| Friday, June 10, 2011 12:12 PM
HAKIMU, Karani akiwemo na Mhasibu wa Mahakama ya Mwanzo Ukonga jijini Dar es Salaam, wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na makosa ya kushawishi kupokea rushwa ya shilingi laki moja. |
Hakimu huyo alifahamika kwa jina la Ndevera Kihangu, Karani alifahamika kwa jina la Eveline Mowo na mhasibu ni Victoria Mtasiwa.
Washitakiwa hao walifikishwa Mbele ya Hakimu Mkazi, Ritha Tarimo na upande wa Mashitaka uliongozwa na Wakili wa Serikali Salha Abdallah
Abdallah alidai kuwa washitakiwa wote kwa pamoja wanakabiliwa na makosa matatu likiwemo la kushawishi na kuomba rushwa ya kiasi hicho cha fedha.
Alidaiwa Aprili 24 mwaka huu, katika Mahakama ya Mwanzo Ukonga washitakiwa hao walimshawishi Joyce Msaki awapatie kiasi hicho cha fedha ili wampatie dhamana katika kesi inayomkabili iliyopo katika mahakama hiyo.
Abdallah alidai kuwa, kosa la pili ambalo linamkabili mshitakwia wa kwanza pekee ni kupokea rushwa ya shiling 40,000 kama kianzio cha deni hilo
Ilidaiwa Mei 27 mwaka huu washitakiwa hao walipokea kiasi cha fedha cha shilingi 60,000 kutoka kwa Joyce ikiwa ni malizio la deni hilo
Kesi hiyo itarudi tena Juni 22, mwaka huu kwa kutajwa |
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni