Jumapili, 3 Julai 2011

AU haitomkamata Gaddafi

Umoja wa Afrika, AU, umesema kuwa mataifa yanachama hayatofuata amri ya Mahakama ya Uhalifu ya Kimataifa , ICC, kwamba kiongozi wa Libya, kanali Gaddafi, akamatwe.
Malabo, mji mkuu wa Equatorial Guinea, walikokutana viongozi wa AU


Uamuzi huo ulifikiwa katika mkutano wa kilele wa AU, uliofanywa Malabo, Equatorial Guinea.
Mataifa ya Afrika yamekubaliana kutoshirikiana na ICC kutekeleza amri ya kumkamata Colonel Gaddafi.
AU ilisema kwenye taarifa yake kwamba amri hiyo inatatanisha sana juhudi za mataifa ya Afrika za kutafuta suluhu ya kisiasa katika vita vya Libya.
Mkuu wa AU, Jean Ping, alisema siyo kwamba viongozi wa Afrika wako dhidi ya ICC, lakini wanaona kuwa mahakama hayo yanawalenga wakuu wa Afrika tu.
Alimuelezea Mkuu wa Mashtaka wa ICC, Luis Moreno Ocampo, kuwa "mzaha" ("a joke"").
Wakati huo huo, wawakilishi wa wapiganaji wa Libya, walikaribisha mpango wa AU wa kufanya mazungumzo bila ya Kanali Gaddafi kuhudhuria.
Hilo linaweza kuwa fanikio la mwanzo la AU kuhusu Libya, ambayo kabla ikionesha kama imegawika juu ya swala hilo.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni