jioni iliyofanyika nyumbani kwake Mikocheni, ambako walikunywa pombe.

Kamanda Shilogile alisema, wanaendelea na uchunguzi kutokana na kuwa matukio ya vifo vinavyotokana na pombe au sumu uchunguzi wake huchukua muda mrefu. Aliahidi kuzungumzia suala hilo kwa undani leo.

Awali, Meneja wa zamu wa kike (jina lake halikufahamika) ambaye mwandishi alimsubiri kwa karibu saa moja, alikataa kuzungumzia suala hilo kwa madai ya Mkurugenzi Mkuu pekee ndiye anayeweza kuzungumzia.

Mkurugenzi Mkuu wa hoteli hiyo, Adam Fuller, alisema kwa kuwa uchunguzi wa Polisi unaendelea, hana cha kueleza.

Chanzo; Gazeti la Habari Leo

Jumapili, 31 Julai 2011

MANCHESTER 2 VS BARCELONA 1

LIVE blog: Manchester United vs. Barcelona

For the first time since their clash in the Champions League final in May, Manchester United and Barcelona will meet again in a friendly here at FedEx Field.
Some major stars are missing, Messi and Chicharito are the most glaring absences, but it remains a compelling match-up between two of the world’s best teams.
Follow along here for live updates from Landover. The lineups were released earlier, you can catch them after the jump.
FINAL: Manchester United 2 - Barcelona 1. Can you call it revenge for the Champions League? Um, no. But it was an entertaining game and had some great goals and fun moments.
Manchester United was the better team in the first half, but Barcelona was more aggressive in the final 45 minutes and the subs helped the pace and entertainment value of the contest late. Thiago had a beautiful goal, but a giveway was punished and United got the result.
Thanks for joining us on the blog for the live chat and sorry for the technical difficulties!
90’+- Wow. Michael Owen with a laugher. Obertan turned the corner and found Owen alone on the far post, but he somehow put his effort way over the frame. That was embarrassing.
89’ - Nearly an equalizer! Barcelona moving the ball well in the final third and get a good look at goal, but Thiago’s shot goes over the bar.
85’ - The pace of the game has certainly picked up since about the 65th minute. That’s when you saw some subs and young players come on. Fresh legs and something to prove. Been a bit more back and forth.
76’ - GOAL! Didn’t take long for Manchester United to reclaim the lead. A very poor square pass from Busquets in his own half was intercepted by Tom Cleverly, and he put Michael Owen in alone. Owen made no mistake in front of net, chipping over Valdes’ left hand to give United the 2-1 lead.
70’ - GOAL! Barcelona finally evens the score on a brilliant play from Thiago. A ball from Carlos Carmona slipped by a sliding Ryan Giggs, Thiago took possession, looked up from 20 yards out and hit a curling ball that turned inside out and into the upper 90. 1-1.
Computer issues kept me from updating the first 25 minutes of the second half.
HALFTIME: Manchester United certainly looked the more dangerous team in the attack, with Barcelona only showing some flashes of its ability when it strings passes together. Iniesta had late signature pass that set up a chance, but Manchester United’s defense handled its business.
Nani was the most dangerous player on the field in the first 45 minutes, constantly taking on defenders down the right sideline and serving in several dangerous crosses. His perfectly-timed run was rewarded and he showed composure with a great finish. It’s 1-0 here at FedEx in favor of United.
43’ - Afellay off. Isaac Cuenca on for Barcelona.
41’ - Looks like Afellay just pulled his left hamstring. Grabbed back of his left leg as he dribbled toward the sideline. He’ll get subbed out.
39’ - Nani continues to cause headaches for Barca, but a Rooney giveaway at the top of the box leads to a counter. No matter. Once again United’s back line steps up, this time Jonny Evans doing well to block a shot and draw a foul.
35’ - United defense is up to the task tonight, but Barcelona seems to be taking extra touches in the box. Looking for special moments in a friendly perhaps.
30’ - Jonathan dos Santos earns a yellow card for a knee-to-thigh challenge on Ashley Young.
28’ - It’s a deserved lead for Manchester United. Barcelona had started to press more and Man U was defending with 11 behind the ball, but they broke out quickly on that counter and Nani timed his run perfectly to stay onside. Barca playing a high line defensively and United looking to exploit it.
22’ - GOAL! Barcelona was holding the ball more in the final third and earns a corner kick but Manchester United clears and counters right up the gut. Nani makes a run crossing defenders to the left side, gets the feed from Welbeck and finishes low. 1-0 Manchester United
20’ - Still not much for Barcelona in the final third. Afellay with a couple stepovers to get into the box but his touch is a bit heavy and the ball goes over the end line for a goal kick.
15’ - A Barca chant breaks out at FedEx but United looking dangerous still. A little combination between Rooney and Nani leads to another cross, but Barca clears. The right side is being exploited right now by the Red Devils. Abidal playing left back.
10’ - Manchester United has what may qualify as more than a half chance. Nani got the ball on the right sideline and served a low curling ball on the ground. Rooney met it at the near post but his effort was wide. Should have at least put the shot on target. Nonetheless, Man U actually with the better of play, I’d argue, through the first 10 minutes.
5’ - Manchester United with the first chance. Evra with a pretty ball down the left sideline to Ashley Young, but his cross is easily collected by Valdes. Now Sergio Busquets is down on the field.
1’ - And we’re off here at FedEx Field. Manchester United kicked off as the crowd still fills in the upper bowl in Landover.

Barcelona Starting XI: Valdes; Fontas, Abidal, Alcantara, dos Santos; Busquets, Iniesta, Keita; Villa, Pedro, Afellay. Subs: Pinto, Masip, Balliu, Pique, Puyol, Xavi, Suarez, Riverola, Cabelino, Lozano, Muniesa, Carmona, Espinosa, Cuenca
Manchester United Starting XI: De Gea; Evra, Vidic, Evans, Rafael; Cleverly, Anderson, Young, Nani; Rooney, Welbeck. Subs: Lindegaard, Amos, Jones, Ferdinand, Smalling, Fabio, Obertan, Owen, Giggs, Carrick, Park, Diouf, Berbatov, Macheda

LIVERPOOL KUENDELEA KUMKOSA GERRAD HADI MWEZI SEPTEMBER AKIENDELEA NA MATIBABU HOSPITALI.

Steven Gerrad kushoto.
Gerrad katika hekaheka za uwanjani mwanzoni mwa msimu uliopita.

SONGEA; MEYA WA MANISPAA YA SONGEA MH. ALLI MANYA AMEFARIKI DUNIA LEO AKIWA HOSPITALI YA PERAMIHO

Marehemu Alli Manya wa kwanza kulia enzi za uhai wake, alikuwa meya wa manispaa ya Songea pia diwani wa kata ya Lizaboni huko Songea, mazishi yanatarajiwa kufanyika kesho huko Lizaboni songea,KWA MUNGU KILA KIUMBE KITARUDI KWAKE,AMINA.

TEKNOLJIA YA KAMERA KATIKA GOLI KUANZA KUTUMIKA.

Teknolojia katika soka

Teknolojia  katika soka
Teknolojia katika soka
Teknolojia ya kutumia kamera katika goli huenda ikaanza kutumika katika ligi kuu ya Premier mwanzoni mwa msimu ujao wa 2012-13.
Halmashauri ya kimataifa ya chama cha mpira cha England itatoa uamuzi kama idhinishe mfumo huo ama la mnamo mwezi wa Machi 2012.
Ikiwa itathibitishwa basi kiongozi wa FIFA Sepp Blatter anasema ligi za soka zitaweza kuutumia mwanzoni mwa msimu wa 2012-13 endapo utakua hauna kasoro wala hautagharimu fedha nyingi.
Mkuu wa ligi ya Premier ya England, Richard Scudamore amesema kwamba watautumia mfumo huo mara tu utakapoidhinishwa.

Teknolojia ya goli kuidhinishwa.
Blatter aliongeza kusema kwamba teknolojia hiyo inaweza pia kutumika katika michuano ijayo ya kombe la dunia la mwaka 2014 nchini Brazil .
Kwa miaka mingi mkuu huyo wa Fifa amekua akipinga matumizi ya teknolojia katika eneo la goli lakini inaelekea alibadili mawazo yake baada ya mabishano makali kuzuka mnamo mwaka 2010.

WAMSHUKU KUWA NI GAIDI KWA KUSOMA KURAN NDANI YA BASI, MMH!!!!



Sunday, July 31, 2011 10:25 AMMwanaume mmoja raia wa Tunisia aliyekuwa akisoma quran kwa sauti ya chini akiwa ndani ya basi la abiria lililokuwa likitoka Denmark kwenda Ufaransa, aliingia matatani baada ya kushukiwa ni gaidi anayejiandaa kujilipua.
Tukio hilo lilitokea kaskazini mwa nchini Ujerumani wakati basi hilo la abiria ambalo lilikuwa likitokea Copenhagen kuelekea Paris lilipolazimika kupaki pembeni ya barabara na kusababisha foleni kubwa kwa masaa mawili wakati polisi, mbwa na wataalamu wa mabomu wakilifanyia uchunguzi basi hilo na mwanaume aliyedaiwa kuwa ni gaidi.

Tukio hilo lilitokea baada ya mwanamke mmoja aliyekuwa amekaa pamoja na mwanaume huyo alipomsikia mwanaume huyo ambaye jina lake halikutajwa akisoma quran kwa sauti ya chini.

"Alimsikia akisoma surah za Quran kwa sauti ya chini na alikichukulia kitendo hicho kama maandalizi ya mwanaume huyo kujilipua", alisema msemaji wa polisi wa mji wa Rotenburg, Detlev Kaldinski.

Alimuonya dereva kuwa kuna mtu anataka kujilipua na kusababisha dereva wa basi hilo lililokuwa limebeba abiria 45 kulipaki basi hilo pembeni ya barabara bila ya kujali ilikuwa ni usiku wa manane.

Baada ya muda mfupi polisi waliwasili wakiwa na timu ya watu 20 wakiwemo wapelelezi, wataalamu wa mabomu na kikosi maalumu cha jeshi pamoja na mbwa wa kunusa mabomu.

Uchunguzi uliofanyika ulionyesha kuwa mwanaume huyo raia wa Tunisia hakuwa na mabomu wala silaha yoyote.

Mwanamke aliyenzisha kasheshe hilo aliwaambia polisi kuwa alimsikia mwanaume huyo akitaja jina la Osama wakati wa dua zake.

Mwanaume aliyeshukiwa kutaka kujilipua alijitetea kwa kusema kwamba marafiki zake hupenda kumuita kwa jina la Osama na yeye mwenye pia hupenda kujiita kwa jina hilo

Jumamosi, 30 Julai 2011

WANAWAKE WAJIHADHARI NA MUUAJI WA WANAWAKE GESTI.



Wanawake jihadharini na mwanaume huyu


Friday, July 29, 2011 2:19 AM
WANAWAKE wa jiji la Dar es salaam mnatakiwa kuwa makini na macho na hasa kupunguza tamaa za kimwili na mali kwa kuwa amejitokeza mwanaume mmoja anayenyonga wanawake mara amalizapo kufanya nae mapenzi imedaiwa.
Mwanaume huyo inasemekana ni mmoja ambaye hadi sasa ameshanyonga wanawake wapatao saba na wa saba ni mwanamke aliyekuwa mke wa mwanamziki wa kundi la Taarabu la Five Star aitwae Issa Kamongo(pichani-Farida) mazishi yake yaliyofanyika juzi Bunju

Kutokana na kukua kwa idadi ya wanawake wanaonyongwa kuongezeka siku hadi siku wanawake wanatakiwa kuwa makini na mwanaume huyu anayenyonga wanawake kwa sababu ambayo haijafahamika hadi sasa

Mwanaume huyu inasemekana anapendelea sana wake za watu, wanawake weupe na wenye mvuto na kisha kumrubuni kuingia nae nyumba ya wageni’gest’ na kisha kumnyonga mwanamke huyo na kumlaza kifudifudi na yeye kutimka

Mwanaume huyo anahisiwa kuwa ni mmoja kwa mujibu wa mashuhuda wanaomuona aingiapo na wanawake ambapo maelezo ya wahudumu wa gesti wanapokufa wanawake huwa yanafanana

Wasifu wa mwanaume huyo anadaiwa kuwa ni Mweupe, mzuri wa maumbile na sura yaani Handsome’ na anapendelea kuvaa kofia aina ya kep

Jana mwanamke mmoja aliweza kuongea ndani ya Redio na kukiri ni kweli mwanaume huyo yupo, na ameshawahi kukatana nae maeneo ya ubungo na mwanaume huyo alimwita kwa lengo la kumuuliza amsaidie kwa kuwa eneo hilo yeye ni mgeni na mwisho akaanza kumrubuni na kumtaka aende nae kwenye msitu wa Chuo Kikuu

Amesema walishaanza safari na mwanamke huyo wakati akiongea nae machale yakamcheza na alijisikia kama haongei na mwanadamu wa kawaida na mwili kuwa kama umekufa ganzi na ghafla mwanamke huyo alimwambia amuache kwanza kuna kitu amesahau pale alipotoka na kumuahidi angerudi na ndipo alipoponea kwenye tundu la sindano

Hata hivyo inahisiwa kuwa huenda mwanaume huyo hutumia pia nguvu za giza kuwapata wanawake hao kwa kutojielewa.

Awali mwanzoni mwa mwezi Juni, jeshi la polisi lilishatoa tahadhari kwa wanawake na kuahidi kumsaka mwanaume huyo lakini bado hajakamatwa na kutangazwa

LIBYA;WAASI WALIMUUA KAMANDA WAO WENYEWE.

Kamanda wa Libya aliuliwa na wenzake

Viongozi wa wapiganaji wa Libya wanasema wafuasi wao wenyewe ndio waliomuuwa kamanda wa jeshi la wapiganaji hao, Jenerali Abdel Fattah Younes.
Mazishi ya Jenerali Younes Ijumaa


Waziri wa Mafuta na Fedha wa wapiganaji, Ali Tarhouni, alisema Jenerali Younis aliuliwa na wapiganaji walioasi, na wanaoshirikiana na waislamu wenye msimamo mkali.

Alisema haijulikani sababu yao ya kumuuwa kamanda huyo.
Alieleza kuwa waasi hao walimchukua Jenerali Younes na kumpiga risasi na kumuuwa, baada ya jenerali huyo kuitwa aende mbele ya kamati inayochunguza kama alikuwa mtiifu kwa wapiganaji.
Serikali ya Kanali Gaddafi ilisema mauaji hayo yanaonesha kuwa wapiganaji hawatoweza kuiongoza Libya, na hata wanashindwa kuwalinda viongozi wao

HONGERA CRDB KWA KUTOA HUDUMA HADI NYUMBANI; GARI LA HUDUMA ZA KIBENKI ZA CRDB LIKIWA LINAHUDUMIA WATEJA MJINI NACHINGWEA JANA.

Wateja wakipata huduma za kibenki.


Gari hili inasemekana lipo siku zote, kwa ushauri tu mnaonaje mkifungua tawi rasmi!!? Inavyoonekana Wateja ni wengi wa kutosha,kazi kwako Dr. Kimei.

Ijumaa, 29 Julai 2011

MH. RAIS J K KIKWETE AMALIZA ZIARA YA SIKU TANO MKOANI MTWARA, APANDA NDEGE UWANJA WA NACHINGWEA ALASIRI HII KUENDELEA NA RATIBA ZINGINE.

Uwanja wa ndege Nachingwea,wananchi wakisubiri kumuaga Mh. Rais
Wnafunzi wa Chuo cha Ualimu Nachingwea wakiwa wamejipanga kumuaga JK

Mama Salma Kikwete alianza kuwasili 
Baadaye Mh. Rais Alipokelewa Uwanjani
JK akisalimia baadhi ya viongozi waliomlaki.

Jumatano, 27 Julai 2011

MBUNGE WA NYAMAGANA NDUGU WENJE ATOLEWA NJE YA BUNGE NA ASKARI BAADA YA KUTOKEA TAFARANI KIDOGO MCHANA HUU.

Huyu bwana Ezekia Wenje huwa naogopa hata kumuita mheshimiwa kwani ana matata sana akiwa bungeni,mengine naona hayana hata msingi........Alitolewa nje na sajini wa Bunge kwa kosa la kuongea bila ruhusa ya Mwenyekiti wa Bunge pale alipokuwa akimtetea mbunge mwenzie Tundu Lissu kuwa ameonewa,alikuka taratibu za kuongea bila ruhusa.

MAITI YAZINDUKA MOCHWARI NA KUZUA TAFRANI.



Mwanaume mwenye umri wa miaka 50 wa nchini Afrika Kusini ambaye alihisiwa kuwa amefariki na mwili wake kulazwa monchwari kwa masaa 21, alizinduka na kuwafanya wafanyakazi wa monchwari wakimbie wakidhani wameona mzimu.
Kelele za maiti akitaka atolewe toka kwenye chumba chenye baridi kali cha monchwari, ziliwafanya wafanyakazi wa monchwari watoke nduki wakidhani wameona mzimu.

Tukio hilo lilitokea juzi jumapili nchini Afrika Kusini wakati mwanaume mwenye umri wa miaka 50 kuhisiwa kuwa ameiaga dunia na mwili wake kupelekwa monchwari wakati taratibu za mazishi zikiandaliwa.

Lakini baada ya mwili wa mwanaume huyo ambaye jina lake halikutajwa kuwekwa kwenye chumba chenye baridi cha monchwari kwa zaidi ya masaa 20, mwanaume huyo alizinduka na kujikuta yuko monchwari kwenye baridi kali sana.

Mwanaume huyo alipiga kelele akitaka atolewe toka kwenye chumba hicho lakini badala yake wafanyakazi wa monchwari walidhani wameona mzimu na kutimua mbio.

"Familia yake walidhani ameiaga dunia", alisema msemaji wa wizara ya afya, Sizwe Kupelo.

"Familia yake ikiamini kuwa ndugu yao amefariki iliwaita waandaaji wa mazishi ambao waliuchukua mwili wa marehemu na kuupeleka monchwari lakini kwenye majira ya saa 11 jioni jana jumapili, mwanaume huyo alizinduka na kupiga kelele atolewe toka kwenye chumba cha baridi", alisema msemaji huyo wa wizara ya afya.

Tukio hilo lililotokea kwenye mji mdogo wa Libode lilisababisha wafanyakazi wawili wa monchwari waliokuwa zamu waamue kutimua mbio wakidhani wameona mzimu.

Baada ya kupiga kelele za kuomba msaada na baadae kurudi monchwari na kumkuta mwanaume huyo yuko hai, waliita ambulansi ambayo ilikuja kumchukua mwanaume huyo na kumuwahisha hospitali.

Msemaji huyo wa wizara ya Afya aliwataka wananchi kutojichukulia majukumu ya kuwaita watu wa monchwari wanapodhani ndugu zao wamefariki.

"Ni madaktari, watoa huduma za afya au mapolisi ndio wenye haki za kuwachunguza wagonjwa na kutoa taarifa kama wamefariki au la", alisema msemaji huyo wa wizara ya afya.

Taarifa iliyotolewa leo na wizara ya afya ilisema kwamba mwanaume huyo alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa asthma na ndugu zake walidhani amefariki alipokutwa amezimia nyumbani kwake.

Taarifa hiyo iliongeza kuwa mwanaume huyo alilazwa kwenye toroli ndani ya chumba chenye baridi kali cha monchwari kwa masaa 21 kuanzia siku ya jumamosi jioni mpaka alipozinduka siku ya jumapili.