Jumatano, 6 Julai 2011

WAVAMIZI WA MITANDAO(HACKERS) YA HABARI WAZUSHA KIFO CHA OBAMA

Uzushi wa Kuuliwa Kwa Rais Barack Obama


Rais wa Marekani, Barack Obama
Habari za uzushi kuhusiana na kuuliwa kwa Rais Barack Obama kwa kupigwa risasi zilitangazwa kwenye akaunti ya Twitter ya televisheni ya Fox News ya Marekani na kuzua kizazaa lakini baadae iligundulika kuwa akaunti hiyo ya Twitter ilikuwa mikononi mwa Hackers.
Hackers jana walifanikiwa kuiiba akaunti ya Twitter ya televisheni ya Fox News na kisha kutangaza kuuliwa kwa rais wa Marekani, Barack Obama.

Televisheni ya Fox News ilithibitisha kuibiwa kwa muda kwa akaunti yake ya Twitter na habari zisizo na ukweli zilianza kuchapishwa kwenye ukurasa wake wa Twitter kuanzia majira ya nane usiku kwa masaa ya Marekani.

"Barack Obama amefariki dunia, rais ameuliwa, siku mbaya ya julai 4, Rais Barack Obama ameuliwa", ilisema taarifa ya kwanza kuhusiana na kuuliwa kwa Obama kwenye akaunti ya Twitter ya Fox News.

Taarifa hiyo iliongeza kuwa Obama ameuliwa kwa kupigwa risasi mbili kwenye mgahawa wa Ross mjini Iowa wakati akipiga kampeni za uchaguzi.

Taarifa hiyo ilizua kizazaa baada ya watu wengi kuanza kuwatumia wenzao taarifa hizo huku blogu nyingi zikianza kunukuu kuuliwa kwa Obama.

Habari hizo ziligundulika baadae kuwa ni za uzushi kwani rais Obama hakuwa Iowa kama ilivyodaiwa badala yake alikuwa Washington pamoja na familia yake.

Fox News waliomba radhi kwa usumbufu uliosababishwa na habari hizo za uongo na kwamba imeanzisha uchunguzi kujua chanzo cha akaunti ya Twitter kuingia mikononi mwa Hackers

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni