Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo TANZIA. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo TANZIA. Onyesha machapisho yote

Jumamosi, 1 Desemba 2012

VITU VILIVYOIBIWA KWENYE AJALI YA SHAROMILIONEA VIMEPATIKANA BAADHI.

VITU VYA SHARO MILIONEA VYAPATIKANA... WATUHUMIWA WAKIMBILIA KUISHI MAPORINI KUHOFIA KUKAMATWA


Baadhi ya vitu vya marehemu Sharo Milionea vilivyoibwa baada ya ajali iliyochukua maisha yake. Picha: Issamichuzi.blogspot.com


Baadhi ya vitu vya marehemu Sharo Milionea vilivyoibwa baada ya ajali iliyochukua maisha yake. Picha: Issamichuzi.blogspot.com

MSAKO mkali wa nyumba kwa nyumba uliofanywa kwa ushirikano wa polisi na wananchi umefanikisha kupatikana kwa baadhi ya vitu vya msanii wa filamu na bongofleva marehemu Hussen Mkieti "Sharo Milionea" vilivyoibwa baada ya gari ndogo aliyokuwa akiendesha kupata ajali katika kijiji cha Maguzoni wilayani hapa na kuchukua maisha yake.

Hayo yalisemwa  juzi  usiku na mkuu wa wilaya ya Muheza, Subira Mgalu wakati akitokea katika msako huo kwenye kijiji cha Maguzoni ambapo watuhumiwa wamezihama nyumba zao kuhofia kukamatwa.

Mgalu alisema kuwa msako huo wa nguvu uliohusisha jeshi la polisi na wananachi wema wa kijiji cha Maguzoni ulifanyika usiku katika kijiji hicho kwa kupita nyumba hadi nyumba mpaka baadhi ya vitu vya msanii huyo vilipoonekana.

Mkuu huyo wa wilaya alivitaja baadhi ya vitu vilivyopatikana kuwa ni tairi la akiba, radio ya gari, betri ya gari, simu ya mkononi, saa ya mkononi, suruali aina ya jeans na fulana, ambavyo walimvua marehemu na kumuacha na 'boxer' tu.

Mgalu alisema kuwa katika msako huo ambao bado unaendelea, jeshi la polisi liliongozwa na mkuu wa polisi wa wilaya ya Muheza Endrew Satta, mkuu wa upelelezi wilaya aliyefahamika kwa jina la Mgimwa na mkuu wa kituo cha polisi Muheza aliyefahamika kwa jina la Joseph.

Juzi, mkuu huyo wa wilaya alitoa siku mbili vitu hivyo viwe vimeonekana na kama havijaonekana msako mkali wa nyumba kwa nyumba utaingia kijijini hapo wakati alipokuwa akitoa nasaha zake katika mazishi nyumbani kwa msanii huyo Jibandeni kijiji cha Lusanga.

Mbunge wa jimbo la Muheza, Herbert Mntangi, diwani wa viti maalum tarafa ya Ngomeni, Jestina Mntangi, mwenyekiti wa CCM wilaya, Peter Jambele na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Muheza, Amiri Kiroboto wamelaani kitendo hicho na kulitaka jeshi la polisi kufanya kazi yake kuhakikisha vitu vyote vinapatikana

Msanii wa filamu za ucheshi na muziki wa bongofleva, Sharo Milionea, alifariki katika eneo la ajali katika kijiji cha Maguzoni, Muheza wakati gari dogo aina ya Toyota Harrier ilipoacha njia na kupinduka mara kadhaa alipokuwa njiani kwenda kwao Lusanga, Muheza kumuona mama yake akitokea jijini Dar es Salaam.

Sharo Milionea alipata umaarufu mkubwa kupitia staili yake ya kuigiza kama mchekeshaji msafi tofauti na wengi ambao huamini kwamba mchekeshaji ni lazima avae vinyago, kikatuni ama ajipake masizi. Misemo yake ya "kamata mwizi meen", "umebugi meen!" na "ohh mamma!" ilimpa mashabiki wengi hasa watoto.

Jumamosi, 13 Oktoba 2012

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MWANZA SACP LIBERATUS BARLOW AMEUAWA USIKU WA KUAMKIA LEO.

BREAKING NEWS: RPC MWANZA AUAWA USIKU WA KUAMKIA LEO


 SACP Liberatus Barlow 


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza Kamishna Mwandamizi wa Polisi (SACP) Liberatus Barlow ameuawa usiku wa kuamkia leo katika tukio linalohusishwa na ujambazi. 

Taarifa kutoka Mwanza ambazo zimethibitishwa na Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini zinasema kuwa Kamanda Barlow aliuawa baada ya kumrudisha dada yake kutoka katika kikao cha harusi ya ndugu yao huko Kitangili mnamo saa 7.30 usiku wa kuamkia leo.
Hata hivyo, kwa mujibu wa mkuu wa operesheni wa jeshi la polisi ni kuwa habari hizo ni za kweli na amewataka wananchi wa mwanza kuwa watulivu na kuahidi wahalifu hao watapatikana.
Pole sana wanafamilia kwa kupoteza kiongozi mzuri wa jamii na familia.
Habari; ITV

Jumamosi, 29 Septemba 2012

MAREHEMU KAMAZIMA AMEAGWA LEO HUKO TEGETA DAR ES SALAAM TAYARI KWA MAZISHI MARUKU BUKOBA.

 

Marehemu Anatoly Kamazima(katikati) wakati alipoapishwa kuwa Wakili wa Mahakama Kuu June 2011 Dar es salaam akiwa na mawakili wenzie Joseph Kiula wa pili toka kulia na Mzalendo wa kwanza kulia, kushoto ni wakili Burhan Othman.
HISTORIA FUPI YA MAREHEMU MEJA JENERALI MSTAAFU ANATOLY KAMAZIMA.Marehemu alizaliwa mwaka 1946 katika kijiji cha Maruku, Mkoani Kagera. Alijiunga na Jeshi mwaka 1967, mara baada ya kuhitimu Chuo Kikuu mwaka 1966.

Marehemu Kamazima amesoma kozi mbalimbali za kijeshi hapa nchini na nchi za China, India, Uingereza na Misri na kulitumikia Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) katika ngazi mbalimbali ambapo mwaka 1989, aliteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Tume ya Kuzuia Rushwa Tanzania, hadi alipostaafu Juni 2003.

Rais amemuelezea marehemu Kamazima kama mzalendo na mtu aliyeipenda na kuitumikia nchi yake kwa weledi mkubwa, uaminifu na moyo mmoja.

“Nimemfahamu Marehemu kwa miaka yote ya utumishi wake jeshini na serikalini kama mzalendo, muaminifu na mwenye moyo wa kulinda nchi yake wakati wote” amesema Rais “Marehemu Kamazima alikua mtu wa kutumainiwa sana katika nchi yetu na kamwe hatutamsahau kwa utumishi wake uliotukuka”.

“Tutamkumbuka na kumuenzi siku zote, tunamshukuru Mwenyezi Mungu kwa yote na tunamuombea mapumziko mema Marehemu Kamazima. Amina”. Rais ameongeza.

Marehemu ameacha mjane, watoto na wajukuu.

Imetolewa na:

Premi Kibanga,
Mwandishi wa Habari wa Rais, Msaidizi,
Ikulu.
DAR ES SALAAM

26 Septemba, 2012
 *************************************************************************
 Rais na Amiri Jeshi Mkuu Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akitoa pole kwa mjane na ndugu wa wa Meja Jenerali Mstaafu Anatoli Kamazima leo nyumbani kwa marehemu Tegeta, Dar es salaam. Marehemu Kamazima, ambaye amefariki dunia usiku wa kuamkia  Jumatano ya Tarehe 26 Septemba, 2012 utokana na mshtuko wa moyo, alikuwa Mkurugenzi Mkuu wa kwanza wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini TAKUKURU.


Rais na Amiri Jeshi Mkuu Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Brigedia Jenerali Mstaafu Tindamanyire, ndugu wa hayati Meja Jenerali Mstaafu Anatoli Kamazima, leo nyumbani kwa marehemu Tegeta, Dar es salaam. Kulia kwa Rais ni Mkuu wa Majeshi Jenerali Davis Mwamunyange na Mnadhimu Mkuu Luteni Jenerali Samwel Albert Ndomba. Marehemu Kamazima, ambaye amefariki dunia usiku wa kuamkia  Jumatano ya Tarehe 26 Septemba, 2012 kutokana na mshtuko wa moyo, alikuwa Mkurugenzi Mkuu wa kwanza wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini TAKUKURU

Jumapili, 27 Mei 2012

STANSLAUS BONIFACE AFARIKI DUNIA, NI YULE MWENDESHA MASHTAKA KESI ZA EPA, R I P BROTHER.

MKURUGENZI Msaidizi wa Mashitaka nchini na Mwendesha Mashitaka mashuhuri katika kesi kubwa mbalimbali nchini, Stanslaus Boniface amefariki ghafla.

Kwa mujibu wa taarifa zilizopatikana jana mchana na kuthibitishwa na Mkurugenzi wa
Mashitaka (DPP), Eliezer Feleshi, Boniface alifariki ghafla jana asubuhi na chanzo cha kifo chake hakijafahamika.

“Boniface amefariki leo (jana) alfajiri katika Hospitali ya Regency alikopelekwa baada ya kujisikia vibaya akiwa nyumbani kwake…msiba upo nyumbani kwake eneo la Chuo Kikuu cha Dar es Salaam,” alisema Ofisa Habari wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu (AG), Siatu Msuya.

Boniface alipata umaarufu katika kesi alizokuwa akiziendesha ambazo ni za wizi wa fedha za Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA) katika Benki Kuu (BoT) ikiwamo inayomkabili kada wa CCM, Rajab Shaban Maranda na wafanyakazi wanne wa BoT wanaodaiwa kuiba Sh 207,284,390.44.
.


Mkurugenzi wa Mashtaka Nchini, Ndg. Eliezer Feleshi

Nyingine ni ile ya wizi wa Sh bilioni 1.1 inayomkabili Bahati Mahenge na wenzake wanne.

Boniface alizaliwa Februari 21, 1968 na ameacha mke na watoto watatu. Amewahi kufanya kazi kama Mwendesha Mashitaka Mkuu katika mikoa ya Mwanza, Mbeya na Dar es Salaam

Jumatatu, 21 Mei 2012

MIAKA 16 YA TANGU KUZAMA KWA MV BUKOBA IMETIMIA, r i p ALL


Leo imetimia miaka 16 tangu Meli ya Mv Bukoba ilipozama Ziwa Victoria Mei 21 mwaka 1996, Tunawakumbuka Ndugu zetu.

Jumanne, 10 Aprili 2012

KANUMBA AMEZIKWA LEO KINONDONI DAR ES SALAAM, R.I.P KANUMBA.

HATIMAYE KANUMBA AZIKWA LEO MAKABURI YA KINDONDONI MAMIA WAFURIKA


 Mwili wa marehemu kanumba ukiwa unaingizwa katika uwanja wa Leaders klabu hivi leo asubui



Mamia walifurika kumuaga ndungu yetu steven Charles Kanumba
Mama mzazi wa marehemu Steven Kanumba akiwa anaelekea kwenye gari kwa ajili ya kuusindikiza mwili wa mtoto wake kaburini

Hali ilikuwa tete baada ya umati uliofurika kushindwa kufuata utaratibu wa kuaga ulioandaliwa mwanzo.
Chanzo; woindeshiza blogu

Jumatatu, 9 Aprili 2012

KANUMBA KUZIKWA KESHO JUMANNE MAKABURI YA KINONDONI BAADA YA KUAGWA VIWANJA VYA LEADERS. MAMA MZAZI AMEBARIKI WAZO HILO.


Mama mzazi wa Steven Kanumba anayeitwa Flora Mtegoa (katikati aliyeshika tama), akiwa amezungukwa na ndugu,jamaa na waombolezaji wengine mara baada ya kuwasili nyumbani kwa Marehemu Sinza-Vatican.Picha kwa hisani ya Shamim Mwasha at 8020 Fashions Blog
Steven Kanumba, muigizaji ambaye bila shaka tunaweza kusema ndiye alikuwa maarufu zaidi miongoni mwa waigizaji wa filamu za kitanzania(Bongo Movies) alifariki majuzi alfajiri kuamkia Jumamosi katika mazingira ambayo bado yanatatanisha na bado polisi wanaendelea na uchunguzi ingawa taarifa ya uchunguzi wao wa awali, iliyotolewa na RPC wa Kinondoni,Charles Kenyela, inaonyesha kwamba huenda marehemu amefariki kutokana na matumizi mabaya (alcohol abuse) ya pombe kali aina ya Jack Daniels.
Taarifa hiyo inafuatia mahojiano kati ya Polisi na muigizaji mwingine Elizabeth Michael “Lulu” ambaye inaaminika ndiye alikuwa na Marehemu ambapo awali kabla mauti hayajamkuta palitokea kutoelewana baina yao.Kwa mujibu wa maelezo ya Lulu, Kanumba alikuwa ametumia kinywaji hicho kwa wingi ana wakati wakiendelea na malumbano, alianguka na kujigonga katika ukuta wa chumbani hapo.
Hata hivyo, taarifa ya kitabibu(Post Mortem) kuchunguza chanzo cha kifo chake  bado haijawekwa wazi na  inatarajiwa kufanyika hivi leo(Jumatatu) na ukimalizika basi ndipo taarifa rasmi itatolewa na hivyo kubariki rasmi kuendelea kwa shughuli za mazishi hapo kesho
Read more: BongoCelebrity

Jumamosi, 7 Aprili 2012

R.I.P STEVEN KANUMBA

STEVEN KANUMBA AFARIKI DUNIA





Nimeshtushwa na message nilizozipata katika simu yangu toka kwa dada Rehema Fredrick Fussi(Mama Latif) alfajiri ya leo kuelezea kifo cha Steven Kanumba na ndipo nilipokurupuka usingizini na kuanza kuwapigia ndugu na jamaa zangu wa karibu lakini wakati nikifanya yote hayo ndipo nilipoingia katika mtandao wa jamii (facebook) na kukuta salamu za msiba, nilishikwa na mshangao na bumbuwazi, taarifa zilianza kuenea jijini Dar es salaam kiasi cha saa nane na nusu usiku kuwa Steven Kanumba amefariki. Habari ambazo zina uhakika ni kuwa maiti yake ilikuwa tayari imekwishapelekwa mochwari Muhimbili. Sababu ya kifo bado ni utata kwani kuna maelezo kuwa alianguka ghafla, kukiwa na maelezo mengine kuwa alifariki usingizini. Na wengine wanasema amepata ajali. Pamoja na yote Mungu Amlaze Pema Kanumba, tulimpenda lakini Mungu amempenda zaidi

Jumatano, 18 Januari 2012

R.I.P MBUNGE MTEMA- AMEZIKWA LEO HUKO IFAKARA



Marehemu Mtema akiagwa leo wakati ya misa ya mazishi huko Ifakara.
Naibu Spika, Job Ngugai (kushoto) akiwa na Mwenyekiti wa CHADEMA, Kiongozi wa Kambi ya Upinzania na Mbunge wa Hai, Mheshimiwa Freeman Mbowe pamoja na Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA na Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Mheshimiwa Zitto Kabwe wakifuatilia kwa makini Misa Maalum ya Mazishi ya aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalum Chadema, Marehemu Regia Mtema Ifakara leo.…
credits; globalpublishers.info

Ijumaa, 30 Desemba 2011

MTANGAZAJI MAARUFU WA ITV NA BAADAE BBC AFARIKI DUNIA LEO HII, NI JOHN NGAHYOMA.

Mpiganaji John Ngahyoma afariki dunia
HABARI ILIYOTUFIKIA HIVI PUNDE INAELEZA KUWA,ALIYEKUWA MTANGAZAJI WA ITV/RADIO ONE MIAKA YA NYUMA NA BAADAE KUHAMIA KWENYE SHIRIKA LA UTANGAZAJI LA UINGEREZA (BBC),BW. JOHN NGAYOMA AMEFARIKI DUNIA MAPEMA LEO ASUBUHI.
HAYATI NGAHYOMA AMBAYE AMEFIKWA NA MAUTI LEO AKIWA HOSPITALI AMBAKO ALIKUWA AKIPATIWA MATIBABU YA MARADHI YALIYOKUWA YAKIMSUMBUA KWA MUDA MREFU AMBAPO ALIENDA MPAKA NCHINI INDIA KWA MATIBABU YA MARADHI YAKE HAYO BILA MAFANIKIO.
MSIBA UPO NYUMBANI KWA MAREHEMU MAENEO YA TABATA SEGEREA NA TARATIBU ZOTE BADO ZINAENDELEA KUFANYIKA.

Jumapili, 31 Julai 2011

SONGEA; MEYA WA MANISPAA YA SONGEA MH. ALLI MANYA AMEFARIKI DUNIA LEO AKIWA HOSPITALI YA PERAMIHO

Marehemu Alli Manya wa kwanza kulia enzi za uhai wake, alikuwa meya wa manispaa ya Songea pia diwani wa kata ya Lizaboni huko Songea, mazishi yanatarajiwa kufanyika kesho huko Lizaboni songea,KWA MUNGU KILA KIUMBE KITARUDI KWAKE,AMINA.

Jumapili, 24 Julai 2011

BURIANI MHARIRI WA GAZETI LA RAI, BW. DAN MWAKITELEKO

L
Gari aliyokuwa akiendesha marehemu, hapa ni baada ya kupata ajali kwa kuingia chini ya tela lililoegeshwa kando ya barabara almaarufu vicheche.

Marehemu Dan Mwakiteleko aliyefariki jana asubuhi kitengo cha MOI hospitali ya Taifa Muhimbili baada ya kupata ajali yagari maeneo ya TOT Tabata usiku akiwa anatokea kazini kuandaa gazeti la RAI la juzi, Mungu ailaze roho ya marehemu mahala pema peponi, AMEN.

Jumamosi, 21 Mei 2011

MWANAMIELEKA WA WWE AFARIKI DUNIA.



Gwiji wa mieleka ya Kimarekani Randy Savage au maarufu kwa jina la Macho Man
Saturday, May 21, 2011 12:02 AM
Gwiji wa mieleka wa Marekani, Randy Savage au maarufu kwa jina la Macho Man amefariki dunia kutokana na ajali ya gari.
Gwiji wa mieleka ya Kimarekani Randy Savage au maarufu kwa jina la Macho Man ameiaga dunia asubuhi ya leo kwa saa za marekani, (Majira ya saa 11 jioni kwa saa za TZ) baada ya kupata ajali ya gari karibu na nyumba yake iliyopo kwenye kitongoji cha Seminole, Florida.

Macho Man amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 58 na alikuwa maarufu sana duniani kutokana na umahiri wake kwenye mieleka kuanzia kwenye miaka ya 1980.

Macho Man alipata ajali baada ya kushindwa kuukontroo usukani wa gari lake la mwaka 2009 modeli ya Jeep Wrangler alilokuwa akiliendesha.

Taarifa zilisema kuwa gari lake lilivuka zege linalotenganisha barabara na kwenda upande wa pili wa barabara ambapo lilisimama baada ya kuugonga mti uliopo pembeni ya barabara.

Alifariki kwenye hospitali ya jirani kutokana na majeraha aliyopata, taarifa ya polisi imethibitisha kuwa Macho Man hakuwa akiliendesha gari hilo huku amelewa.

Macho Man katika anga ya mieleka aliwahi kuwa bingwa wa WWE mara mbili, bingwa wa dunia wa uzito wa juu kwenye mieleka mara mbili na pia alikuwa bingwa wa mabara kwa miezi 14.

Taarifa kamili juu ya sababu ya kifo chake itatolewa baada ya uchunguzi wa maiti yake kukamilika.

LEO NI KUMBUKIZI YA MIAKA 15 TOKEA NDUGU ZETU TAKRIBANI 800 WAPOTEZE MAISHA KWA AJALI YA MV BUKOBA HUKO ZIWA VICTORIA.

Mnara wa kumbukumbu, upo eneo walilozikwa wahanga wa ajali hiyo.

MV Bukoba ikiwa imeshazama tayari na kugeuka juu chini.

SHEIKH YAHYA HUSSEIN AFARIKI DUNIA JANA ALFAJIRI AKIWA NJIANI KUPELEKWA HOSPITALI. MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU MAHALA PEMA PEPONI, AMIN.

Marehemu Sheikh Yahya Hussein aliyekuwa mtabiri/mnajimu maarufu pande za Afrika Mashariki na Kati

Alhamisi, 19 Mei 2011

MAZEMBE JOSEPH NYERERE AFARIKI DUNIA USIKU WA KUAMKIA JANA HOSPITALI MUHIMBILI.

Marehemu Mazembe Joseph Nyerere.
Familia ya Nyerere na Burito inasikitika kutangaza kifo cha mpendwa wao Mazembe Joseph Nyerere, mipango ya mazishi inafanywa nyumbani Mtaa wa Longido, Upanga Dar es salaam.

Jumamosi, 2 Aprili 2011

ADAM LUSEKELO IS NO MORE AT ALL

At foolish day 1/4/11 many people denied the news that the giant deceitful views writer has passed away,thinking that people publish the story only to enlish the foolish day, all of them mistaken themselves, It is true that Adam Lusekelo of Sunday News/BBC reporter has died on thursday night this week from longterm diabetic problems, REST IN PEACE.