UONGOZI wa klabu ya Yanga umesema kwamba, nchi ya Ujerumani na kituo cha kurusha matangazo cha SuperSports, wameonyesha nia ya kuisaidia klabu yao pamoja na soka la Tanzania kwa ujumla.
Kongamano hilo lililofanyika mjini Accra Mei 26 na 27 mwaka huu, pia lilihudhuriwa na Mkuu wa Maendeleo kutoka Shirikisho la Soka Duniani (FIFA), Cyril Loisel, aliyekuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Kombe la Dunia Afrika Kusini, Danny Jordan,wajumbe wa Shirikisho la Soka Afrika (CAF) na Mashirika yasiyo ya kiserikali.
Akizungumza Dar es Salaam jana, Mwenyekiti wa Yanga, Lloyd Nchunga alisema kuwa hayo yamo katika kongamano hilo la kimataifa lililokuwa likijadili soka ya Afrika na kutoa michango mbalimbali ya kuendeleza mchezo huo Afrika.
"Katika mkutano huo niliweza kuzungumza kwa kina na Mkurugenzi anayesimamia Ligi ya Bundesliga, Jog Daubitzer ambaye aliniahidi kuwa atafanya juhudi za kuanzisha mahusiano ya karibu kati ya timu ya Yanga na klabu mbambali za Tanzania zikiwemo na timu za nchi jirani za Afrika Mashariki," alisema Nchunga
Lloyd Nchunga
Alisema Mkurugenzi huyo wa Bundesliga amesema yupo tayari kuisaidia klabu ya Yanga kupitia soka la vijana.Nchunga alisema kituo cha kurusha matangazo cha SuperSports cha Africa Kusini kupitia Mkurugenzi wa Masoko, Gary Rathbone, alisema watafanya jitihada za kurusha matangazo ya mpira pamoja na mambo mbalimbali kwa ajili ya kuinua kiwango cha soka nchini.
Aliongeza kuwa, wadau hao wa soka pia walijadili mikakati ya karne ya 21 katika Masoko, uongozi na utawala kwa ajili ya maendeleo ya soka Afrika
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni