Sunday, July 31, 2011 10:25 AMMwanaume mmoja raia wa Tunisia aliyekuwa akisoma quran kwa sauti ya chini akiwa ndani ya basi la abiria lililokuwa likitoka Denmark kwenda Ufaransa, aliingia matatani baada ya kushukiwa ni gaidi anayejiandaa kujilipua. | ||
Tukio hilo lilitokea kaskazini mwa nchini Ujerumani wakati basi hilo la abiria ambalo lilikuwa likitokea Copenhagen kuelekea Paris lilipolazimika kupaki pembeni ya barabara na kusababisha foleni kubwa kwa masaa mawili wakati polisi, mbwa na wataalamu wa mabomu wakilifanyia uchunguzi basi hilo na mwanaume aliyedaiwa kuwa ni gaidi. Tukio hilo lilitokea baada ya mwanamke mmoja aliyekuwa amekaa pamoja na mwanaume huyo alipomsikia mwanaume huyo ambaye jina lake halikutajwa akisoma quran kwa sauti ya chini. "Alimsikia akisoma surah za Quran kwa sauti ya chini na alikichukulia kitendo hicho kama maandalizi ya mwanaume huyo kujilipua", alisema msemaji wa polisi wa mji wa Rotenburg, Detlev Kaldinski. Alimuonya dereva kuwa kuna mtu anataka kujilipua na kusababisha dereva wa basi hilo lililokuwa limebeba abiria 45 kulipaki basi hilo pembeni ya barabara bila ya kujali ilikuwa ni usiku wa manane. Baada ya muda mfupi polisi waliwasili wakiwa na timu ya watu 20 wakiwemo wapelelezi, wataalamu wa mabomu na kikosi maalumu cha jeshi pamoja na mbwa wa kunusa mabomu. Uchunguzi uliofanyika ulionyesha kuwa mwanaume huyo raia wa Tunisia hakuwa na mabomu wala silaha yoyote. Mwanamke aliyenzisha kasheshe hilo aliwaambia polisi kuwa alimsikia mwanaume huyo akitaja jina la Osama wakati wa dua zake. Mwanaume aliyeshukiwa kutaka kujilipua alijitetea kwa kusema kwamba marafiki zake hupenda kumuita kwa jina la Osama na yeye mwenye pia hupenda kujiita kwa jina hilo |
KARIBU KATIKA BLOGU HII YA KUELIMISHA, KUBURUDISHA NA KUONYA KUPITIA MADA MBALIMBALI NA HATA PICHA. ONGEZA MAHUSIANO KWA KUJUMUIKA NA WENZIO HAPA.UNAWEZA TUMA PICHA NA MAELEZO KWA ANUANI HII;mkuu74@gmail.com
Jumapili, 31 Julai 2011
WAMSHUKU KUWA NI GAIDI KWA KUSOMA KURAN NDANI YA BASI, MMH!!!!
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni