Alhamisi, 2 Februari 2012

PICHA YA LEO; SHIDA HULETA MAARIFA,MBINU SALAMA YA KUVUKA BARABARA KWA WANAFUNZI

Waliyosema wahenga kuwa "shida huleta maarifa" "shida huleta akili" hawakukosea kwani, kwani mfano huu wa picha inayoonekana hapa ambapo watoto wanavuka barabara kwa kushikana mikono na na kuvuka kwa pamoja, ni njia nzuri ya kuepukana na shida za waendesha vyombo vya usafiri barabarani ambao baadhi yao si makini katika kuwaruhusu waenda kwa mguu kuvuka barabara. Wengine hawajali kabisa watoto wadogo ambao ndiyo wanajifunza matumizi ya barabara.

Kila leo wanafunzi wanagogwa na kuachwa na vilema huku wengine wakipoteza uhai wao.

Mbinu hii ya kuvuka barabara nadhani ni sahihi zaidi hasa maeneo yasiyo na alama za pundamilia za kuvukia barabara.
Picture
picha via gazeti la Majira

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni