Jumatatu, 17 Oktoba 2011

SIMBA YAONGOZA LIGI.

SIMBA imerejea kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu Tanzania bara baada ya kuichapa African Lyon mabao 4-0 katika mechi iliyochezwa kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam.

Ushindi huo umeifanya Simba sasa kukalia kilele ikiwa na pointi 21 ikifuatiwa na JKT Oljoro yenye pointi 19 na Azam ikishika nafasi ya tatu kwa pointi 18.

Yanga iko nafasi ya nne ikiwa na pointi 15.
Wachezaji wa Simba wakishambulia bao la tatu jana.


Wakati Simba ikiibuka na ushindi huo, habari za ndani ya klabu hiyo zinasema kuwa imemtupia virago beki wake Kelvin Yondani.

Chanzo cha habari kutoka ndani ya Simba kinasema kuwa uamuzi wa kumtupia virago Yondani uliamuliwa na Kamati ya Utendaji iliyokutana karibu siku tano mfululizo wiki iliyopita.

“Taarifa rasmi zitatolewa na Mwenyekiti (Aden Rage) kesho (leo) lakini ameondolewa kwenye timu kwa utovu wa nidhamu, hakuonekana kambini tangu tulipocheza na Kagera mwezi uliopita,” alisema mtoa habari wetu.

Katika mechi ya jana, Simba ilipata bao la kwanza katika dakika ya 14 likifungwa na Felix Sunzu kwa mkwaju wa penalti iliyotolewa na mwamuzi Oden Mbaga wa Dar es Salaam baada ya mchezaji wa Lyon Aziz Sibo kuunawa mpira katika eneo la hatari.

Bao hilo la Simba lilidumu hadi mapumziko. Muda wote wa kipindi cha kwanza Simba ililiandama lango la Lyon kwa kasi huku mashuti ya Ulimboka Mwakingwe yakigonga mwamba mara mbili dakika ya 35 na 39 huku Lyon ikijibu mapigo mara nne lakini ilishindwa kufanya
madhara kutokana na safu yake ya ushambuliaji kutokuwa makini.

Emmanuel Okwi iliipatia Simba bao la pili dakika ya pili baada ya kuanza kipindi cha pili, alifunga kwa shuti kali kabla hajafunga bao la tatu katika dakika ya 51.

Dakika ya 57 Shomari Kapombe aliifungia Simba bao la nne akiunganisha mpira wa krosi wa Sunzu.

Katika mechi hiyo, Lyon ililazimika kumaliza mchezo pungufu baada ya mchezaji wake Bakari
Nzige kutolewa kwa kadi nyekundu baada ya kuushika mpira kwa makusudi katika dakika ya 64, awali alikuwa na kadi ya njano.

Kipindi cha pili mechi hiyo ilisimama kwa dakika 15 baada ya kipa wa Lyon Noel Munishi kuzimia baada ya kugombana na Amri Kiemba, hakuweza kuendelea na mchezo na kupelekwa Hospitali ya Temeke kwa matibabu zaidi.

Simba: Juma Kaseja, Nasoro Masoud, Juma Jabu, Juma Nyoso, Obadia Mungusa, Shomari
Kapombe/Gervas Kago, Ulimboka Mwakingwe/Amri Kiemba, Jerry Santo, Felix Sunzu/Mutesa Mafisango, Emmanuel Okwi na Uhuru Selemani.

African Lyon: Noel Munishi, Azizi Sibo, Sunay Juma, Shaaban Aboma, Bakar Nzige, Hassan Mwamba, Agustino Sino, Suleiman Kassim, Iddi Mbaga, Hood Mayanja na Semmy Kessy

Jumapili, 16 Oktoba 2011

ARSENAL YAILAZA SUNDERLAND 2-1

Robin van Persie
Robin van Persie

Mabao mawili mazuri aliyofunga Robin van Persie yameiwezesha Arsenal kupata ushindi dhidi ya Sunderland katika uwanja wa Emirates.
Nahodha huyo wa Arsenal alifunga bao la kwanza katika sekunde ya 29 tangu mchezo ulipoanza, bao linaloonekana ni la mapema sana kufungwa katika Ligi Kuu ya England msimu huu.
Lakini ilionekana kama Sunderland ingepata pointi katika mchezo huo baada ya mchezaji wa zamani wa Arsenal Sebastian Larsson kusawazisha kwa mkwaju wa adhabu ya moja kwa moja katika dakika ya 30.
Lakini Van Persie ndiye aliyekuwa na kauli ya mwisho ya matokeo ya mchezo huo baada ya kufumua shuti la adhabu ya moja kwa moja katika dakika ya 82 na kuipatia Arsenal ushindi na pointi tatu muhimu ilizokuwa ikihitaji.
Arsenal imefikisha pointi 10 na kujisogeza nafasi ya 10.
Nayo West Bromwich Albion katika mchezo ulioanza mapema imefanikiwa kuzoa pointi tatu baada ya kuilaza Wolves mabao 2-0 na kufanikiwa kupata ushindi wa kwanza wa nyumbani na kujikwamu eneo la kushuka daraja.
Chris Brunt alikuwa wa kwanza kuipatia West Brom bao la kuongoza baada ya kazi nzuri iliyofanywa na Billy Jones.
Kevin Doyle naye alikaribia kuipatia bao Wolves na Roger Johnson akapoteza nafasi nzuri ya kufunga baada ya kupiga mpira kichwa uliotoka nje.
Lakini mchezaji wa akiba Peter Odemwingie aliipatia West Brom ushindi dakika za mwisho na kuifanya Wolves ipoteze mchezo wa tano mfululizo wa ligi.
Kwa matokeo West Brom imefikisha pointi nane na wapo nafasi ya 12

SAFU-POLISI WANAPOTIA FORA KWA RUSHWA INASIKITISHA SANA.

SIKU zote tumelalamikia polisi kuwa wanaongoza kwa rushwa.

Ni sekta ambayo inaendekeza ‘mshiko’ na wakati mwingine hadi askari hao wanalitia aibu Jeshi letu zuri la Polisi.

Polisi wanadai rushwa bila ya aibu, angalia walivyomfilisi huyu mfugaji wa Iyumbu huko Singida hadi akauza ng’ombe wake 31 ili awatulize watumishi hao wa vyombo vya Dola kwa kumbambikia kesi.
Shedrack Sagati


Mzee Shigela kabambikiwa kesi na hiyo inatokana na utajiri wake lukuki wa ng’ombe alionao. Watumishi hao wa vyombo vya Dola wakaona watakula wapi zaidi kwa huyo mzee tajiri wa ng’ombe.

Wakaamua kumwingia na kumbambikia kesi kibao, mara kapatikana na fuvu na mifupa ya binadamu, mara kapatikana na ngozi ya simba na chui.

Kwa mtu wa kijijini masikini ambaye hajui sheria katika hali hiyo unadhani atafanya nini? Kisa hiki cha Singida kinasikitisha sana!

Kwamba kinawahusisha polisi wawili na raia watatu waliofanya unyama wa namna hii kuamua kumfilisi mfugaji huyo wa kijijini.

Angalia yumo Mtendaji wa Kijiji, Mtendaji wa Kitongaoji na mkazi wa kijii hicho ambaye nadhani yeye kuingizwa kwenye kesi hiyo inawezekana katika eneo hilo ndiye mjuaji kuliko raia wengine.

Kashfa hii kwa polisi sio ngeni, raia wamekuwa wanalalamika kuwa polisi wanawabambikia watu kesi na hata wakilalamika kwa wakubwa wao hakuna hatua zinazochukuliwa na vigogo wa Jeshi hilo.

Mara ngapi raia wamelalamikia namna trafiki wanavyopiga mabao daladala na mabasi yanayoenda mikoani na nchi jirani.

Kuna hatua yoyote imechukuliwa? Zaidi ya trafiki kuhamishwa kutoka sehemu moja kwenda nyingine?

Tena ukiandika zaidi mambo ya polisi, wanakuwekea bifu kuanzia juu hadi chini na wanatafuta namna ya kukubana kama ilivyofanyika kwa paparazi mmoja baada ya kuanika uozo huo wa polisi wa Usalama Barabarani.

UKATILI KWA ALBINO WAANZA UPYA HUKO GEITA

VITENDO vya mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi (albino) vimeibuka tena wilayani Geita mkoani Mwanza, baada ya mlemavu mmoja wa ngozi kunyofolewa vidole vitatu vya mkono wa kulia pamoja na kukatwa mkono wa kushoto.
Mtoto mwenye ulemavu wa ngozi, Albino.

Tukio hilo lilitokea usiku wa kuamkia juzi katika Kijiji cha Nyaruguguna, Kata na Tarafa ya Nyang’hwale ambapo mlemavu huyo, Adam Robert (14), mwanafunzi wa darasa la nne, alivamiwa na kukatwa mkono wa kulia na kisha kunyofolewa vidole vitatu vya mkono wa kushoto.

Akisimulia mkasa huo, mlemavu huyo ambaye amelazwa katika Hospitali ya Wilaya ya Geita akiuguza majeraha yake, alisema alikumbwa na mkasa huo saa 1:40 usiku akiwa nyumbani
kwao ambapo alivamiwa na mtu mmoja waliyekuwa wanakula naye chakula nje ya nyumba.

Akizungumza kwa shida katika kitanda namba 5 alikolazwa, alisema siku ya tukio saa 12 alifika nyumbani kwao mtu huyo akidai amekwenda kuangalia ng’ombe wake waliokuwa wamepotea ambapo walianza maongezi na yeye juu ya upotevu wa ng’ombe hao.

‘‘Wakati tuko nje na baba, mtu huyo alifika na kubisha hodi kisha tukamkaribisha tukampa kiti akakaa ndipo akaanza kutueleza kuwa anawatafuta ng’ombe wake waliopotea machungani.

Tukaendelea kuzungumza naye hadi tulipoletewa chakula hapo nje tukaanza kula,’’ alisema
na kuongeza: ‘‘Ghafla mvua ikaanza kunyesha ikabidi tuhamie ndani, baba akawa amechukua ugali akatangulia ndani mimi nikabeba mboga yule mtu akabeba kiti chake, wakati tunaingia ndani nilikuwa katikati ya baba na mtu huyo, lakini katika hali isiyokuwa ya kawaida kabla sijaingia ndani yule mtu akanishika na kunivuta nje”.

Alisema baada ya kuvutwa mtu huyo alianza kumkata mkono wake wa kushoto upande wa begani wakati huo akiwa amelala chini akijitupatupa na baada ya kuona ameshindwa kuukata na kuunyofoa mkono kuanzia kwenye kiganja, akaacha na kuanza kuukatia tena kwenye kiwiko.

“Aliposhindwa pia kuukatia kwenye kiwiko aliamua kuugeukia mkono wangu wa kulia na kukata vidole vyangu vitatu vya mkono huo na kuvinyofoa kabisa, wakati huo baba alishindwa
afanye nini akabaki kukimbilia huku na kule na wakati huo kaka yangu alikuwa amejificha kwenye nyumba nyingine na kilichonishangaza sana ni kwamba pamoja na kupiga sana kelele za kuomba msaada hakuna mtu hata mmoja aliyejitokeza kwa ajili ya kuja kunisaidia,” aliongeza kusema.

Akizungumzia tukio hilo baba mzazi wa mlemavu huyo, Robert Tangawizi (36) alisema wakati tukio hilo linatendeka alikuwa kama vile amechanganyikiwa na kushindwa kabisa kumuokoa mwanawe muda wote wa purukushani kati yake na mhalifu huyo na kwamba alishikwa na bumbuwazi na hasa baada ya kumuona mtu ambaye walikuwa wanakula naye chakula kwenye meza moja amegeuka mhalifu kwa mwanawe.

Jumamosi, 15 Oktoba 2011

LIVERPOOL 1 NA MANCHESTER UNITED 1, MECHI IMEISHA ANFIELD, ACHENI PRESHA.

WANAWAKE WAWABAKA WANAUME HUKO ZIMBABWE, WAHITAJI MBEGU ZAO KWA USHIRIKINA.



NewsImages/6004758.jpg
Sophie Nhokwara mmoja wa wanawake watatu waliokamatwa kwa kuwabaka wanaume
Uchawi wa mpya umeibuka nchini Zimbabwe ambapo mbegu za uzazi za wanaume zimekuwa dili kiasi cha kundi la wanawake kuwabaka wanaume na kisha kuiba mbegu zao za kiume.
Wanaume kaeni chonjo sasa maana wanawake siku hizi nao wanabaka wanaume kama inavyotokea nchini Zimbwabwe ambapo wanaume wengi wamekuwa wakibakwa au kulazimishwa kufanya mapenzi na wanawake kinguvu ilimradi tu wanawake waweze kupata mbegu zao za kiume.

Kesi za wanaume kubakwa zimeripotiwa kwenye miji ya Gweru, Harare na Mashonaland.

Wanawake watatu wametiwa mbaroni kwenye mji wa Gweru kutokana na matukio ya kuwabaka wanaume waliyoyafanya hivi karibuni.

Wanawake hao watatu walikamatwa kwenye gari lao ambalo walikuwa wakilitumia kama chambo cha kuwavuta wanaume wakijifanya wanawapa lifti.

Ndani ya gari hilo kulikutwa jumla ya kondomu 33 ambazo zilikuwa na mbegu za kiume za wanaume mbalimbali ambao hadi sasa hawajajulikana.

Wanaume wanapokubali kupewa lifti, hutekwa kwa bunduki na kupelekwa sehemu za mbali ambako hulazimishwa kufanya mapenzi na wanawake hao kwa kutumia kondomu au wakati mwingi bila hata kinga huku wakiwa wameelekezewa bunduki. Baada ya hapo wanawake hukusanya mbegu za kiume na kisha huwatupa wanaume waliowateka pembeni ya barabara.

Wanawake waliotiwa mbaroni wametajwa kuwa ni Rosemary Chakwizira mwenye umri wa miaka 24, Sophie Nhokwara mwenye umri wa miaka 26, na Netsai Nhokwara ambaye naye pia ana umri wa 24, wote ni wakazi wa Gweru. Pia dereva wao mwanaume naye ametiwa mbaroni kwa makosa ya kufanya shambulizi nje ya maadili. Dereva huyo pia anatuhumiwa kesi ya mauaji baada ya kumuua kwa kumgonga kwa gari mtoto na kisha kukimbia.

Inasemekana kuwa wanawake hao wamekuwa wakizikusanya mbegu za kiume za wanaume wanaowateka na wamekuwa wakizitumia mbegu hizo za kiume kwenye mambo ya kishirikina.

Wakazi wa Gweru hawakuamini masikio yao pale majina ya wanake hao yalipotajwa kuwa wanabaka wanaume.

"Wanawake hawa wanajulikana sana hapa kwakuwa wamekuwa wakionekana kwenye kumbi za starehe mara kwa mara", alisema mmoja wa wakazi wa Gweru.

Mkazi mwingine wa Gweru aliyejitambulisha kwa jina la Harry Mohammed Misi aliiambia redio moja nchini Zimbabwe "Tumeshtushwa sana na haya yanayotokea kwenye jamii yetu, wanaume sasa nao wanabakwa na wanawake, inaonekana sasa mambo yamebadilika".

Polisi wa Zimbabwe wamesema kuwa watatumia DNA ili kugundua mbegu kiume za wanaume waliobakwa na wanawake hao

PICHA YA LEO; MWENGE WA UHURU WAWASHWA JANA HUKO BUTIHAMA NA KUANZA MBIO ZAKE.


Makamu wa Rais, Dk. Mohammed Gharib Bilal akimkabidhi Mwenge wa Uhuru kiongozi wa mbio za mwenge mwaka 2011/12, Mtumwa Rashid Halfan kutoka Mkoa wa Kaskazini Unguja. Mbio hizo zilianza jana katika Kijiji Cha Butiama mkoani Mara. (Picha na Amour Nassor OMR).

NDOA YA UZEENI, HAMZA KALALA AMUOA MAMA YAKE KALALA JUNIOR BAADA YA MIAKA 24 YA KUISHI PAMOJA, HONGERENI SANA.

Hamza Kalala na mkewe Stella Momose Cheyo wamefunga ndoa kanisa katoliki Manzese mwanzoni mwa mwezi huu na kufuatiwa na sherehe ya kukata na shoka huko Ukumbi wa Vatcan City Hotel maeneo ya Sinza.
Bi harusi akimlisha keki mumewe.

Mmoja wa watoto wa wanandoa hao ni Kalala Junior ambaye ni mwanamuziki wa kundi la mapacha watatu akiimba na babake Hamza Kalala.

Credits; Glabalpublisherstz.info



NYASI ZA ANFIELD KUWAKA MOTO MUDA MFUPI UJAO KATI YA MAN U NA LIVERPOOL PREMIER LEAGUE.


United: De Gea; Smalling, Ferdinand, Evans, Evra; Park, Jones, Fletcher, Giggs, Young; Welbeck. Subs: Lindegaard, Anderson, Rooney, Hernandez, Carrick, Nani, Valencia.
Liverpool: Reina; Kelly, Carragher, Skrtel, Enrique; Kuyt, Lucas, Gerrard, Adam, Downing; Suarez. Subs: Doni, Agger, Carroll, Henderson, Spearing, Bellam, Robinson

HAJI RAMADHANI ANYAKUA MILIONI AROBAINI ZA MSHINDI BSS JANA USIKU.

Haji Ramadhani mshindi BSS akiwa na Mratibu wa shindano hilo Madam Rita.

Haji akiwa na briefcase yenye zawadi.

Shangwe za kupatikana mshindi.

Credits; Globalpublisherstz.info



Ijumaa, 14 Oktoba 2011

TAKUKURU YABAINISHA UPUNGUFU KATIKA UGAWAJI VOCHA ZA PEMBEJEO.


TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) mkoani Mbeya imetaja upungufu ilioubaini baada ya kufuatilia shughuli nzima ya ugawaji wa pembejeo za ruzuku kwa msimu wa kilimo uliopita.

Mkuu wa Takukuru mkoani hapa, Daniel Mtuka alisema hayo katika kikao chake na waandishi wa habari na kutaja upungufu uliobainika kuwa ni pamoja na baadhi ya wataalamu wakiwemo maofisa kilimo wilaya kulipwa kupitia dhana ya kujitolea.

Mtuka alisema kutokana na hali hiyo, ilikuwa rahisi mno kwa wataalamu na wajumbe wa Kamati kurubuniwa kwa kuwa wakati wakifanya shughuli hiyo, wanakuwa wakikabiliwa na changamoto nyingine ikiwemo za kushughulikia mahitaji ya familia zao.

“Utakuta mtu anajitolea kufanya shughuli hiyo inayogharimu fedha nyingi lakini nyumbani kwake wakati huo huo ana matatizo na pengine ya magonjwa na inakuwa rahisi kurubuniwa,” alisema.
Credits; Mwananchi Gazeti 

APOTEZA KUMBUKUMBU BAADA YA KUFANYA MALAVIDAVI YA NGUVU.



NewsImages/6002830.jpg
Friday, October 14, 2011 2:18 AMMwanamke mwenye umri wa miaka 54 wa nchini Marekani aliwahishwa hospitali baada ya kupoteza kumbukumbu ya muda mfupi wa maisha yake baada ya kumaliza tendo la ndoa na mumewe.
Mwanamke huyo ambaye jina lake halikutajwa aliwasili kwenye hospitali ya jijini Washington nchini Marekani akiwa amekumbwa na mshtuko mkubwa kwa kupoteza kumbukumbu ya mambo yote yaliyotokea katika maisha yake kwa masaa 24 yaliyopita.

Hali hiyo ilimtokea mwanamke huyo baada ya kupewa malavi davi ya nguvu na mumewe kiasi cha kupelekea apoteze kumbukumbu.

Madaktari waliohojiwa kutokana na hali ya mwanamke huyo walisema kuwa mwanamke huyo alisumbuliwa na ugonjwa unaojulikana kitaalamu kama "transient global amnesia" ambayo huufanya ubongo upoteze kumbukumbu kwa muda mfupi.

Ugonjwa huo hausababishi madhara kwa ubongo lakini huweza kumsababishia mtu kuwa mwenye stress sana.

Hali iliyomtokea mwanamke huyo iliripotiwa kwenye jarida la Journal of Emergency Medicine, ambapo ilielezwa kuwa hali kama hiyo humtokea mtu mmoja katika kila watu 100,000 kila mwaka.

Hali hii imeelezwa kuwa mara nyingi hutokea pale mtu anapoufanyisha mwili wake mazoezi mengi kuliko kawaida au kufanya kitu kinachouchosha sana mwili

LEO NI KUMBUKIZI YA MIAKA 12 TANGU BABA WA TAIFA HILI ALIPOTUTOKA OKTOBA 14 1999, TUMWOMBEE APUMZIKE KWA AMANI.

Mwl. Nyerere akiwa na mgeni wake IDD amin DADA kabla hawajafarakana.
Mwenge wa Uhuru.
Akicheza bao na wazee wenzie akiwamo rais Mwinyi na mkewe mama Maria.
Jeneza la mwalimu.





Alhamisi, 13 Oktoba 2011

NYUMBA YA JAMBAZI SUGU YACHOMWA MOTO.

NewsImages/6001866.jpg
Nyumba ikitekea kwa moto.

Ile nyumba ya jambazi maarufu katika mkoa wa Iringa yateketezwa kwa moto na wanachi wa eneo hilo la kigamboni. Jambazi hilo kwa jina Msafiri Ilomo alikuwa akitumia nyumba hiyo kama ghala la kuhifadhia vitu vya wizi.
Ile nyumba ya jambazi maarufu katika mkoa wa Iringa yateketezwa kwa moto na wanachi wa eneo hilo la kigamboni.

Jambazi hilo kwa jina Msafiri Ilomo alikuwa akitumia nyumba hiyo kama ghala la kuhifadhia vitu aina mbalimbali ambavyo alikuwa akivinyang'anya kwa njia nguvu na vitisho ukiwa mbishi hutumia nondo kwa kumchapa binadamu mwenzie mbavuni au kichwani.

Baada ya nyumba hiyo kuteketezwa na moto jopo la wananchi walionekana wakibeba vitu vya aina malimbali kwa njia isiyo halali katika eneo hilo na kutokomea kusikojulikana.

Mheshimiwa Amani Mwamwindi ambaye ndiye meya wa Manispaa ya Iringa alifika katika eneo hilo na kushuhudia vitu vya aina mbalimbali vlivyoporwa kutoka kwa wananchi.

Mstahiki meya alisema kabla ya kukubaliana na wananchi juu ya uvunjaji wa chumba hiyo alilitaka jeshi la Polisi kuchukua mali zote kutoka kwenye nyumba hiyo,ambapo polisi wa usalama walikuwepo hapo kwa muda huo.

Tayari watu zaidi ya wawili wamepoteza maisha kwa kupigwa na jambazi hilo kwa kutumia nondo, katika hali ya kusikitisha zaidi jambazi hilo lilikuwa likiwabaka Wanawake mbalimbali.

Mheshimiwa Mwamwindi alisema kuwa amepokea kwa masikitiko makubwa juu ya tukio hilo la ujambazi katika kata hiyo ya Mwangata ambao wananchi wengi walikuwa wakiishi kwa hofu kubwa kwa kipindi kirefu zaidi.

Meya aliendelea kusema kijana Damas Kisinga amepoteza maisha kwa kupingwa na Nondo na kundi hilo la kijambazi ,kijana huyo Damas alizikwa juzi katika eneo la Makanyagio.

Majambazi hayo yalishindwa kabisa mbinu zao baada ya kuzungukwa na wananchi wakati walipovamia nyumba ya diwani wa Kata ya Mkwawa Thobias Kikula.

Mpaka sasa majeruhi waliopigwa na nondo na kukatwa na mapanga ni Michael Chengula 37 aliyevujwa mkono kabla ya kuchukuliwa simu na fedha taslimu laki moja na Mpiga picha Adilian Lusasi 45 aliyeporwa kamera yake pamoja na picha za wateja wake.

Diwani Lugenge alisema jambazi huyo alikuwa amefunga dishi la DSTV kitu ambacho wananchi wameona si cha kawaida katika nyumba hiyo ya udongo na kuitilia mashaka na kuivamia.

Bwana Lugenge aliendelea kusema takribani mwezi mmoja sasa tangu jambazi hilo lifiwe na mtoto wake ambaye aliweza kumzika kwa siri na msiba aliupeleka wa wazazi wake kwa kuhofia wananchi kujua siri kubwa ndani ya nyumba yake.

Mpaka sasa vitu vilivyokwisha kamatwa ni Nguo,Visu,DVD,TV,Sofa,Magodoro,Baiskeli,Mabati na simu aina mbalimbali, Vitanda, Vyombo vya makanisani na misikitini na mali nyingine nyingi ambazo zilijaa ndani ya chumba hiyo.

Kwa sasa vitu hivyo vipo mikononi mwa jeshi la polisi Iringa.

Jumatano, 12 Oktoba 2011

WALIOMUUA IMRAN KOMBE WAACHWA HURU.

 
 WALIHUKUMIWA KUNYONGWA NA MAHAKAMA KUU, RUFAA
Daniel Mjema, Moshi
ASKARI Polisi wawili waliokuwa wamehukumiwa adhabu ya kifo mwaka 1998 baada ya kupatikana na hatia ya kumuua kwa makusudi Mkurugenzi wa zamani wa Usalama wa Taifa, Luteni Jenerali Imran Kombe wameachiwa huru.Koplo Juma Mswa na Konstebo Mataba Matiku, ambao wamekuwa gerezani takriban kwa miaka 16, wamechiwa huru kwa huruma ya Rais Jakaya Kikwete ambaye alipunguza adhabu hiyo ya kifo, kuwa kifungo cha miaka miwili jela.

Kombe aliuawa kwa kupigwa risasi nne kifuani Juni 30, 1996 baada ya polisi waliokuwa wakisaka gari aina ya Nissan Patrol mali ya W. Ladwa, kumfananisha na mtuhumiwa sugu wa wizi wa magari.

Akizungumza na Mwananchi jana, Matiku alisema walitoka gerezani Mei mwaka huu walikokuwa wakisubiri kutekelezwa kwa adhabu yao ya kunyongwa, kabla ya Rais Kikwete kuwaonea huruma na kuwapunguzia adhabu.

“Unajua baada ya jaji kutuhukumu kunyongwa tulikata rufaa, Mahakama ya Rufani ambayo iliona ile hukumu ilikuwa ni sahihi ikasema tuendelee nayo hadi tulipoomba huruma ya Mheshimiwa Rais,” alisema Matiku na kuongeza:

“Jopo lililomshauri Rais lilipendekeza tupunguziwe adhabu kutoka kunyongwa hadi kifungo cha miaka miwili na kwa kuwa tulikuwa mahabusu tangu 1998, kifungo hicho kilitosha.”

Alipoulizwa wanachofanya sasa yeye na mwenzake Mswa, Matiku alisema anajishughulisha na shughuli za kilimo wakati mwenzake anajishughulisha na biashara.

Maisha gerezani
Konstebo Matiku aliliambia alisema katika miaka yote 16 aliyokuwa gerezani (1996 – 2011), aliishi katika magereza matatu tofauti, Karanga, Kilimanjaro; Maweni, Tanga na Ukonga, Dar es Salaam.

“Kwanza tulikaa Karanga kwa miaka miwili hadi tulipohukumiwa na Mahakama Kuu mwaka 1998, tukahamishiwa Gereza la Maweni kwenda kusubiri kunyongwa, lakini mwaka 1999 mimi nilianza kuumwa hivyo nikahamishiwa Ukonga ili niweze kupata matibabu,” alisema Matiku.Alisema kuanzia wakati huo alitengana na mwenzake, Mswa hadi walipoachiwa kwa huruma ya Rais Mei mwaka huu.

Alisema katika kesi hiyo walikuwa washtakiwa sita wakiwamo askari polisi watano na raia mmoja. Alidai kwamba raia huyo aliyekuwa akiitwa Ismail Katembo alifariki dunia akiwa gerezani mwaka 1997, huku askari wengine wakiachiwa huru na Mahakama Kuu baada ya kutopatikana na hatia.

Matiku alisema katika kesi hiyo walikuwa wakitetewa na mawakili watatu tofauti na kwamba wakili wake anamkumbuka kwa jina moja tu la Sande... “Alikuwa akiitwa Sande, lakini kwa bahati mbaya mimi sina mawasiliano naye hadi sasa, wale wengine walioachiwa walikuwa wakitetewa na Profesa Msenga na huyu Mswa alikuwa akitetewa na wakili mmoja hivi ni profesa naye lakini jina lake limenitoka.”

Matakwa ya Katiba
Madaraka ya Rais ya kumsamehe mtu yeyote aliyepatikana na hatia, yamo katika Ibara ya 15 (1) (c) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 kama ilivyofanyiwa marejeo mwaka 2005.

Ibara hiyo inatamka “Bila kuathiri masharti mengineyo yaliyomo katika Ibara hii, Rais anaweza kutenda lolote ikiwamo kuibadilisha adhabu yeyote aliyopewa mtu yeyote kwa kosa lolote ili iwe adhabu tahafifu.”

Kisheria, huruma hiyo ya Rais inatambulika kama 'Presidential Amnesty' wakati madaraka hayo ya Rais yakifahamika kama 'Prerogative Mercy' na hata Rais mstaafu Benjamin Mkapa aliwahi kuitumia wakati wa utawala wake.

Madai ya familia
Baada ya polisi hao kupatikana na kuhukumiwa adhabu ya kifo kwa kile Jaji Buxton Chipeta alichosema: “Uzembe wa hali ya juu”, mjane wa Kombe, Roselyne Kombe alifungua kesi ya madai dhidi ya Serikali.

Mjane huyo na watoto wa marehemu, walifungua kesi Mahakama Kuu wakiidai Serikali fidia ya Sh690 milioni kwa msingi kuwa kifo cha Kombe kiliifanya miradi iliyoanzishwa na marehemu kupoteza mwelekeo na kufa.

Oktoba 4, 2001, Jaji Lawrence Mchome ambaye sasa amestaafu, aliiona Serikali kuwa inawajibika kuilipa familia hiyo fidia kutokana na vitendo vya watumishi wake hao wawili lakini ikaiamuru ilipe fidia ya Sh300 milioni.

Hata hivyo, Serikali haikuridhika na hukumu hiyo na ilikata rufaa Mahakama ya Rufaa ya Tanzania ambayo kimsingi nayo iliafiki Serikali kulipa fidia isipokuwa ilipunguza kiwango cha fidia hadi kufikia Sh200 milioni.

Adhabu ya kifo
Hatua ya Rais kuwapunguzia adhabu polisi hao imekuja katika kipindi ambacho wanaharakati wa haki za binadamu wakipaza sauti kutaka adhabu ya kifo ifutwe na badala yake iwe kifungo cha maisha.

Tangu Rais Kikwete aingie madarakani 2005, hajawahi kusaini hukumu yoyote ya kifo kama ilivyokuwa kwa mtangulizi wake, Benjamin Mkapa na hadi sasa zaidi ya watu 500 wanasubiri kunyongwa.

Kwa mujibu wa hotuba ya aliyekuwa msemaji wa kambi ya upinzani bungeni, Fatma Maghimbi (CUF), mwaka 2008, Mkapa alibadilisha hukumu za watu 100 waliohukumiwa kunyongwa na kupewa adhabu mbadala.

Maghimbi ambaye sasa ni mwanachama wa CCM, alisema Rais wa Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi ndiye pekee aliyesaini utekelezwaji wa hukumu ya kifo kwa watu 21 ambao walinyongwa mwaka 1994.

Adhabu ya kifo ni kati ya zile sheria 40 ambazo Tume ya Marekebisho ya Sheria chini ya, hayati Jaji Francis Nyalali ilipendekeza zifutwe, kwa kuwa haimsaidii aliyeua, aliyeuliwa wala Serikali kuzuia kosa kama hilo kutokea.

POLISI WAFUNGUA MADUKA YENYE MSAMAHA WA KODI KAMA YALE YA JW


Mkuu wa Jeshi la Polisi, Saidi Mwema.


Kilio cha polisi chaanza kusikika

Na Florah Temba, Moshi

SERIKALI imeondoa kodi kwenye baadhi ya bidhaa za ujenzi kwa askari polisi ili kuwawezesha kujenga nyumba kwa gharama nafuu kulingana na vipato vyao.Hatua hiyo imechukuliwa
siku chache baada ya Kambi ya Upinzani Bungeni kulia na serikali kuhusu huduma duni inazotoa kwa askari polisi, hatua iliyotafsiriwa kuwa kambi hiyo ilikuwa inawachochea askari hao kugoma.

Hayo yalibainishwa jana na Kamishna ya Idara ya Kodi za Ndani wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Patrick Kassera wakati akifungua mafunzo ya usimamizi wa udhibiti na uendeshaji wa maduka ya bidhaa zenye msamaha wa kodi kwa Jeshi la Polisi iliyofanyika katika Chuo cha Polisi Moshi(CCP).

Bw. Kassera alisema msamaha huo wa kodi kwa maduka ya jeshi ni mwendelezo wa msamaha ambao ulikuwepo kwa muda mrefu wa vinywaji vya bia na soda ambao ulikuwa kwa lengo la kuwapa askari motisha ya kufanya kazi.

Alisema msamaha wa sasa unalengo la kumnufaisha askari zaidi na kumuongezea uwezo wa kununua bidhaa muhimu zinazohitajika.

“Kwa kuzingatia hali halisi ya kazi za askari, ambapo muda mwingi anakuwa kazini na hivyo hana muda wa kufanya kazi nyingine ya kumuongezea kipato, ili kujiendeleza ikilinganishwa na watumishi wengine wa umma," alisema na kuongeza;

"Serikali imeondoa kodi kwenye baadhi ya bidhaa za ujenzi vinavyouzwa kwenye maduka hayo ya polisi ili askari waweze kujenga nyumba kwa gharama nafuu.”

Kamishna alitumia nafasi hiyo kuwataka askari kuhakikisha wanatumia fursa hiyo vizuri.

Alisema hatarajii kusikia ofisa yeyote amechukua bidhaa na kupeleka nje au kwa ndugu yake, kwani kufanya hivyo ni kukiuka matakwa na kusudio la serikali.

Kwa mujibu wa kamishana huyo misamaha ya kodi imekuwa ikipunguzia serikali mapato yake na kupunguza uwezo wake wa kuwahudumia wananchi.

Msamaha wa kodi uliotolewa safari hii ni kwa askari wote bila kubagua kwa kuangalia cheo, hivyo ni wajibu wa wasimamizi wakuu kuhakikisha kila askari anafaidika na msamaha huo.

Awali, akitoa taarifa ya mafunzo Kamishna wa Utawala na Usimamizi wa Rasilimali wa Jeshi la Polisi, Bw. Clodwin Mtweve alisema, mafunzo hayo ni muhimu ili kuwajengea uwezo maofisa wanadhimu wa mikoa na wenyeviti wa kamati za kantini.

Wakati wa Bunge la Bejeti Waziri Kivuli wa Mambo ya Ndani, Bw. Godbless Lema alitoa lawama mbalimbali wa serikali kwa kushindwa kupatia mishahara ya kukidhi mahitaji yao wala kuwajengea nyumba, hatua inayosababisha wengi wao, hasa wa vyeo vya chini kuishi uraiani au katika nyumba zisizolingana na majukumu yao.

Chanzo; Gazeti la Majira

Jumanne, 11 Oktoba 2011

NHC YATOA NOTISI YA MIEZI MIWILI KWA WADAIWA SUGU



NewsImages/6000902.jpg
Mkurugenzi Mkuu wa NHC Bw. Msechu alipokuwa akizungumza na vyombo vya habari
TSHIRIKA la Nyumba la Taifa (NHC) limeipa notisi ya
miezi miwili Wizara na taasisi za serikali zinazodaiwa na shirika hilo wawe wamemaliza madeni yao kinyume na hapo watafunga ofisi kwa makufuli
Kati ya wizara zinazodaiwa na shirika hilo ni pamoja na JWTZ, Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa linadaiwa billion 2, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Wizara ya Fedha, Wizara ya Afya, Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Jeshi la Polisi, Mawasiliano na Uchukuzi pamoja na Wizara ya Ujenzi.

Bodi ya Usajili wa Waandisi, Wizara ya Kilimo, Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Utamaduni, Katibu Mkuu Wizara ya Kazi Maendeleo ya Vijana.

Nyingine ni Idara ya Habari Maelezo ambapo tayari wameshatolewa vifaa vyao vya kazi nje ya jingo hilo, Bodi ya Filamu na Michezo ya Kuigiza, Tume ya Haki za Binadamu na Haki na Utawala Bora, Msajili wa Mahakama Kuu Tanga, Ofisi ya Rais, Tumre ya Utumishi wa Umma na Mkuu wa Jeshi la Polisi.

Akizungumza na vyombo vya habari jana jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba (NHC), Bw. Nehemiah Mchechu alisema kuwa hatua hiyo imefikiwa baada ya wadaiwa hao kuomba muda wa mwezi mmoja ili kulipa madeni yao.

Alisema tasisi hizo zimeomba shirika hilo muda huo ili kuweza kumaliza muda wao na wasiwatolee vyombo vyao nje kama inavyopanga shirika hilo.

Alisema endapo malimbikizo hayo hayatalipwa kwa kipindi hicho basi wataendelea na utaratibu wao huo wa kuzifunga ofisi hizo na kuwakabishi madadali kupiga mnada mali za wadeni hao ili kupata fedha zao wanazodai.

Alisema hatua hiyo pia imekuja kwa kuwa shirika hilo lina kazi kubwa ya ujenzi wa nyumba hivyo linahitaji fedha hizo ili kuweza kuanza ujenzi huo.

Pia alisema kuwa shirika hilo halina ugomvi na serikali bali wapo katika majukumu yao ya kikazi

JAMBAZI MSAFIRI ILOMO AKAMATWA NA MALI KIBAO HUKO IRINGA.



NewsImages/5998010.jpg
Baadhi ya mali zilizopatikana nyumbani kwa jambazi Msafiri Ilomo. Picha na Francis Godwin, Iringa
Hili sio ghala la kuhifadhia mali za duka lolote lile nchini bali ni nyumba ambayo jambazi sugu wa mkoani Iringa alikuwa akificha mali alizozipora toka kwa wananchi aliowaua kwa kutumia nondo au kuwajeruhi vibaya kwa nondo.
Jambazi Msafiri Ilomo pamoja na kundi la majambazi wenzake sugu wa mkoani Iringa, walikuwa wakiwatesa wananchi kwa kuvamia nyumba zao na kuwajeruhi kwa nondo kama sio kuwaua kabisa.

Katika matukio yao ya ujambazi, Msafiri na wenzake walipora mali na kuzificha kwenye nyumba yao ya udongo kwenye eneo la Kigamboni kata ya Mwangata.

Mali nyingi zilizofichwa na Msafiri kwenye shimo ambapo juu yake alilima bustani ili isijulikane.



Mali nyingi zaidi zilifichwa chini ya ardhi kwenye shimo kubwa lililochimbwa mbele ya nyumba hiyo ambapo kwa juu shimo hilo lilifunikwa na kuwekwa matuta na kuonekana kama vile ni bustani ya mboga mboga.

Msafiri na wenzake walikuwa hawachagui ni nani wamuibie au waibe sehemu gani. Mali zilizokutwa kwenye nyumba yao ziliibwa toka kwa wananchi na hata misikitini na makanisani.
Jambazi Msafiri katika pozi.


Mali zilizokutwa kwenye nyumba hiyo ni pamoja na TV, DVD, nguo, vyombo, magodoro, baiskeli, sofa, masanduku ya nguo, vitanda, mabati, simu za modeli mbalimbali, visu, CD na pia vyombo vya makanisani na misikitini.

Wananchi wa kata ya Kigamboni walikuwa wakiishi kwa hofu ya majambazi hao ambao hadi sasa wameishawaua jumla ya wananchi wawili na kuwajeruhi kwa ncndo watu wengi.

Siku za mwizi zilitimia 40 juzi baada ya majambazi hao kufeli jaribio lao la kumpora mali kijana mmoja wa kata hiyo ambaye alipiga kelele kali baada ya kunusurika kutandikwa na nondo. Kelele zake ziliwavuta wananchi ambao waliwakimbiza majambazi hao ambao walimbilia kwenye nyumba ya Msafiri.

Wananchi walipoingia ndani ya nyumba hiyo walipigwa na butwaa kukuta mali mbali mbali zikiwa zimezagaa kila kona. Hata hivyo majambazi hayo yalifanikiwa kutoroka na kutokomea vichakani.

Mstahiki meya wa Manispaa ya Iringa Amani Mwamwindi alifika kwenye eneo la tukio na kushuhudia wingi wa mali zilizokutwa ndani ya nyumba hiyo na aliamuru nyumba hiyo ivunjwe pindi polisi watakapomaliza taratibu zao kwakuwa nyumba hiyo ilikuwa imejengwa kinyume cha sheria na ilikuwa imeishapigwa X.

Jambazi Msafiri alikamatwa na kwa bahati nzuri alikubali kuwaonyesha polisi sehemu ya siri waliyokuwa wakificha mali hizo ambayo ilikuwa ni shimo lililokuwa chini ya bustani iliyokuwa mbele ya nyumba hiyo.

Mali zilizopatikana chini ya shimo hilo zilizidi kuwashtua wananchi kutokana na wingi wake. Mali zote zilizopatikana kwenye nyumba hiyo zilichukuliwa na kupelekwa kwenye kituo cha polisi kwa utambuzi zaidi.

Taarifa zaidi zilisema kuwa mwezi uliopita Msafiri alifiwa na mtoto wake lakini alifanya msiba huo kuwa wa wasiri ambapo mazishi yalifanyika nyumbani kwa wazazi wake kwa kuhofia watu wangegundua mali zilizopo kwenye nyumba hiyo iwapo msiba ungefanyika hapo.

Taarifa zaidi ziliongeza kuwa jambazi Msafiri alitoka jela kwa msamaha wa rais lakini hadi sasa ameishafanya matukio mengi ya kikatili katika kupora mali za wananchi.

Polisi mkoani Iringa wanaendelea na uchunguzi wa tukio hilo lililowagusa wakazi wengi wa mkoani humo

Jumatatu, 10 Oktoba 2011

DK. MWAKYEMBE AUGUA UGONJWA MBAYA WA NGOZI, APELEKWA INDIA KWENYE MATIBABU, TUNAMWOMBEA KWA MUNGU APONE UPESI MPIGANAJI WETU.

Rais Kikwete alipomjulia hali Dk. Mwakyembe nyumbani kwake Kunduchi-Mtongani, Dar es Salaam hivi karibuni.

Dk. Harrison Mwakyembe akiwa na Mh Victor Mwambalaswa Bungeni Dodoma siku zilizopita
Naibu  Waziri wa Ujenzi, Dk Harrison Mwakyembe leo amepelekwa nchini India kwa matibabu zaidi ya ugonjwa wa ajabu  uliomuanza  kiasi cha miezi mitatu iliyopita kabla ya hali kubadilika siku za karibuni na hatimaye mwili wake kunza  kuvimba na ngozi kuharibika.

Msemaji wa familia ambaye pia ni Mbunge wa Lupa Mh. Victor Mwambalaswa amesema kwamba hali ya  ngozi Dk Mwakyembe ni mbaya, japokuwa ana nguvu zake na fahamu na anaongea bila shida na anatembea mwenyewe


source: http://www.wavuti.com/

TAIFA STARS YAFUNGWA 3-1 NA MOROCCO.

Matokeo haya yamefifisha matumaini ya Stars kuendelea mbele kwa tiketi ya best looser ili kuingia kwenye kinyang'nyiro cha fainali ya kombe la mataifa huru ya Afrika hapo mwaka ujao.
Timu ya Tanzania katika mechi na Morocco Oktoba 9 mwaka jana ambapo tulifungwa pia.
Mpambano mkali(picha zote kutoka maktaba)