Jumatano, 8 Juni 2011

MUSTAFA A. MKULLO AWASILISHA BAJETI YA SERIKALI YENYE MATUMAINI KIASI KWA WANANCHI. SOMA SEHEMU YA BAJETI HIYO..

Bajeti imewakumbuka hawa?

............ Sheria ya Ushuru wa Bidhaa, SURA 147;Mheshimiwa Spika, marekebisho ya mfumo wa kodi
j) Marekebisho madogo madogo katika baadhi ya sheria
za kodi;
k) Marekebisho ya Ada na Tozo Mbalimbali za Wizara,
Mikoa na Idara zinazojitegemea;
l) Sheria ya Forodha ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, ya
mwaka 2004;
A. Sheria ya Kodi ya Ongezeko la Thamani, SURA 148
75.
kuboresha uzalishaji katika Sekta za Kilimo, Mifugo, Viwanda,
Biashara na Utalii na kuziwezesha kuchangia zaidi kwenye pato
la Taifa, napendekeza kufanya marekebisho katika Sheria ya
Kodi ya Ongezeko la Thamani, SURA 148 kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Spika, ili kuhamasisha uwekezaji na
90
i)
vya Zana za kilimo zifuatazo:- fyekeo (threshers),
mashine za kukausha na kukoboa mpunga (rice dryers
and mills), mashine za kupandia mbegu (planters), na
matrekta ya kukokota kwa mkono (power tillers).
Kusamehe Kodi ya Ongezeko la Thamani kwenye Vipuri
ii)
cha kuku (NASCOR Pellet Feed). Hatua hii ina lengo la
kuhamasisha uwekezaji katika ufugaji wa kuku hapa
nchini;
Kusamehe Kodi ya Ongezeko la Thamani kwenye chakula
iii)
(Nylon Fishing Twine) zinazotumika kutengeneza nyavu
za kuvulia samaki. Hatua hii inalenga katika kupunguza
gharama za uzalishaji na kuendeleza sekta ya uvuvi hapa
nchini;
Kusamehe Kodi ya Ongezeko la Thamani kwenye nyuzi
iv)
vya mashine za kunyunyiza na kutifua udongo (sprayers
Kusamehe Kodi ya Ongezeko la Thamani kwenye vipuri
91
and harrows) na mashine za kupanda nafaka (grain
conveyors); na
v)
mauzo ya rejareja kwa bidhaa za ndani zinazouzwa kwa
abiria ambao sio raia wa Tanzania wanaosafiri nje ya
nchi. Utaratibu huu utaanza kutekelezwa kwa kuanzia na
Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius
Nyerere na Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa
Kilimanjaro kwa mauzo ya thamani ya shilingi 400,000 na
zaidi. Utekelezaji wa utaratibu huu mpya utaanza rasmi
tarehe 1 Januari 2012.
76.
marekebisho katika Sheria ya Kodi ya Ongezeko la Thamani,
SURA 148 kwa nia ya kuongeza mapato na kuhamasisha
Mashirika na Taasisi mbalimbali ziweze kuchangia katika juhudi
za serikali za kuboresha huduma katika sekta ya elimu.
Kuanzisha utaratibu wa marejesho ya Kodi kwenyeMheshimiwa Spika, napendekeza pia kufanya
92
vi)
kwenye kuuza na kupangisha majengo ya kuishi ya
nyumba za Shirika la Nyumba la Taifa (NHC);
Kuondoa msamaha wa Kodi ya Ongezeko la Thamani
vii)
uliokuwa unatolewa kwa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali
(Non Governmental Organizations). Hatua hii haitazihusu
Taasisi za Kidini (Religious Organizations); na
Kuondoa unafuu wa Kodi ya Ongezeko la Thamani
viii)
Mashirika yasiyo ya kiserikali (Non Governmental
Organizations) kwa vifaa vya matumizi binafsi ya
kawaida (household consumables) kama vile vyakula,
mavazi, na vifaa kama sabuni ambavyo vinatolewa
Kutoa unafuu wa Kodi ya Ongezeko la Thamani kwa
93
msaada kwenye vituo mahsusi vya kulelea watoto yatima
na shule.
Hatua hizi katika Kodi ya Ongezeko la Thamani kwa
pamoja zitaongeza mapato ya Serikali kwa kiasi cha
shilingi
B. Sheria ya Kodi ya Mapato, SURA 332
milioni 71,518.9.
77.
ya sheria ya Kodi ya Mapato, SURA 332 kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Spika, napendekeza kufanya marekebisho
i)
wafanyakazi wa Serikali na wanaofanya kazi kwenye
Taasisi zinazopata ruzuku kutoka kwenye bajeti ya
Serikali..
Kusamehe kodi ya mapato kwenye posho wanazolipwa
94
ii)
kwa kutumia ndege za nje. Hatua hii inalenga katika
kuhamasisha mauzo ya samaki nje ya nchi.
Hatua hizi za Kodi ya Mapato zitapunguza mapato ya
Serikali kwa kiasi cha shilingi
C. Sheria ya Ushuru wa Bidhaa, SURA 147
Kufuta Kodi ya Zuio kwa usafirishaji wa samaki nje ya nchimilioni 20,287.5
78.
katika Sheria ya Ushuru wa Bidhaa, SURA 147 kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Spika, Napendekeza kufanya marekebisho
i)
kuendeshea mitambo kutoka shilingi 80 hadi shilingi 40
kwa lita ili kupunguza gharama za uzalishaji wa bidhaa
hapa nchini;
Kupunguza ushuru wa bidhaa kwenye mafuta mazito ya
95
ii)
120 kwenye mifuko ya plastiki za microns 30 na zaidi
yaani Polymers of ethylene na nyinginezo za (HS. Code
3923.2900).
Kutoza ushuru wa bidhaa wa asilimia 50 badala ya asilimia
iii)
bidhaa mbalimbali isipokuwa zile za mafuta ya Petroli
kama ifuatavyo: -
a) Vinywaji baridi kutoka shilingi 63 kwa lita hadi shilingi 69
kwa lita;
b) Bia inayotengenezwa na nafaka ya hapa nchini na ambayo
haijaoteshwa, kutoka shilingi 226 kwa lita hadi shilingi 249
kwa lita;
c) Bia nyingine zote, kutoka shilingi 382 kwa lita hadi shilingi
420 kwa lita;
Kurekebisha kwa asilimia 10 viwango vya Ushuru wa
96
d) Mvinyo uliotengenezwa kwa zabibu inayozalishwa nje ya
nchi kwa kiwango kinachozidi asilimia 25, kutoka shilingi
1,223 kwa lita hadi shilingi 1,345 kwa lita;
e) Mvinyo uliotengenezwa kwa Zabibu inayozalishwa hapa
nchini kwa kiwango kinachozidi asilimia 75 utatozwa
shilingi 420 kwa lita; na
f) Vinywaji vikali, kutoka shilingi 1,812 kwa lita hadi shilingi
1,993 kwa lita.
(iv) Kurekebisha viwango vya Ushuru wa bidhaa kwenye
sigara kama ifuatavyo: -
a) Sigara zisizo na kichungi na zinazotengenezwa kutokana na
tumbaku inayozalishwa hapa nchini kwa kiwango cha
angalau asilimia 75, kutoka shilingi 6,209 hadi shilingi
6,830 kwa sigara elfu moja;
97
b) Sigara zenye kichungi na zinazotengenezwa kutokana na
tumbaku inayozalishwa hapa nchini kwa kiwango cha
angalau asilimia 75, kutoka shilingi 14,649 hadi shilingi
16,114;
c) Sigara nyingine zenye sifa tofauti na (a) na (b) kutoka
shilingi 26,604 hadi shilingi 29,264 kwa sigara elfu moja;
d) Tumbaku ambayo iko tayari kutengeneza sigara (cut filler)
kutoka shilingi 13,436 hadi shilingi 14,780 kwa kilo; na
e) Ushuru wa (Cigar) unabaki asilimia 30.
Hatua hizi katika Ushuru wa Bidhaa kwa pamoja
zinatarajiwa kuongeza mapato ya Serikali kwa kiasi cha shilingi
milioni 99,521.5
98
D. Sheria ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi, SURA 82
79.
kwenye sheria ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi, SURA 82
kama ifuatavyo:
Mheshimiwa Spika, napendekeza kufanya marekebisho
i)
yatokanayo na tozo ya kuendeleza ufundi stadi (Skills
Development Levy) ya asilimia 6 ili asilimia 4 zipelekwe
kwenye Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu,
na asilimia 2 zipelekwe Mamlaka ya Elimu na Mafunzo
ya Ufundi Stadi (Vocational Education and Training
Authority - “VETA”). Lengo la hatua hii ni kuongeza
fedha za mikopo kwa wanafunzi wa Elimu ya Juu.
Hatua hii katika Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi
haitarajiwi kupunguza wala kuongeza mapato ya
Serikali.
Kufanya marekebisho katika mgawanyo wa mapato
99
E. Sheria ya Ushuru wa Stempu, SURA 189
80.
ya Ushuru wa Stempu, SURA 189 kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Spika, napendekeza kufanya marekebisho
i)
(Asset) unapohamishiwa katika chombo maalum
(Kampuni) cha kutekeleza na kusimamia uzalishaji wa
kipato (Special Purpose Vehicle “SPV”) kwa madhumuni
ya kutoa dhamana zinazotegemea hiyo mali ambayo
umiliki wake umehamishwa. Hatua hii inalenga katika
kuhamasisha miradi ya uwekezaji inayohitaji fedha
nyingi, mfano; miradi ya barabara, madaraja, nishati na
maji. Aidha, ni njia mbadala ya mabenki ya upatikanaji
wa fedha za kugharamia miradi.
Hatua hii ya ushuru wa stempu haitapunguza mapato
ya Serikali bali inalenga katika kuhamasisha utunzaji wa
Kusamehe ushuru wa stempu wakati umiliki wa mali
100
akiba na kuchochea uwekezaji (Savings Mobilization and
Investment Promotion).
F. Sheria ya Ushuru wa Mafuta ya Petroli, SURA 220
81.
katika Sheria ya Ushuru wa mafuta ya petroli, SURA 220 kama
ifuatavyo:
Mheshimiwa Spika, napendekeza kufanya marekebisho
i)
mafuta yanayotumika kwenye kuendesha meli, na vifaa
vingine vinavyotumika katika utafiti wa mafuta na gesi na
msamaha huu utatolewa kupitia Tangazo la Serikali. Aidha,
maombi ya msamaha yatahakikiwa na kupitishwa na Shirika
la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) kabla ya
kuwasilishwa Wizara ya Fedha. Hatua hii inalenga katika
kutoa unafuu wa gharama kwa Kampuni zinazofanya utafiti
wa mafuta na gesi.
Kusamehe Ushuru wa Mafuta ya Petroli unaotozwa kwenye
101
ii)
refunds) kwenye mafuta yanayonunuliwa na Kampuni za
madini, Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) itaanzisha
utaratibu wa kuweka kiasi cha fedha kwenye Akaunti
maalum (escrow account) ambacho kinawiana na kiwango
cha mahitaji ya mafuta kwa mwezi. Aidha Kampuni
itaruhusiwa kununua mafuta kwenye matanki ya Kampuni za
waagizaji wa mafuta bila ya kulipia kodi kwa kiwango cha
fedha ilichoweka kwenye akaunti. Endapo mahitaji ya mafuta
kwa mwezi yatakuwa makubwa zaidi ya kiwango ilichoweka
kwenye akaunti, Kampuni hiyo itawajibika kuongeza fedha za
ziada zenye kukidhi mahitaji yake. Hatua hii inatarajiwa
kutatua tatizo la ucheleweshaji wa marejesho ya kodi
iliyolipwa kwenye mafuta.
Ili kutatua tatizo la ucheleweshaji wa marejesho ya kodi (tax
102
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) itaandaa utaratibu wa
utekelezaji utakaohusisha kampuni za madini na kampuni za
mafuta.
Hatua hizi kwa pamoja zitapunguza mapato ya Serikali kwa
shilingi
G. Sheria ya Leseni ya Biashara, SURA 208
milioni 2,007.6
82.
katika Sheria ya Leseni ya Biashara, SURA 208 ili kutoza ada ya
leseni ya biashara kwa viwango na maeneo yafuatayo: -
a) Mamlaka za Miji (Majiji, Manispaa na Miji) zitoze shilingi
50,000 kwa mwaka kwa kila aina ya biashara inayostahili
Mheshimiwa Spika, napendekeza kufanya marekebisho
103
kupewa leseni ya biashara (isipokuwa ya vileo)
inayoendeshwa katika maeneo ya mamlaka hizo.
b) Halmashauri za Wilaya zitoze na kukusanya Ada ya leseni
ya biashara ya shilingi 30,000 kwa mwaka kwa biashara
zinazoendeshwa katika maeneo ya miji midogo na vituo
vya biashara.
c) Halmashauri za vijiji zitoze na kukusanya shilingi 10,000
kwa mwaka kwa kila biashara inayoendeshwa katika
maeneo yake.
Lengo la hatua hii ni kuimarisha usimamizi wa Kanuni za
biashara hapa nchini na kuwianisha ukuaji wa biashara na
mapato yanayokusanywa. Pia itaongeza mapato kwa
Serikali za Mitaa na kuongeza uwezo katika kuhimili
mahitaji yao. Aidha, utekelezaji wa hatua hii unazingatia
Sera ya Serikali ya ugatuaji madaraka kwa wananchi
(Decentralization by Devolution “D by D”).
104
H. Sheria ya Fedha ya Serikali za Mitaa, SURA 290
83.
katika Sheria ya Fedha ya Serikali za Mitaa SURA 290 ili
kuziwezesha Serikali za Mitaa kutoza ada ya leseni ya biashara
kwa viwango na maeneo yaliyoainishwa kwenye sheria ya leseni
ya biashara.
Mheshimiwa Spika, napendekeza kufanya marekebisho
I. Sheria ya Usalama Barabarani, SURA168
84.
Sheria ya Usalama Barabarani, Sura, 168 ili kuongeza ukomo wa
kiwango cha faini inayotozwa kwa kufanya makosa wakati wa
uendeshaji gari barabarani (Traffic Notification Fee) kutoka
shilingi 20,000 hadi shilingi 300,000.
Mheshimiwa Spika, napendekeza kufanya marekebisho ya
105
J. Marekebisho madogo madogo katika baadhi ya Sheria
za Kodi
85.
mengine madogo madogo yasiyo ya kisera katika Sheria
mbalimbali za kodi ili ziwe sanjari na azma ya kurahisisha
utekelezaji wake.
Mheshimiwa Spika, napendekeza kufanya marekebisho
K. Marekebisho ya Ada na Tozo Mbalimbali za Wizara,
Mikoa na Idara zinazojitegemea.
86.
ya viwango vya ada na tozo mbali mbali zinazotozwa na Wizara,
Mikoa na Idara zinazojitegemea ili kuvihuisha kulingana na hali
halisi ya ukuaji wa uchumi.
Mheshimiwa Spika, napendekeza kufanya marekebisho
106
L. Sheria ya Forodha ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, ya
mwaka 2004
87.
Mawaziri wa Fedha wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (Pre-Budget
Consultations of EAC Ministers for Finance) kilichofanyika tarehe
7 Mei 2011 jijini Kampala, Uganda; kilipendekeza marekebisho
ya viwango vya Ushuru wa pamoja wa Forodha (EAC Common
External Tariff “CET”) na Sheria ya Forodha ya Jumuiya ya Afrika
Mashariki (EAC Customs Management Act, 2004). Marekebisho
hayo yanalenga katika kukuza Sekta za Viwanda, Usafirishaji,
Mifugo, Biashara na Utalii. Aidha yanalenga pia katika kuboresha
afya ya jamii na kuimarisha ulinzi na usalama wa raia na mali
zao.
Mheshimiwa Spika, kikao cha maandalizi ya Bajeti cha
107
88.
kufanyiwa marekebisho kwenye viwango vya Ushuru wa Pamoja
wa Forodha (EAC Common External Tariff) ni yafuatayo:-
i) Tanzania iruhusiwe kutoza ushuru wa forodha wa
asilimia 10 badala ya asilimia 35 kwenye ngano
inayotambuliwa katika HS Code 1001.90.20 na HS
Code 1001.90.90 kwa muda wa mwaka mmoja. Lengo
la hatua hii ni kupunguza gharama za uingizaji nchini
wa bidhaa hiyo na kuwezesha walaji kupata vyakula
kwa bei nafuu.
ii) Kutoa msamaha wa ushuru wa forodha (duty
remission) kwenye malighafi ya kutengeneza sabuni
(Palm Stearin, RBD) inayotambuliwa katika HS Code
1511.90.40 kwa kipindi cha mwaka mmoja. Hatua hii
inalenga kutoa unafuu wa kodi kwenye viwanda
Mheshimiwa Spika, maeneo yanayopendekezwa
108
vidogo na vya kati vya kutengeneza sabuni hapa
nchini.
iii) Kutenganisha malighafi zinazotambulika katika HS
Code 2710.19.59 ili kutoa msamaha wa ushuru wa
forodha (duty remission) kwenye malighafi za
kutengeneza manukato na sabuni (white oil). Hatua
hii inalenga katika kupunguza gharama za uzalishaji
viwandani.
iv) Kutoa msamaha wa ushuru wa forodha (duty
remission) kwenye malighafi za kutengeneza maganda
ya viberiti (duplex boards) yanayotambuliwa katika HS
Code 4810.92.00. Hatua hii inalenga katika kupunguza
gharama za uzalishaji na kulinda Viwanda vya Viberiti
kutokana na ushindani wa viberiti vinavyoagizwa nje.
109
v) Kutoza ushuru wa forodha wa asilimia 10 badala ya
asilimia 0 kwenye waya za chuma ambazo
zimenakisiwa na zink (Galvanized Plated/Coated Wire),
zinazotambuliwa katika HS Code 7217.20.00 kwa kuwa
waya ambazo hazikunakisiwa (Non Plated/Coated
Wire) hutozwa ushuru wa forodha wa asilimia 10.
Lengo la hatua hii ni kuwianisha ushuru wa malighafi
inayotumika kuzalisha bidhaa hii ili iendane na
kanuni/taratibu za kutoza ushuru zinazozingatia
viwango vya usindikaji.
vi) Kupunguza ushuru wa forodha kwenye mifuko ya
plastiki ya kuhifadhia malighafi za matunda (aseptic
bags) kutoka asilimia 25 hadi asilimia 10
inayotambuliwa katika HS Code 3923.29.00 kwa
kipindi cha mwaka mmoja ili kupunguza gharama za
110
uzalishaji na kuhamasisha usindikaji wa mazao ya
matunda hapa nchini.
vi) Kutoa msamaha wa ushuru wa forodha (duty
remission) kwa kipindi cha mwaka mmoja kwenye shaba
ghafi (copper Cathodes) inayotambuliwa katika HS Code
7403.11.00. Hivi sasa bidhaa hii inatozwa ushuru wa
asilimia 10 ambapo shaba iliyotengenezwa kwa ukamilifu
(copper alloys/refined copper) hutozwa ushuru wa
asilimia 0, ambapo ni kinyume na matakwa ya sheria ya
ushuru wa forodha ya Jumuiya ya Afrika Mashariki ya
mwaka 2004. Lengo la hatua hii ni kuwianisha ushuru wa
malighafi inayotumika kuzalisha bidhaa hii ili iendane na
kanuni/taratibu za kutoza ushuru zinazozingatia viwango
vya usindikaji.
111
viii) Kutoa msamaha wa ushuru wa forodha (duty
remission) kwa waunganishaji wa majokofu
(refrigerators and freezers) ili walipe ushuru wa
forodha wa asilimia 10 badala ya asilimia 25 kwenye
vifaa vya kuunganisha majokofu hayo (component
parts and inputs for assemblers of refrigerators and
freezers). Hatua hii inalenga katika kuhamasisha
uzalishaji wa bidhaa hizo na kuongeza ajira hasa kwa
vijana.
ix) Kutenganisha malighafi zinazotambulika katika HS
Code 2309.90.00 ili kutoa msamaha wa ushuru wa
forodha kwenye malighafi za kutengeneza vyakula vya
mifugo (premixes). Lengo ni kutoa unafuu katika bei
za chakula cha mifugo na kuhamasisha ufugaji.
x) Kuendelea kutoza ushuru wa forodha wa asilimia 10
badala ya asilimia 25 kwenye mabasi yenye uwezo wa
112
kubeba abiria zaidi ya 25 yanayotambuliwa katika HS
Code 8702.10.99 na HS Code 8702.90.99.
xi) Kuendelea kutoza ushuru wa forodha wa asilimia 10
badala ya asilimia 25 kwenye magari ya mizigo yenye
uwezo kati ya tani 5 na tani 20 yanayotambuliwa
katika HS Code 8704.22.90 kwa muda wa mwaka
mmoja.
xii) Kuendelea kutoa msamaha wa ushuru wa forodha
kwenye magari ya mizigo yenye uwezo zaidi ya tani 20
yanayotambuliwa katika HS Code 8704.23.90 kwa
muda wa mwaka mmoja.
xiii) Kutoza ushuru wa forodha wa asilimia 10 badala ya
asilimia 25 kwenye mabasi yatakayoagizwa kwa ajili ya
mradi wa mabasi wa jiji la Dar es Salaam
yanayotambuliwa katika HS Code 8702.10.99 na HS
Code 8702.90.99 kwa muda wa mwaka mmoja.
113
(xiv) Kutenganisha bidhaa zinazotambulika katika HS Code
8703.90.10 ili kutoa msamaha wa ushuru wa forodha
kwenye pikipiki maalumu za kubeba wagonjwa
(motorcycle ambulances). Hatua hii inalenga
kuimarisha utoaji wa huduma ya kusafirisha wagonjwa
hasa katika maeneo ya vijijini.
xv) Kutenganisha virutubisho vya chakula
vinavyotambulika katika HS Code 2106.90.90 ili kutoza
ushuru wa forodha wa asilimia 10 badala ya asilimia
25 kwenye virutubisho vya vyakula vya binadamu
(food supplements) ili kuendana na Sera ya Serikali ya
kuboresha afya za wananchi.
xvi) Kutenganisha bidhaa zinazotambulika katika HS Code
9616.10.00 ili kutoza ushuru wa forodha wa asilimia
10 badala ya asilimia 25 kwenye malighafi za
114
kutengeneza vifaa vya kunyunyizia (scent sprays and
other similar toilet sprays and mounts and heads).
(xvii) Kuendelea kutoa msamaha wa ushuru wa forodha
kwenye matrekta ya kukokota mizigo
yanayotambuliwa katika HS Code 8701.20.90 kwa
muda wa mwaka mmoja. Hatua hii inalenga katika
kuboresha usafirishaji mizigo na kuongeza ufanisi
katika Sekta ya usafirishaji.
(xviii) Kuendelea kutoa msamaha wa ushuru wa forodha
kwenye migahawa ya Majeshi ya Ulinzi kwa kipindi cha
mwaka mmoja.
89.
kufanya marekebisho kwenye Sheria ya Forodha ya Jumuiya ya
Afrika Mashariki (EAC Customs Management Act, 2004) kama
ifuatavyo:-
Mheshimiwa Spika, Mawaziri wa Fedha walikubaliana
115
i)
Tano la Sheria ya Forodha ya Jumuiya ya Afrika Mashariki ili
kuliwezesha Jeshi la Polisi kunufaika na msamaha wa ushuru wa
forodha kama linavyonufaika Jeshi la Ulinzi. Hatua hii inalenga
katika kuimarisha usalama wa raia na mali zao.
Kufanya marekebisho katika kifungu cha pili (2) cha Jedwali la
ii)
Forodha ya Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa nia ya kutekeleza
yafuatayo:
a) Kutoa msamaha wa ushuru wa forodha kwenye mitego
ya mbung’o (tsetse fly traps). Hatua hii inalenga katika
kuchochea ukuaji wa kilimo na kuboresha mazingira ya
kuvutia utalii hapa nchini.
b) Kutoa msamaha wa ushuru wa forodha kwenye vifaa vya
kudhibiti usalama (security equipments: - hand held
metal detectors, walk through metal detectors, CCTV
cameras, bomb detectors and undercarriage mirrors).
Kufanya marekebisho katika Jedwali la Tano (5) la Sheria ya
116
Hatua hii inalenga katika kuboresha usalama wa raia na
mali zao.
c) Kutoa msamaha wa ushuru wa forodha kwenye magari
yanayoendeshwa kwa kutumia beteri (battery operated
vehicles/Golf carts). Hatua hii itaimarisha huduma za
kitalii na huduma za afya kwani magari haya yanaweza
kutumika kubeba wagonjwa ndani ya hospitali na kubeba
wageni na mizigo katika maeneo ya hoteli.
d) Kutoa msamaha wa Ushuru wa forodha kwenye magari
yanayotumika kubeba abiria katika viwanja vya ndege
(Apron buses) ili kuboresha huduma kwa wasafiri na
kuweka mazingira yenye kuvutia wageni na hasa watalii.
e) Kutoa msamaha wa ushuru wa forodha kwenye malighafi
za kutengeneza vifaa vinavyotumia mionzi ya jua (inputs
for manufacture of solar panels) kwa lengo la
kuhamasisha uzalishaji wa vifaa hivyo hapa nchini.
117
f) Kupunguza kiwango cha ada ya ukaguzi (Destination
Inspection Fee) kinachotozwa kwenye bidhaa za biashara
zinazotoka nje kutoka asilimia 1.2 ya thamani ya huduma
ya kuzifikisha hadi bandarini (FOB) na kuwa asilimia 0.6.
Hatua hii inalenga katika kupunguza muda wa kuondoa
mizigo bandarini na kupunguza gharama za uingizaji
bidhaa na hivyo kupunguza bei za bidhaa kutoka nje.
Hatua hizi kwa pamoja zinatarajiwa kupunguza mapato ya
Serikali kwa kiasi cha shilingi
M. Tarehe ya Kuanza Kutekeleza Hatua Mpya za Kodi
milioni 4,669.7
90.
zitaanza kutekelezwa tarehe 1 Julai, 2011, isipokuwa pale
ilipoelezwa vinginevyo.
Mheshimiwa Spika, hatua hizi za kodi zinazopendekezwa
118
MFUMO WA BAJETI KWA MWAKA 2011/12:
91.
pamoja na misingi na sera za bajeti, SURAya Bajeti
inaonesha kwamba jumla ya shilingi bilioni 13,525.9
zinahitajika kutumika katika kipindi cha 2011/12. Jumla ya
mapato yanayotarajiwa ni shilingi bilioni 13,525.9. Kati ya
mapato hayo, Serikali inalenga kukusanya mapato ya kodi na
yasiyo ya kodi ya jumla ya shilingi bilioni 6,775.9, sawa na
asilimia 17.2 ya Pato la Taifa. Aidha, mapato kutoka vyanzo
vya Halmashauri ni shilingi bilioni 350.5. Kadhalika, Serikali
inategemea kukopa kiasi cha shilingi bilioni 2,475.9 kutoka
vyanzo vya ndani na nje. Kati ya fedha hizo, shilingi bilioni
810.9 ni kwa ajili ya kulipia hatifungani na dhamana za
Mheshimiwa Spika, kwa kuzingatia sera za uchumi
119
Serikali zinazoiva, shilingi bilioni 393.4 ni mikopo kutokana
na mauzo ya hatifungani za Serikali na shilingi bilioni 1,271.6
zitatokana na mikopo yenye masharti ya kibiashara.
92.
wanatarajiwa kuendelea kuchangia bajeti kupitia misaada na
mikopo ya jumla ya shilingi bilioni 3,923.6. Kati ya fedha
hizo, shilingi bilioni 869.4 ni misaada na mikopo ya kibajeti
na shilingi bilioni 3,054.1 ni misaada na mikopo kwa ajili ya
miradi ya maendeleo, ikijumuisha mifuko ya kisekta.
93.
mwaka 2011/12 Serikali imepanga kutumia jumla ya shilingi
bilioni 13,525.9 kwa matumizi ya kawaida na maendeleo.
Kati ya fedha hizo, kiasi cha shilingi bilioni 8,600.3
Mheshimiwa Spika, washirika wa MaendeleoMheshimiwa Spika, kwa upande wa matumizi, katika
120
kimetengwa kwa ajili ya matumizi ya kawaida, ikijumuisha
shilingi bilioni 3,270.3 kwa ajili ya mishahara ya watumishi
wa Serikali, taasisi na wakala za Serikali na shilingi bilioni
1,910.4 kwa ajili ya Mfuko Mkuu wa Serikali. Aidha, jumla ya
shilingi bilioni 4,925.6 zimetengwa kwa ajili ya miradi ya
maendeleo, ambapo shilingi bilioni 1,871.5 ni fedha za ndani
na shilingi bilioni 3,054.1 ni fedha za nje.
94.
wa Bajeti yaliyotolewa hapo juu, Sura ya Bajeti kwa mwaka
2011/12 itakuwa kama ifuatavyo:
Mheshimiwa Spika, kutokana na maelezo ya mfumo
121
Mapato Shilingi milioni
A:
(i) Mapato ya Kodi (TRA) 6,228,836
(ii) Mapato Yasiyo ya Kodi 547,116
Mapato ya Ndani 6,775,952
B:
Mapato ya Halmashauri 350,496
C:
Mikopo na Misaada ya Nje 3,923,551
D:
Mikopo ya Ndani 1,204,262
E:
Mikopo ya Masharti ya Kibiashara 1,271,634
JUMLA YA MAPATO YOTE 13,525,895
F:
(i) Mfuko Mkuu wa Serikali 1,910,376
(ii) Mishahara 3,270,292
(iii)Matumizi Mengineyo 3,419,619
Wizara 2,727,472
Mikoa 49,981
Halmashauri 642,166
Matumizi ya Kawaida 8,600,287
G:
(i) Fedha za Ndani 1,871,471
(ii)Fedha za Nje 3,054,137
Matumizi ya Maendeleo 4,924,608
JUMLA YA MATUMIZI YOTE 13,525,895
122
HITIMISHO:
95.
mwendelezo wa juhudi za Serikali za kuwaletea maendeleo
wananchi. Bajeti hii imezingatia:
i) Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025;
ii) Mkakati wa Kukuza Uchumi na Kupunguza Umasikini
Awamu ya Pili (MKUKUTA II);
iii) Malengo ya Maendeleo ya Milenia 2015;
iv) Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010-2015;
v) Mkakati wa Pamoja wa Misaada Tanzania (MPAMITA);
vi) Mkakati wa Taifa wa Madeni; na
vii) Sera za Kijumla za Uchumi kwa mwaka 2011/12.
96.
zaidi, kila mwananchi anapaswa kujituma na kushiriki kikamilifu,
Mheshimiwa Spika, Bajeti ya mwaka 2011/12 niMheshimiwa Spika, ili kufikia malengo hayo mapema
123
kwa kutumia fursa zilizopo za kuzalisha mali na kujiongezea
kipato. Ni matumaini yangu kuwa utekelezaji sahihi wa Bajeti hii
utaiwezesha Serikali kuwaletea wananchi maendeleo
tunayokusudia. Bajeti ya mwaka 2011/12 imeandaliwa katika
kipindi ambacho nchi yetu inakabiliwa na changamoto ya
kiuchumi ikiwemo upungufu wa umeme na ongezeko la bei za
mafuta katika soko la dunia. Hali hii imetishia ustawi wa uchumi
na uwezo wa kukusanya mapato ya ndani. Serikali imejipanga
kukabiliana na changamoto hizi, ikiwa ni pamoja na kuharakisha
miradi ya uzalishaji umeme na uanzishwaji wa hifadhi kubwa ya
mafuta yanayoagizwa. Wakati Serikali ikichukua hatua hizi,
wananchi wanaombwa kuanza kutumia kwa uangalifu vyanzo
hivyo vya nishati, ili kupunguza gharama. Hivyo, ni matumaini ya
Serikali kwamba bajeti ya mwaka 2011/12 itatekelezwa kama
ilivyopangwa.
124
97.
imedhamiria kwa dhati kuendeleza misingi imara ya kujenga
uwezo katika kukusanya mapato ya ndani. Hili litawezekana kwa
kuwekeza katika vichocheo vya ukuaji uchumi ili kuongeza wigo
wa mapato ya ndani kwa lengo la kutuongezea uwezo wa
kujitegemea. Kama nilivyoeleza hapo awali, maeneo yafuatayo
ya kimkakati yatazingatiwa katika mgao wa rasilimali katika
muda wa kati: nishati ya umeme; reli, bandari; TEHAMA; maji;
kilimo na kulinda mafanikio yaliyopatikana katika sekta ya elimu
na afya. Hivyo basi, hatuna budi kila mmoja wetu na kwa
pamoja kuongeza ubunifu katika uzalishaji wenye tija
utakaoongeza Pato la Taifa na hatimaye kuondokana na
umaskini.
Mheshimiwa Spika, Serikali ya Awamu ya Nne,
125
98.
Waheshimiwa Wabunge wa Kamati ya Fedha na Uchumi na
Kamati nyingine za Kisekta. Pia, imezingatia mawazo na
mapendekezo ya wadau mbalimbali, wakiwemo
wafanyabiashara, wenye viwanda, sekta ya kilimo, utalii na
wengine wengi. Nawashukuru wote hao kwa mawazo na ushauri
wao.
99.
wapiga kura wangu wote wa Jimbo la Kilosa kwa kunichagua
tena kuwa Mbunge wao kwa kipindi kingine cha miaka mitano.
Napenda kuwaahidi kwamba tutashirikiana pamoja kuliletea
maendeleo Jimbo letu la Kilosa. Ninaamini kwamba
sitawaangusha. Mwisho nachukua pia nafasi hii kumshukuru
kipekee mke wangu mpendwa kwa kuwa msaada mkubwa
kwangu.
Mheshimiwa Spika, bajeti hii imezingatia ushauri waMheshimiwa Spika, nachukua fursa hii kuwashukuru126

d) Sheria ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi, SURA 82;
e) Sheria ya Ushuru wa Stempu, SURA 189;
f) Sheria ya ushuru wa Mafuta ya Petroli, SURA 220;
g) Sheria ya Leseni za Biashara, SURA 208;
h) Sheria ya Fedha ya Serikali za Mitaa, SURA 290;
i) Sheria ya Usalama Barabarani, SURA 168.

89

POLISI WAUA TENA HUKO MKOANI MARA.




JESHI la polisi limedaiwa kufanya tena muaji Mugumu mkoani Mara ambapo safari hii, askari wa Kituo cha Mugumu wilayani Serengeti, wamedaiwa kumuua Nyitamboka Mwita (28) kwa  kumpiga risasi akiwa nyumbani kwake kwa madai ya kuwa ni jambazi.

Mauaji ya Nyitamboka ambaye ni mkazi wa Kijiji cha Nyiboko, Kata ya Kisaka yaliyotokea Juni 6, mwaka huu yamekuja huku taarifa zikionyesha kuwa ni ya nne kufanywa na  polisi wa kituo hicho tangu Septemba mwaka 2010 hadi sasa.

Hata hivyo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara, Robert Boaz alipoulizwa alisema marehemu alitoka na panga na kumshambulia PC Sixbert kwa kukamata magazine na kumuangusha chini.Alisema  PC Rajabu akampiga risasi ya mkononi, lakini marehemu aliendelea kutaka kumshambulia na kwamba ndipo PC huyo akampiga risasi ya mgongoni iliyotokea kifuani na kumuua.

Alisema tukio hilo lilitokea saa 9:00 usiku na kwamba watu wengine wawili (majina yanahifadhiwa) walikamatwa katika msako huo. Watuhumiwa wote ni wakazi wa Kijiji cha Nyiboko na kwamba wanatuhumiwa kwa ujambazi wa kutumia silaha na kupora Tarime, Mwanza na Musoma.

Lakini mke wa marehemu, aliyejitambulisha kwa jina la  Benadeta Joseph, akisimulia mkasa huo, kwa maelezo kwamba alishuhudia tukio hilo, alisema kabla ya tukio,  saa 8;45 usiku, mumewe alitoka kwenye msiba nyumba ya jirani kwa mtu aliyetajwa kwa jina moja la Toli.

“Ghafla tulisikia mbwa wanabweka sana ikiashiria kuna watu nje ,mume wangu alilala kwa kuwa alikuwa amelewa, nikasikia milango
inagongwa kwa fujo sana, watu walisema wao ni polisi, waligonga sana bila kupumzika wengine madirishani,”alisema.

Alisema waliendelea kugonga wakisema, “wewe jambazi fungua, alikuwa uchi, nikamwamsha akakaa kitandani na kuuliza hao ni watu gani sungusungu au?, nikamwambia ni polisi akasema ngoja niende kuwasikiliza,”alisimulia Benadeta.

Shuhuda huyo aliliambia Mwananchi kuwa kutokana na kugonga kwa fujo mlango uliachia ukitaka kuanguka ambapo marehemu aliweka kiti kuzuia usianguke. Alisema kwa kuwa walikuwa wakigonga kwa fujo alitilia shaka hali hiyo na kutaka kuchukua panga, lakini aliamua kukubali kujisalimisha akiwa uchi.

“Alipotoka nje tu nikiwa nyuma yake nikasikia mlio wa risasi, mume wangu akapiga kelele wakampiga tena, akapepesuka na kuangukia nje ya uwanja,nikapiga kelele, wakapiga risasi juu na kuniamru kurudi ndani kulala,”alisema.

-Benadetha alibainisha kuwa kitendo hicho kiliwashtua wengine ambapo waliulizana, "mmempiga risasi, kwa nini mmemuua?," alisimulia.Alisema baada ya kuulizana walimmulika kwa tochi  kali na kuulizana kama ndiye waliyekusudia ambapo mmoja wa polisi hao alijibu kuwa ndiye na baada ya hapo waliita  gari la polisi aina ya pick up lililokuwa na rangi nyeusi alilodai lilikuwa limefichwa nje ya eneo lao.

"Wakati gari linaingia hapo nyumbani nililazimika kutoka na nguo ili kumstiri kwa kuwa alikuwa uchi, lakini polisi walinifukuza, walisema, unampelekea nani nguo, kwa sababu gani?, sisi tutambeba hivi hivi," alizidi kudai Benadeta akisema polisi hao walifanya hivyo wakijua mumewe ameishakufa.

Alisema hadi polisi hao walipoondoka hakuelezwa sababu za wao kuingia nyumbani kwao na kumuua mumewe, zaidi ya kumtishia kila alipotaka kujua kinachoendelea ambapo waliiondoka na kumwacha nyumbani hapo.

Hata hivyo alisema kuwa taarifa za polisi zinadai kuwa walimuua jambazi aliyekuwa wanapambana nao jambo alilosema siyo kweli.Hata hivyo, alikiri kuwepo kwa taarifa hivi karibuni zilizodai mumewe anahusishwa na mauaji ya aliyekuwa Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji cha Borenga, Mchanake Maho mwezi Aprili ambaye alichinjwa na watu wasiojulikana.

“Kuna taarifa kuwa kijana mmoja anaitwa Julius alikamatwa Musoma akihusishwa na mauaji hayo na kuwa aliwataja watu mbalimbali na hata usiku kwenye tukio inasemekana ndiye aliyeulizwa kuwa ndiye huyu akakiri ndiye akiwa ameishauawa,”alisema.

Mganga Mkuu wa Hospitali ya Nyerere DDH, Amosi Kittoh alikiri kupokea mwili wa marehemu huyo kwa ajili ya uchunguzi

Jumanne, 7 Juni 2011

NDUNDU - SOMANGA NOMA. KUNA KIPANDE KAMA CHA MITA MIA HIVI KIMEOZA KISHENZI CHIN, MDAU WENU WA BLOGU HII YUPO LINDI KIKAZI NA ATAKUWA AKIRUSHA VITU VYETU TOKEA HUKO KUANZIA SASA.

Safari ikianza alfajiri ya leo Ubungo

Basi la Akida ambalo mdau alikuwa ndani yake likiwa limekwama maeneo ya Somanga leo, Mwarami ambaye ni kondakta wa basi hilo akipunguza tope ili safari iendelee. 

Stendi kuu ya mabasi Lindi mjini leo mchana.

KASHFA KWA WATEULE WA KENYA MHIMILI WA MAHAKAMA.

Mutunga: Sishiriki mapenzi na wanaume

Willy
Dk Willy Mutunga

Jaji mkuu mteule nchini Kenya Dk Willy Mutuga amekanusha kama anashiriki mapenzi ya jinsia moja.
Mutunga aliyasema hayo alipokuwa anahojiwa na kamati maalum ya bunge.
Kamati hiyo ya bunge ilifanya vikao vyake vya siku mbili kusikia shutuma zilizotolewa dhidi ya walioteuliwa kuchukua nyadhifa za jaji mkuu,naibu jaji mkuu na mwendesha mashtaka mkuu.

Anashiriki

Hatua hii ilichukuliwa baada ya baadhi ya watu na hasa makanisa yakidai walioteuliwa si watu wanaozingatia maadili ya kifamilia kukiwemo na shutuma kuvaa hereni kwenye sikio la kushoto kwa Dk Mutunga ni ishara kwamba anashiriki mapenzi ya jinsia moja.
"Sishiriki mapenzi na wanaume,ila siwezi kuwabagua wanaume au wanawake wanaoshiriki mapenzi hayo,mimi mwenyewe mpwa wangu ni wa jamii hio",alisema Dk Mutunga.

Mchakato

Naibu jaji mkuu mteule Nancy Baraza pia alikuwa na muda wake wa kujitetea,alipoulizwa kwa nini alikita utafiti wake wa shahada ya uzamifu katika suala la haki za wapenzi wa jinsia moja.
Baraza alisema anafanya hivyo kwa kuwa alitaka kuwa mbunifu na kufanya utafiti wa kipekee ambao haujawahi kufanywa nchini Kenya.
Baada ya vikao hivyo kwa uma ambavyo vimetumika kuwatathmini tena wateule,majina hayo yatawasilishwa bungeni kwa ajili ya kupigiwa kura,ikiwa wataidhinishwa basi watachukuwa nyadhifa na iwapo watakataliwa bai mchakato wa usaili utaanza upya

Jumatatu, 6 Juni 2011

MBOWE KUPELEKWA ARUSHA KUSIKILIZA KESI YAKE.

<><><><>
<>
<><><><>
Askari polisi wakilinda kwenye kituo kikuu cha polisi kati anakoshikiliwa mwenyekiti wa Chadema Freeman MbowePicha na Fidelis Felix/Silvan Kiwale
CHADEMA, POLISI WAKWARUZANA, MBOWE KUTUA ARUSHA
Waandishi Wetu, Dar na Arusha
JESHI la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, jana lililazimika kuimarisha ulinzi katika Kituo chake Kikuu (Central) na baadhi ya maeneo ya jiji kukabiliana na tishio la wanachama wa Chadema kuandamana ili kushinikiza Mwenyekiti wao, Freeman Mbowe aliyekamatwa juzi aachiwe.Mbowe ambaye alikamatwa juzi ikiwa ni kutekeleza amri ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha iliyoamuru akamatwe popote alipo na afikishwe hapo kwa kutotii amri ya kufika mahakamani katika kesi inayomkabili, alitarajiwa kupelekwa huko wakati wowote kuanzia jana akiwa chini ya ulinzi.

Jana, vijana wa Chadema walikusanyika katika kituo hicho huku wakilaani kitendo cha kukamatwa kwa mwenyekiti wao huku wengine wakijikusanya katika vikundi vidogovidogo katika maeneo mbalimbali katika Barabara za Morogoro na Nyerere, lengo likiwa kushinikiza kiongozi huyo atolewe rumande na asisafirishwe kupelekwa Arusha.

Taarifa kutoka Arusha ambako kesi ya kiongozi huyo inatarajiwa kuendelea leo asubuhi zinaeleza kuwa polisi jana jioni waliendesha msako wa wanachama wa Chadema waliokuwa wakihamasishana kuhudhuria kwa wingi katika Mahakama ya Hakimu Mkazi wa Arusha.

Wanachama na mashabiki hao wa Chadema walidai kwamba kitendo cha kukamatwa kwa kiongozi huyo wa kambi ya upinzani bungeni ni mpango uliobuniwa na CCM wa kubinya demokrasia ya vyama vingi nchini.

Mbowe na Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho Bara, Zitto Kabwe walikamatwa katika maeneo tofauti nchini juzi. Wakati Mbowe alidaiwa kutotii amri ya mahakama, Zitto alidaiwa kuzidisha muda wakati wa kuhutubia mkutano wa hadhara mkoani Singida.

“Tumeongea na polisi, bado wanamng'ang'ania Mbowe. Msimamo wao ni kumpeleka Arusha, tuangalie utaratibu utakaotumika katika kumsafirisha,” alisema Mkurugenzi wa Mambo ya Nje wa Chadema, John Mnyika.

Baada ya kauli hiyo ya Mnyika ambaye pia ni Mbunge wa Ubunge, vijana wa chama hicho wakiongozwa na Diwani wa Kata ya Ubungo, Boniface Jacob walianza kuimba nyimbo za kulaani kukamatwa kwa mwenyekiti wao huku wakisema muziki wa Chadema polisi hawauwezi.

Ofisa mmoja mwadamizi wa Polisi Ilala ambaye hakujitambulisha jina aliwaambia vijana hao kuwa polisi na walishakubaliana na viongozi wa Chadema kuwa mtuhumiwa huyo amepangiwa utaratibu wa kusafirishwa kwenda Arusha kuhudhuria kesi yake.Ofisa huyo aliwataka wananchi waliokuwa kwenye eneo hilo kuondoka ili kupisha jeshi hilo kuendelea na kazi ya kutoa huduma kwa watu wengine.

“Tumeshaongeza na wakubwa wenu, hiki ni kituo cha polisi watu mbalimbali wanakuja kupata huduma hapa. Mtu haji kuangaliwa kwa aina hii ya hamasa na nyimbo, tunaomba muondoke,” alisema ofisa huyo.Kauli hiyo ilipingwa na vijana hao wakisema ofisa huyo ni mtu wa kawaida hawezi kuwaeleza mambo kama hayo.

“Sisi hapa tuna viongozi wetu mambo kama hayo tungeelezwa na kuelewa kama yangesemwa nao na si mtu wa kawaida kama wewe,”alisikika mmoja wa wanachama hao akisema kwa sauti.

Kauli hiyo ilimshangaza ofisa mwingine wa polisi aliyeibuka na kuhoji: “Mnasema huyu ni mtu wa kawaida? Akajibiwa “ndiyo”, “huyo siyo mtu wa kawaida."Vijana hao waliendelea na msimamo wao: “Sisi tunasema huyo ni mtu wa kawaida kwa sababu siyo kiongozi wetu, ndiyo maana tunasema angekuwa kiongozi wetu tungemwelewa.”

Kauli hiyo ilimlazimisha Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, Faustine Shilogile kujitokeza na kuwataka watu hao kuondoka katika eneo hilo kwa sababu kulikuwa na shughuli mbalimbali zilizokuwa zikiendelea.

“Tumeongea na viongozi wenu, tumeshakubaliana tunawaomba mtawanyike na sisi tuendelee na kazi, sitaki mkusanyiko wowote katika kituo cha polisi,” alisema Shilogile.Mara baada ya kauli hiyo gari la maji ya kuwasha lilianza kusogea walipokuwa wafuasi hao wa Chadema likitanguliwa na Polisi wa Kutuliza Ghasia waliokuwa wakiwafukuza katika eneo hilo.

Kundi hilo liliondoka na kuelekea makao makuu ya Chadema ambako Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk Willibrod Slaa alikuwa na mkutano na waandishi wa habari.

Msimamo wa Kamanda Kova
Akizungumzia mvutano huo, Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova alisema jeshi lake haliwezi kumwachia Mbowe kwa sababu wanaheshimu amri ya Mahakama.

Kova aliwaambia waandishi wa habari jana kwamba jeshi hilo lilipokea amri ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha ya kumkamata kiongozi huyo wa Chadema na kwamba hawaruhusiwi kuhoji lolote juu ya amri hiyo.

“Sisi kama jeshi la Polisi tumepokea amri ya mahakama ya kumtia hatiani Mheshimiwa Mbowe na hatuna mamlaka ya kumwachia huru hadi mahakama itoe amri ya kumwachia,”alisema.

Alisema sheria hairuhusu kuhoji sababu za amri inayotolewa na mahakama na kufafanua kuwa hizo ni sheria zilizotungwa na wabunge wenyewe.Alisema Mbowe anatarajiwa kusafirishwa chini ya ulinzi wa Polisi kwenda mkoani Arusha kujibu kesi inayomkabili na kwamba taratibu zote za safari tayari zimekamilika.

“Tunachokifanya ni maagizo ambayo yametoka ngazi ya juu kuhusu suala hili kwa hiyo Mbowe atapelekwa Arusha chini ya ulinzi wa polisi muda wowote kuanzia sasa alimradi awahi muda wake wa mahakama,”alisema Kova.

Alisema atapelekwa Arusha chini ya ulinzi wa polisi kwa sababu amekiuka masharti yake ya dhamana na kwamba tayari wamezungumza na baadhi ya viongozi wa vyama vya upinzani waliokwenda kumuona kiongozi huyo wa kambi yua upinzani bungeni jana.

Kova alisema kulingana na taratibu na sheria za Tanzania, mahakama ikitoa amri hakuna mtu anayeweza kuipinga.

Aliwataka wananchi watulie na kuipa fursa mahakama itekeleze sheria zilizotungwa na Bunge.Akizungumzia kukamatwa kwa Mbowe, Mnyika alisema hizo ni njama za kuudhalilisha upinzani na pia mbinu za kumtaka Mbunge huyo wa Hai asihudhurie kwenye Kikao cha Bunge la Bajeti.

“Endapo watashindwa kutumia busara za mazungumzo tuliyoyafanya kumwachia Mbowe, jambo hili tutalirudisha kwa wananchi na nguvu ya umma itatumika kusuluhisha tatizo hilo,” alisema.

Alisema amani ni tunda la haki lakini inaweza kupotea kama haki haitatendeka na kuongeza kuwa kuna watu ambao wanashutuma nzito za ufisadi, lakini hawachukuliwi hatua zozote isipokuwa viongozi wa upinzani.


Tamko la Dk Slaa
Dk Slaa alisema kesi zinazowakabili viongozi wa chama hicho na wabunge wa vyama vya upinzani vinalifedhehesha Bunge la Tanzania kimatifa.

“Ili mtuhumiwa akamatwe sheria iko wazi, notisi zilitakiwa kutolewa kwa mdhamini wake na pia kwa wakili, lakini kwa Mbowe haikuwa hivyo na hiyo inaonyesha ni agizo kutoka mahali Fulani,” alidai.

“Polisi mkoa wa Mwanza wametuma barua kwa Katibu wa Bunge kuomba kibali cha kwenda kumhoji Mbunge wa Jimbo la Busega, Dk Titus Kamani, iweje kwa wabunge wa upinzani kukamatwa bila utaratibu? Alihoji Dk Slaa.

Alisema kutokana na mazingira hayo kama Mbowe hatafikishwa leo mahakamani wabunge wa Chadema hawataingia bungeni.

Kuhusu uwakilishi kwenye kamati ya uongozi alisema hata kama Zitto atakuwa nje ya mahabusu, hataingia kuwakilisha upinzani kwa sababu anayetakiwa kumpa kibali cha kufanya hivyo yupo ndani.

Kuhusu kosa la Zitto kukamatwa na polisi alisema inashangaza kwa sababu alikuwa kwenye mkutano wa hadhara kama mbunge na alizidisha dakika 20 kwenye mkutano huo.

Alisema hiki siyo kipindi cha kampeni na Zitto ni kiongozi mwenye haki ya kufanya hivyo na kusisitiza kilichofanyika kimelenga kufifisha demokrasia nchini.

Profesa Lipumba aishambulia Polisi
Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba jana alifika Kituo cha Polisi Kati na kulaani kitendo cha kukamtwa kwa Mbowe akisema kinadidimiza demokrasia nchini.

Lipumba alisema chama chake kina mpango wa kuitisha maandamano makubwa kupinga kitendo cha kukamatwa Mbunge wa Viti Maalumu wa chama hicho, Magdalena Sakaya.

Alisema Mbowe hakusitahili kukamtwa kwa sababu yuko kwenye maandalizi ya hoja za upinzani bungeni kuhusu bajeti.

“Nimeshtuka kwa sababu huyo ni kiongozi wa kambi ya upinzani bungeni na kipindi hiki ni kipindi cha maandalizi ya bajeti naye anapaswa kuwa katika kazi ya kutunga hoja kwa sababu yuko kwenye Kamati ya Uongozi ya Bunge,” alisema Lipumba.

Alisema kumweka Mbowe katika misukosuko ni kuminya demokrasia ya vyama vingi hapa nchini.Lipumba alielezea kushangazwa na Spika wa Bunge, Anne Makinda kukaa kimya kuhusu vitendo hivyo na kusema alitarajia kutolea tamko.


Mnyika ataka Ofisi ya Bunge kuwajibika
Kwa upande wake, Mnyika aliitaka Ofisi ya Bunge kuwajibika kutokana na vitendo vya kukamatwa kwa wabunge wa vyama vya upinzani.Alisema tayari alishamwandikia barua Spika kuhoji hali hiyo kila wanapokuwa kwenye shughuli zao za kisiasa.

Wabunge wa Chadema kutangulia Arusha
Wakati polisi jana ikificha mpango wake wa namna itakavyomsafirisha Mbowe, baadhi ya wabunge walieleza nia yao ya kutangulia Arusha.

Wabunge waliothibitishia kufanya hivyo ni Grace Kilwelu Suzan Lyimo na Pauline Gekul.

Masheikh, wanazuoni watoa tamko
Jopo la Masheikh na wanazuoni wa Kiislamu nchini limewataka Watanzania kuzingatia utawala wa sheria na kutii amri za mamlaka zilizoundwa kwa mujibu wa katiba na sheria za nchi.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Katibu wa taasisi hiyo, Sheikh Khamis Mataka alisema suala linalomkabili Mbowe hivi sasa ni la kisheria na si la kisiasa hivyo Watanzania wasikubali suala hilo liwe ni sababu ya kufanya vitendo vya kisiasa kama vile maandamano au kuhamasisha kuchukuliwa kwa sheria mkononi kama kuvamia vituo vya polisi kwa nia ya kumtoa mtuhumiwa.

"Mambo haya ni kinyume cha sheria na kuvunja misingi ya utawala wa sheria tunayotaka itekelezwe na wote," alisema.

*Habari hii imeandikwa na Geofrey Nyang'oro, Aziza Masoud, Elizabeth Ernest, Boniface Meena Dar na Mosses Mashalla, Arusha

CHANZO; MWANANCHI

VIJANA U-23 WAIFUNGA NIGERIA, TAIFA STARS HOI.

 
Timu ya Taifa ya soka kwa wanaume wa umri wa chini ya miaka 23 (U23) imeshinda katika mpambano wao wa kwanza dhidi ya Nigeria katika mchezo wa kusaka nafasi ya kushiriki mashindano ya Olympic.

Tanzania imeshinda bao 1 lililofungwa na Thomas Ulimwengu katika dakika ya 81 na kuwaacha Nigeria waliokuwa wakicheza kwa kuzuia zaidi wakibaki na nyavu zao.

Kwa matokeo hayo, Tanzania inahitaji sare yoyote katika marudiano yatakayofanyika wiki mbili toka sasa ili iweze kusonga katika ngazi zinazofuata za michuano hiyo.

Kwa mechi ya African Nations Cup, mambo yaliingia shubiri huko mjini Bangue kwani timu ya Central African Republic iliibangua 2:1 timu ya Tanzania.

Matukio muhimu kama yalivyorekodiwa na tovuti ya BBC ni:

1315GMT: So we are learning that the CAR v Tanzania game will kick-off at 1500GMT - the head of the Taifa Stars delegation, Samwel Nyala, has told a local radio that the pitch in Bangui is bumpy but the Tanzanian team is in top mood.

1538GMT: In Bangui its approaching half-time and it's still goalless between Central African Republic and visiting Tanzania.

1550GMT HALF-TIME CAR 1-0 TANZANIA: The hosts, who have been dominating, score on the stroke of half-time.

1610GMT: Back playing in Bangui where hosts CAR lead 1-0 over Tanzania.

1636GMT: Tanzania are fighting back and Athuman Machupa is one of several Taifa Stars who has failed to convert good chances against the CAR.

1640GMT GOAL! CAR 1-1 Tanzania. Star striker Mbwana Samata, who has come on as a second-half substitute, equalises for Tanzania.

1646GMT GOAL! CAR 2-1 Tanzania. The hosts score what should be a winner in the last few minutes of the game.

1659GMT: FINAL SCORE CAR 2-1 Tanzania: That result means CAR are second in the group behind Morocco on goal difference - both teams have seven points. Tanzania are third now ahead of Algeria on goal difference.

Matokeo mengine ya mechi zilizochezwa siku ya leo, Jumapili 5, 2011 hadi chapisho hili linapotoka ni:
  • Group E: Mauritius 1-2 DR Congo - Result
  • Group C: Comoros 1-1 Libya - Result
  • Group K: Botswana 0-0 Malawi - Result
  • Group A: Zimbabwe 2-1 Mali - Result
  • Group B: Ethiopia 2-2 Nigeria - Result
  • Group H: Benin 2-6 Ivory Coast - Result
  • Group I: Swaziland 1-2 Sudan - Result
  • Group H: Burundi 3-1 Rwanda - Result
  • Group D: Central African Republic 2-1 Tanzania - Result
  • Group J: Angola 1-0 Kenya - Result
  • Group A: Liberia 1-0 Cape Verde (Latest)
  • Group B: Guinea v Madagascar
  • Group K: Tunisia 2-0 Chad (Latest)
  • Group G: Egypt v South Africa (1830GMT)

ZAIDI YA WATU 20 WAJERUIWA KATIKA MLIPUKO HUKO NAIROBI KENYA, MMOJA AHOFIWA KUFA.

 
At least 1 person died leaving at least 28 others injured on Sunday, when an explosion went off in downtown Nairobi and set a gas station on fire.

“One person has died from this explosion 28 others are still receiving treatment in hospitals around the city, the number of casualties might rise because businessmen and their customers were caught unaware,” Police Spokesman Erick Kiraithe told journalist late on Sunday.

AFP photographer said the blast went off around 11 a.m. local time near Nairobi's Kirinyaga Road injuring dozens of people and sending ambulances and police rushing to the scene. The injured were taken to a local hospital, where several were being treated for serious burns.

Omar Alwiya, a bus conductor, said he was sleeping at around 11 a.m. when he heard an explosion that shook the room he was in and filled it with dust. He rushed to the scene and found two shipping containers overturned, several cars destroyed and a fire at a gas station.

Prime Minister Raila Odinga visited the scene of the blast and said in a brief statement to reporters that at least 28 people had been injured.Dr. Peter Kamau Wanyoike said 29 people were admitted to Kenyatta National Hospital. Nine had burns on 60 percent of their body. Others were injured by falling glass or minor burns.

Authorities have not ruled whether the explosion was accidental or set on purpose,  “It is still too early to ascertain the cause but we have our team of the anti terrorism police, our bomb experts and the officers from the Criminal Investigations Department on the ground,” the Spokesman added.

Kenya has experienced bombings in the past, most recently in December on a bus that was set to travel to the Ugandan capital, Kampala. At least two people died in that attack.

The Somali militant group al-Shabab which controls vast swathes of neighbouring Somalia,has repeatedly threatened to attack Kenya because of its support for the U.N.-backed Somali government in Mogadishu.

WAUAJI WA ALBINO WAHUKUMIWA KIFO

WASHITAKIWA watatu kati ya watano waliokamatwa miaka mitatu iliyopita wakituhumiwa kumuua mtoto mlemavu wa ngozi (albino), Ester Charles Juni 3 walihukumiwa kunyongwa hadi kufa baada ya kutiwa hatiani na Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Tabora.
Jaji Laurence Kaduri aliyekuwa akisikiliza shauri hilo, aliwahukumu kunyongwa hadi kufa washitakiwa hao, Charles Kalamuyi (zungu), Masumbuko Madada (Sumbu) na Merdadi Maziku (Machunda) kutokana na kuridhika na ushahidi uliotolewa na upande wa mashitaka bila shaka yoyote.
Katika hukumu hiyo iliyosomwa kwa takribani saa nne, mshitakiwa mwingine Peter Mahina, aliachiwa huru baada ya kukosekana ushahidi wa kumuunganisha wakati mshitakiwa wa tano Malalija Jiduta, alifariki dunia akiwa rumande wakati kesi hiyo haijaanza kusikilizwa.
Awali upande wa mashitaka ukiongozwa na jopo la mawakili watatu Neema Ringo, Prudence Rweyongeza na Janeth Sekule, uliiambia Mahakama kuwa washitakiwa walitenda kosa hilo Oktoba 19, 2008.
Ilidaiwa kuwa siku hiyo katika kijiji cha Shilela Usala, wilayani Kahama mkoani Shinyanga, washitakiwa walimuua mtoto huyo kwa kumkata mapanga sehemu za mabega.
Kwa mujibu wa madai hayo, baada ya kutenda unyama huo washitakiwa walikinga damu yake na kutokomea nayo na kumwacha mlemavu huyo akiwa hajitambui na baadaye akapoteza maisha kutokana na kuvuja damu nyingi.
Serikali katika kesi hiyo iliwasilisha mashahidi watano na kupitia mawakili wake iliomba Mahakama itoe adhabu kali kwa washitakiwa kutokana na kitendo kibaya na cha kinyama walichofanya.
Washitakiwa kwa upande wao waliokuwa wakitetewa na mawakili Kamaliza Kayaga, Merdai Mutongole na Vedastus Lauriani waliiomba Mahakama iwaachilie huru wateja wao kwa madai kwamba hawakuhusika katika mauaji ya mtoto huyo, ombi ambalo lilitupiliwa mbali na Jaji Kadur

Jumapili, 5 Juni 2011

VIONGOZI NA BAADHI YA WAFUASI WA CHADEMA WAINGIA KITUO KIKUU CHA POLISI KUFUATILIA DHAMANA YA MWENYEKITI WAO. ULINZI MKALI WAIMARISHWA.

Wafuasi wa CHADEMA nje ya kituo kikuu cha polisi Dar es salaam

Mbunge wa Ubungo akiongea na waandishi wa habari

Wazee wa kazi wakiwa makini kwa lolote litakalotokea.

Profesa Abdallah Safari naye alikuwepo.

MBOWE ASWEKWA LUPANGO, KUSAFIRISHWA HADI ARUSHA AKAJIBU MASHTAKA.

Mh.Freeman Mbowe
 

Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Bw. Freeman Mbowe amekamatwa na jeshi la Polisi mkoani Dar es salaam kufuatia agizo la pili la Hakimu wa Mahama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Arusha baada ya kushindwa kujisalimisha mahakamani katika kesi inayomkabili ya kufanya kusanyiko usio halali mkoani Arusha tarehe 5 Januari 2011. Mbowe alikamatwa jana jijini Dar es Salaam wakati alipokwenda kujisalimisha katika kituo Kikuu cha Polisi. Habari zinasema kuwa Mbowe amelala Rumande na atasafirishwa kwenda Mjini Arusha kujibu shtaka linalomkabili. Polisi wameimarisha ulinzi katika kituo hicho

Jumamosi, 4 Juni 2011

PICHA YA LEO; TBC ENZI HIZO.

Wanamuziki wakirekodi katika studio za kizamani kama unavyoziona redio Sauti ya Dar es salaam. Inasemekana studio zilikuwa pale maeneo ya Mchikichini kilipo kiwanda cha bia hivi sasa.

Mtangazaji wa redio Sauti ya Dar es salaam enzi hizo akiwa kazini. hapo akipiga muziki kwa kutumia santuri enzi hizo miaka ya 1950 hivi.

YANGA YAITANGAZA TANZANIA

Clara Alphonce na Jessca Nangawe
UONGOZI wa klabu ya Yanga umesema kwamba, nchi ya Ujerumani na kituo cha kurusha matangazo cha SuperSports, wameonyesha nia ya kuisaidia klabu yao pamoja na soka la Tanzania kwa ujumla.

Kongamano hilo lililofanyika mjini Accra Mei 26 na 27 mwaka huu, pia lilihudhuriwa na Mkuu wa Maendeleo kutoka Shirikisho la Soka Duniani (FIFA), Cyril Loisel, aliyekuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Kombe la Dunia Afrika Kusini, Danny Jordan,wajumbe wa Shirikisho la Soka Afrika (CAF) na Mashirika yasiyo ya kiserikali.

Akizungumza Dar es Salaam jana, Mwenyekiti wa Yanga, Lloyd Nchunga alisema kuwa hayo yamo katika kongamano hilo la kimataifa lililokuwa likijadili soka ya Afrika na kutoa michango mbalimbali ya kuendeleza mchezo huo Afrika.

"Katika mkutano huo niliweza kuzungumza kwa kina na Mkurugenzi anayesimamia Ligi ya Bundesliga, Jog Daubitzer ambaye aliniahidi kuwa atafanya juhudi za kuanzisha mahusiano ya karibu kati ya timu ya Yanga na klabu mbambali za Tanzania zikiwemo na timu za nchi jirani za Afrika Mashariki," alisema Nchunga

Lloyd Nchunga
Alisema Mkurugenzi huyo wa Bundesliga amesema yupo tayari kuisaidia klabu ya Yanga kupitia soka la vijana.
Nchunga alisema kituo cha kurusha matangazo cha SuperSports cha Africa Kusini kupitia Mkurugenzi wa Masoko, Gary Rathbone, alisema watafanya jitihada za kurusha matangazo ya mpira pamoja na mambo mbalimbali kwa ajili ya kuinua kiwango cha soka nchini.

Aliongeza kuwa, wadau hao wa soka pia walijadili mikakati ya karne ya 21 katika Masoko, uongozi na utawala kwa ajili ya maendeleo ya soka Afrika

Ijumaa, 3 Juni 2011

MBOWE ANATAFUTWA NA MAHAKAMA.

Friday, June 03, 2011 11:16 AMMAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Arusha imeliagiza Jeshi la Polisi kumkamata Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA),Bw. Freeman Mbowe kwa kosa la kutofika mahakamani kutokana na kesi inayomkabili.
Hakimu Magesa alitoa hukumu hiyo baada ya mshitakiwa huyo kutofika mahakamani kujisalimisha katika kesi inayowakabili na viongozi wenzake wa juu wa chama hicho kwa kosa la kufanya mkusanyiko Januari 5 mwaka huu isivyo halali.

Wengine wanaojumlishwa katika kesi hiyo akiwemo Katibu Mkuu wa Chama hicho, Dkt. Willibrod Slaa, Bw. Phillemon Ndesamburo Mbunge wa Moshi Mjini na Bw. Godbless Lema Mbunge wa Arusha Mjini ambapo wao walijisalimisha

Washtakiwa wengine ni mchumba wa Dk. Slaa, Bi. Josephine
Mushumbusi, Bw. Richard Mtui, Bi. Aquiline Chuwa na Mwenyekiti wa chama hicho Mkoa wa Arusha, Bw. Samson Mwigamba.

Hakimu Magesa alitoa hukumu hiyo kwa mshitakiwa wa kwanza (Mbowe) baada ya kutolewa hati ya kumkamata au kujisalimisha mahakamani na matokeo yake hakufanya hivyo wala mdhamini wake naye hakufika.

“Hivyo kutokana na kitendo hicho ni kosa kisheria, Kimsingi si sahihi kutofika mahakamani bila taarifa hata kama alikuwa na udhuru”alisema Hakimu Magesa

Kesi hiyo imeahirishwa hadi Juni 24, mwaka huu.

MKULIMA AUAWA HUKO MANYARA

Mkulima auawa kinyama Tanzania

Polisi nchini Tanzania inapeleleza mauaji ya meneja na muwekezaji nchini humo Sifael Jackson.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Manyara kaskazini, Parmena Sumari ameiambia BBC kuwa maofisa wake wanaendelea kuwasaka wauaji wa mfanyabiashara huyo.

Mwandishi wa habari Benny Mwaipaja ameiambia BBC kuwa marehemu alivamiwa na kuuawa na genge lililokuwa na mikuki, magongo na mapanga akiwa ndani ya gari lake.
Mauaji haya yanatokea wakati kukiwa na upinzani mkubwa wa raia dhidi ya mpango wa serikali wa kupigia debe uwekezaji wa kilimo kwa kiwango kikubwa.
Uvamizi

Mwandishi huyo aliendelea kusema kuwa "Bw Jackson aliuawa kinyama na kukatwa kichwa na genge la hadi watu 15 siku ya Jumanne jioni.
Baadhi ya wakaazi wa mkoa huo wa Manyara wanaishutumu serikali kwa kutishia hali yao ya maisha kwa kugawa ardhi yao vipande vikubwa kwa wakulima wa kibiashara wa mashamba makubwa, wakiwemo wakulima wa kigeni.
raia wapinga ardhi kupewa wageni
serikali yataka ardhi itumiwe


Lakini serikali inasema kuwa lengo la sera hiyo ni kujaribu kuimarisha uzalishaji wa chakula na kuhakikisha kwamba ardhi inatumiwa kikamilifu.
Kwa uchache mashamba manne yamevamiwa mwaka huu karibu na mji wa Babati huko Manyara, ambako mazao yalichomwa na mali kuteketezwa kwa moto.
Waziri Mkuu Mizengo Pinda alituma ujumbe mkubwa wa Mawaziri wa serikali kwenda kupeleleza kuhusu mzozo huo.
Ujumbe huo uliwaonya wananchi katika maeneo walioyazuru dhidi ya vitendo vyao vya kuvamia na kuteketeza mali za watu la sivyo watakamatwa na kuhukumiwa.
Mwandishi huyu Mwaipaja alisema kuwa serikali ina wasiwasi kuwa ghasia hizo sasa zinaweza kuikosesha Tanzania wawekezaji ambao ina imani wangeweza kusaidia mpango wake wa kijani.
Kampeni ya serikali ya kutaka kilimo cha kiwango kikubwa kibiashara ni mabadiliko makubwa ukizingatia sera zilizokuwepo baada ya Uhuru zilizokuza na kupendelea Usoshalisti

Alhamisi, 2 Juni 2011

SEPP BLATTER ACHAGULIWA TENA FIFA.

Sepp Blatter na Afrika

Sepp Blatter ameteuliwa tena bila ya kupingwa kwa kipindi kingine cha miaka minne kuwa Rais wa Shirikisho la soka duniani FIFA.
Sepp
Sepp Blatter mara tu baada ya kuchaguliwa tena

Kuteuliwa kwa Bw Blatter kunafanyika huku kukiwa na mgogoro mkubwa ndani ya shirikisho hilo kuhusu madai ya rushwa katika mchakato wa kuwania nafasi za kuandaa michuano ya kombe la dunia mwaka 2018 na 2022.
Je, Sepp Blatter anagusa vipi soka barani Afrika? Mwandishi wetu Mohammed Allie ameandika tathmini ifuatayo kutoka Cape Town, Afrika Kusini.
Jibu la swali hili, litategemea unaongea na nani.
Nchini Afrika Kusini, Sepp Blatter anachukuliwa kuwa ama ni shujaa au ni muovu.

Ukakamavu

Wapenzi wengi wa soka wa Afrika ya Kusini wanaamini kwamba ni kutokana tu na juhudi na ukakamavu wa Rais wa FIFA ndio hatimae bara la Afrika lilipata fursa ya kuandaa michuano ya kombe la dunia mwaka uliopita; ikiwa ni mara ya kwanza katika historia ya miaka 80 ya michuano hiyo, na kwa ajili hiyo daima watamshukuru raia huyo wa Uswisi mwenye umri wa miaka 75.
Baada ya juhudi za Afrika Kusini kuandaa michuano ya kombe la dunia ya mwaka 2006 kushindwa katika hali ya utata mkubwa, Blatter aliazimia kuhakikisha kuwa kombe la dunia linakwenda Afrika kwa kuanzisha mfumo wa kupokezana kati ya mabara ya dunia ambapo nchi tano za Afrika zilichuana kuwania nafasi ya kutayarisha michuano ya 2010 .

Heshima

Serikali ya Afrika ya Kusini ilimtunukia Blatter heshima kuu ya Oliver Tambo kwa mchango wake wa kupeleka michuano ya kombe la dunia nchini humo.
Wengine wanaamini Blatter aliiburuza kamati ya matayarisho pamoja na serikali kujenga viwanja vipya na miundo mbinu iliyohusika na kombe la dunia vilivyogharimu fedha nyingi bila ya lazima wakati nchi ilikuwa na mahitaji mengine muhimu katika nyanja ya afya, umeme, maji na usafi.

Dikteta

Wanatoa mifano ya viwanja ambavyo havitumiki sana nchini humo kama urithi wa fedha ziliopotezwa. Wakosoaji wake pia wanamuona Blatter kuwa ni mtu mjanja na dikteta ambae aliidhibiti vilivyo Afrika ya Kusini katika kipindi kabla na wakati wa michuano ya kombe la dunia.

Hata hivyo si siri kwamba Afrika imenufaika sana wakati wa enzi ya miaka 13 ya Blatter kama Rais wa FIFA.
Ilikuwa chini ya uongozi wake kwamba uwakilishi wa Afrika katika michuano ya Kombe la Dunia uliongezeka kufikia mataifa matano na baadae kiwango cha rikodi cha mataifa sita katika michuano ya mwaka 2010 baada ya kujumuisha mwenyeji Afrika Kusini.

Mafunzo

Wakati wa utawala wake FIFA imewekeza takriban dola nusu billioni barani Afrika kupitia huduma, vituo vya mafunzo, mkiwemo viwanja vinavyoweza kutumika majira yote pamoja na mipango ya kutoa mafunzo kwa waandishi habari na maafisa wa utawala.
Kwa mfano kituo cha maendeleo cha Rwanda, kimezaa matunda yake ya kwanza kwa timu ya vijana ya chini ya umri wa miaka 17 kufaulu kushiriki katika michuano ya kombe la dunia la vijana wa chini ya umri wa miaka 17 yatakayoanza nchini Mexico baadae mwezi huu.
Mchukie mpende, Fifa chini ya Sepp Blatter imetoa mchango mkubwa kwa bara la Afrika ambao umepindukia mipaka ya kandanda.

SYRIA KUMECHAFUKA BAADA YA MTOTO KUUWAWA KWENYE MAANDAMANO.

Mtoto wa Miaka 13 Akatwa Uume na Polisi, Avunjwa Shingo, Miguu


Maiti ya Hamza
Mtoto wa kiume wa miaka 13, alikamatwa na kuteswa na polisi, alipigwa risasi sehemu mbalimbali za mwili wake, alikatwa uume wake, alivunjwa shingo na miguu yake, kosa alilolifanya ni kushiriki maandamano ya kuipinga serikali.
VIDEO utakayoiona chini, inamuonyesha mtoto Hamza Ali al-Khateeb mwenye umri wa miaka 13 wa kijiji cha Jiza, Dar'a nchini Syria ambaye video ya maiti yake imekuwa gumzo duniani baada ya baba yake kuiweka kwenye YouTube kuonyesha ukatili wa polisi wa Syria katika kuzuia maandamano ya watu wanaoipinga serikali ya rais Bashar al-Assad.

Mtoto Hamza alikamatwa na polisi aprili 29 wakati alipojiunga na wakazi wengine wa mji wake katika maandamano ya kuipinga serikali.

Mwili wake ulikabidhiwa baadae kwa wazazi wake ukiwa katika hali ambayo iliwafanya watu wengi wasiamini unyama wa polisi kwa mtoto mwenye umri mdogo kama Hamza.

Hamza alivunjwa shingo yake, miguu yake, alipigwa risasi kifuani na sehemu nyingine za mwili wake, na kama haitoshi polisi waliukata uume wake.

Wazazi wake walikabidhiwa mwili wake wauzike huku wakitishiwa wasiseme chochote au la watakiona cha moto.

Baba mzazi kutokana na uchungu wa unyama aliofanyiwa mwanae, aliamua kuchukua video ya maiti ya Hamza akionyesha wazi majeraha na unyama aliofanyiwa mwanae. Aliiweka Video hiyo kwenye YouTube.

Haukupita muda mrefu, baba yake Hamza alitiwa mbaroni na polisi na tangu wakati huo haijajulikana kama yuko hai au la huko alipo.

Jumatano, 1 Juni 2011

MLOKOLE AMUUA MWANAE WAKATI WA MAOMBEZI.


Mama mmoja wa nchini Marekani huenda akahukumiwa miaka 45 jela kwa jaribio lake la kutoa mashetani toka tumboni mwa mtoto wake, jaribio ambalo lilipelekea kifo cha mtoto huyo.



Mama huyo, Latisha Lawson mwenye umri wa miaka 31 alidai kuwa mtoto wake wa kiume wa miaka miwili aliyejulikana kwa jina la Jezaih, alikuwa na shetani tumboni mwake linaloitwa "Marzon".

Ili kulitoa shetani hilo, Latisha aliandaa mchanganyiko wa mafuta ya alizeti na siki. Alimnywesha kinguvu mtoto wake huyo wa miaka miwili na kumfunga mdomo wake kwa nguvu ili kumzuia asitapike wala kuutema mchanganyiko huo.

Mtoto Jezaih alishindwa kupumua na matokeo yake alifariki dunia.

Akisomewa mashtaka ya mauaji mahakamani, Latisha aliiambia mahakama kuwa aliamini kuwa pepo baya lilimuingia mtoto wake wakati alipokuwa mjamzito kwani wakati huo hakuwa akimuabudu Mungu.

Mahakama iliambiwa kuwa Latisha pamoja na mwanamke mwingine waliwanywesha watoto wanne mchanganyiko huo ili kuyatoa mashetani waliyo nayo.

Watoto wengine walitapika mchanganyiko huo lakini Latisha alimzuia mwanae kutapika kwa kuufunga mdomo wake kwa nguvu.

Tukio hilo lilitokea mwezi novemba mwaka 2009. Baada ya kuona mtoto wake amefariki, Latisha alianza kuomba dua akimtaka Mungu amrudishe duniani mwanae kama alivyofanya kwa Lazarus kama maandishi yanavyosema.

Baada ya kuona hakuna kinachotokea, Latisha aliuchukua mwili wa mwanae na kuueweka kwenye mfuko wa rambo na kuuficha kwa zaidi ya mwaka mmoja hadi alipokamatwa mwezi disemba mwaka jana, 2010.

Madaktari wa akili walimfanyia uchunguzi Latisha ambapo ripoti zao zilipelekea mahakama imuone Latisha ana hatia ingawa wakili wake alimtetea kwa kusema kuwa Latisha alikuwa hajui afanyalo wakati huo.

Latisha huenda akahukumiwa miaka 45 jela atakaposomewa hukumu yake mwezi ujao.