Jumapili, 8 Januari 2012

MTUHUMIWA WA MAUAJI AKAMATWA BAADA YA MIAKA MINNE.

JESHI la Polisi wilayani Nkasi limefanikiwa kumkamata mtuhumiwa wa mauaji, Charles
Mwananjela (38) maarufu kama `Topaz’.

Mtuhumiwa huyo alikuwa akitafutwa kwa takribani miaka minne.

Kamanda Isuto Mantage katikati.

Mtuhumiwa huyo anayedaiwa alikuwa dereva teksi na mkazi wa kitongoji cha Kipundu mjini Namanyere, Nkasi alikuwa anatafutwa na polisi tangu mwaka 2009 kwa tuhuma za mauaji ya
Mboje Masesa (60) mkazi wa Shishiyu, Shinyanga.

Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Rukwa , Isuto Mantage mtuhumiwa huyo alikamatwa juzi saa tisa mchana mjini Namanyere baada ya kuamua kurejea mjini hapo huku akidhani kuwa polisi walishasahau tukio hilo la mauaji.

“Mtuhumiwa huyu ambaye miaka minne iliyopita alikuwa dereva teksi mjini Namanyere anadaiwa kuwa alishiriki mauaji hayo yaliyotendeka Septemba 21, 2009 saa saba usiku katika pori lililopo katikati ya vijiji vya Mkole na Ipanda wilayani Nkasi.

“Yeye (mtuhumiwa ) akiwa pamoja na wenzake watano ambao tayari tumeshawakamata na kuwafikisha mahakamani walimshambulia mzee huyo pamoja na mkewe kwa marungu na kumuua pale pale,“ alisema Mantage.

Inadaiwa kuwa usiku huo wa tukio mtuhumiwa na wenzake hao pia walimshambulia mke wa marehemu ambaye alizirai kwa zaidi ya saa tano ambapo baadaye alizinduka akiwa hospitalini.

Kamanda Mantage alibainisha kuwa uchunguzi wa awali ulibaini kuwa mtuhumiwa na wenzake walikuwa wamekodiwa na Moshi Malambo ambaye alikuwa ni mfanyakazi wa marehemu,
akidaiwa kutaka kumrithi mke wa marehemu pia mali zake ikiwa ni pamoja na ng’ombe

RAIS WA SUDAN ZIARAN LIBYA.

Rais Omar al-Bashir wa Sudan - ambaye anasakwa na Mahakama ya Uhalifu ya Kimataifa kwa mauaji ya watu wengi - yuko nchini Libya kwa ziara ya siku mbili.
Rais Omar al-Bashir wa Sudan
Omar  Bashir wa Sudan.

Shirika la Human Rights Watch limesema, baada ya kuvumilia kwa miongo kadha uongozi wa kikatili wa Kanali Gaddafi, inatia wasiwasi kuwa serikali mpya mjini Tripoli inazungumza na kiongozi mwengine anayetuhumiwa mauaji vitani.
Sudan imesema iliwapatia silaha wapiganaji waliompindua Kanali Gaddafi mwaka jana.
Uhusiano wa Gaddafi na Sudan ulikuwa mbaya kwa sababu Gaddafi akiwasaidia wapiganaji wa Darfur.

Jumatano, 4 Januari 2012

HII KALI!!!!! MCHINA AGUNDUA GARI LINALOWEZA KUTEMBEA KWENYE MAJI,BARABARANI NA KWENYE BARAFU.

Concept: The Volkswagen Aqua car would be capable of travelling on road, sand, water and ice


A Chinese inventor has come up with an incredible new design for a car that will work on tarmac, sand, ice... and even water.
The all-terrain vehicle, which has a top speed of 62mph and works like a hovercraft, can move seamlessly between different surfaces.
Designer Yuhan Zhang, 21, created the spectacular car - called the Volkswagen Aqua - for a competition sponsored by the German car manufacturer.
Concept: The Volkswagen Aqua car would be capable of travelling on road, sand, water and ice
It features a shiny, sleek design with four fans and integrated airbags that inflate to make it hover.
And it's also environmentally-friendly as its two motors are powered by a hydrogen fuel cell - with zero carbon emissions.
One of the motors inflates a 'skirt' around the vehicle to lift it off the ground, while the other drives it forward and controls direction.
Futuristic: Created by Chinese designer Yuhan Zhang, the Aqua would be powered by a hydrogen fuel cell and would emit zero carbon dioxide


Futuristic: Created by Chinese designer Yuhan Zhang, the Aqua would be powered by a hydrogen fuel cell and would emit zero carbon dioxide
Sleek: The car was dreamt up for a Volkswagen competition and features technology found in hovercraft
Mr Zhang said: 'There is no better form of transport than an air cushion vehicle because it travels equally well over land, ice and water.
'I hope Aqua will become an affordable supercar that is available to the general public one day.'


The competition asked designers to come up with a 'Chinese off-road vehicle'. Aqua is based on technology that is currently available.

Jumanne, 3 Januari 2012

WAATHIRIKA WA MAFURIKO KUONDOLEWA KWENYE KAMBI ZA MASHULENI.

Mbunge wa Mafia Mh. Shaha akisaidia kuokoa waathirika wa mafuriko kwa Boti ya kukodi.


Hayo yamekuja ili kutakiwa kuwapisha wanafunzi wanaotarajiwa kufungua shule wiki ijayo nchini kote

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Saidi Meck Sadiki, alimesema Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Mgulani na Mbweni, limetoa nafasi za kuhifadhi waathirika hao baada ya kuondolewa katika kambi za shuleni
Amesema Shirika la Msalaba Mwekundu limeahidi kutoa mahema ya kutosha kwa ajili ya kuhifadhi waathirika hao Mabwe Pande na wanatarajia kuyafunga katika eneo hilo ndani ya wiki hii.

Amesema mahema hayo yatawahusu wenye nyumba waliopoteza nyumba zao na zoezi hilo halitawahusu wapangaji na hao kutakiwa kutafuta maeneo na kuondoka katika kambi hizo

Shule zinatarajiwa kufunguliwa Januari 9 mwaka huu, ambapo zilifungwa katika likizo ndefu iliyoanza mwanzoni mwa mwezi Desemba

NIFAHAMISHE ilitembelea kambi hizo na kupata maoni ya waathirika hao ambao walikuwa wamepanga na kutakiwa kuondoka katika kambi hizo na kusema kuwa, serikali haiwatendei haki kwani wao pia ni waathirika na kuiomba serikali iwafikirie japo wka nkwuapa msaada kidogo

Wamesema kuondoka katika kambi hizo kwa sasa itakuwa ngumu kwani hawana pa kuanzia na kuiomba serikali iwasaidie japo msaaada wa kuwapa kodi za pango japo ya mwaka mmoja ilki waweze kupanga.

Jumamosi, 31 Desemba 2011

HERI YA MWAKA MPYA 2012.

IT IS HEREBY SUBMITTED THAT  2011 HAS BEEN OVERTAKEN BY EVENTS, THEREFORE IT IS WITHDRAWN AND 2012 IS FILED.WITHOUT PREJUDICE TO THE FOREGOING, I DISPUTE ALL CLAIMS THAT 2011 IS THE END OF EVERYTHING. JUST FORGET AND FORGIVE THE PAST, LIFE GOES ON. MAY 2012 COMES WITH REVOLUTION, BE BLESSED. I ALSO SUBMIT THAT THE READER OF THIS MESSAGE WHETHER IS A LEARNED FRIEND OR A LAYMAN, THE AFFIDAVIT OF OUR FRIENDSHIP, PRAYERS AND GOOD WISHES FOR THE NEW YEAR 2012 IS ATTACHED HEREWITH, I CRAVE LEAVE FOR IT TO BE CONSTRUED AS PART OF THESE GREETINGS.

BALOZI SEFUE AMEAPISHWA LEO IKULU KUSHIKA WADHIFA MPYA WA UKATIBU MKUU.

Hapa Balozi akisubiri shughuli za kuapishwa zianze rasmi.

Rais Jakaya M. Kikwete akimwapisha Balozi Ombeni Sefue kuwa Katibu Mkuu leo asubuhi Ikulu Dar es Salaam.

BALOZI OMBENI SEFUE ATEULIWA KUWA KATIBU MKUU KIONGOZI, KUMRITHI LUHANJO.

Balozi Ombeni Sefue, Katibu Mkuu Kiongozi mpya, kabla ya kuteuliwa alikuwa Balozi wa Tanzania nchini Marekani.

NAIBU WAZIRI WA ELIMU AGAWA LAPTOP KWA WANAFUNZI WA CHUO KIKUU HURIA CHA TANZANIA(OUT)

DIRECTORATE OF COMMUNICATIONS AND MARKETING
ANNOUNCEMENT
LAUNCH OF LAPTOP PROJECT FOR STUDENTS AND
STAFF IN HIGHER LEARNING INSTITUTIONS
This is to inform students and staff in Higher Learning Institutions,
who deposited their funds for the purpose of purchasing laptops for
assisting their learning/teaching through the Open University
Students Organization (OUTSO) that the laptops will be distributed on
Friday December 30
The distribution of the laptops will be launched by the Deputy Minister
for Education and Vocational Training, Hon. Phillipo Mulugo, MP.



Naibu Waziri wa Elimu akizindua mradi wa kuwagawia wanafunzi wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania Laptops jana katika Hotel ya Serena Dar es Salaam,kushoto ni Makamu Mkuu wa Chuo hicho Profesa Tolly Mbwete. Kompyuta hizi zimeuzwa kwa bei raisi ya shilingi laki nne na nusu tu toka kampuni ya Royal Mark ya Dar es salaam.

THE OPEN UNIVERSITY OF TANZANIA

Ijumaa, 30 Desemba 2011

MTANGAZAJI MAARUFU WA ITV NA BAADAE BBC AFARIKI DUNIA LEO HII, NI JOHN NGAHYOMA.

Mpiganaji John Ngahyoma afariki dunia
HABARI ILIYOTUFIKIA HIVI PUNDE INAELEZA KUWA,ALIYEKUWA MTANGAZAJI WA ITV/RADIO ONE MIAKA YA NYUMA NA BAADAE KUHAMIA KWENYE SHIRIKA LA UTANGAZAJI LA UINGEREZA (BBC),BW. JOHN NGAYOMA AMEFARIKI DUNIA MAPEMA LEO ASUBUHI.
HAYATI NGAHYOMA AMBAYE AMEFIKWA NA MAUTI LEO AKIWA HOSPITALI AMBAKO ALIKUWA AKIPATIWA MATIBABU YA MARADHI YALIYOKUWA YAKIMSUMBUA KWA MUDA MREFU AMBAPO ALIENDA MPAKA NCHINI INDIA KWA MATIBABU YA MARADHI YAKE HAYO BILA MAFANIKIO.
MSIBA UPO NYUMBANI KWA MAREHEMU MAENEO YA TABATA SEGEREA NA TARATIBU ZOTE BADO ZINAENDELEA KUFANYIKA.

MBUNGE ASEMA RAIS MUGABE NI SHOGA.

Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe.
Mbunge wa chama cha MDC (Movement for Democratic Change) cha nchini Zimbabwe amejikuta akiingia matatani baada ya kudai rais wa Zimbabwe, Robert Mugabe alifanya mapenzi ya jinsia moja.Mbunge huyo ametupwa jela kwa siku saba.

Mbunge huyo wa kike aliyetajwa kwa jina la Lynette Kareny alisema kuwa Robert Mugabe ambaye pia ni rais wa chama tawala cha Zanu-PF alifanya mapenzi na wanasiasa wawili wa kiume.

"Karenyi anatuhumiwa kutoa kauli hiyo ya kumkashifu kiongozi wa nchi wakati wa mkutano wa hadhara wa chama cha MDC uliofanyika disemba 9 kwenye viwanja vya mpira vya Chimanimani,” limeripoti gazeti la The Herald la nchini Zimbabwe

Alhamisi, 29 Desemba 2011

MALKIA WA MIPASHO AL ANISA HADIJA KOPA KUTUMBUIZA NACHINGWEA LINDI MWAKA MPYA TAREHE 02.



Malkia Hadija Kopa.


Kundi zima la TOT Taarab chini ya uongozi wa Al Anisa Khadija Bint Kopa linatarajiwa kutumbuiza mjini Nachingwea siku ya pili baada ya mwaka mpya kuingia yaani tarehe 02/01/2012 ikiwa ni shamrashamra za kuukaribisha mwaka 2012 katika Ukumbi maarufu wa Nachingwea Resort (NR).Wakati wakazi wa Nachingwea wakisubiri kwa hamu kumuona Malkia na kundi lake la TOT, kwa sasa Hadija yupo katika ziara ya nchi kadhaa za Ulaya, lakini kwa mujibu wa waandaaji wa ziara hiyo,wamesema hilo lisiwatishe na wana uhakika kuwa Hadija atakuwepo siku hiyo ili kuwaburudisha.

Jumatano, 28 Desemba 2011

MAHAKAMA YASEMA KAFULILA BADO MBUNGE HALALI

MAHAKAMA Kuu imetoa amri kusitisha kutekelezwa kwa uamuzi wa Halmashauri Kuu ya
Chama cha NCCRMageuzi wa kumfukuza uanachama Mbunge wa Kigoma Kusini, David Kafulila
hadi kesi aliyofungua itakapomalizika.

Uamuzi huo ulitolewa jana katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam na Jaji Alise Chingwile kutokana na maombi ya zuio yaliyowasilishwa na Kafulila kupitia Kampuni ya Uwakili ya Asyla ya Dar es Salaam.
David Kafulila
Wakili wa Kafulila kutoka kampuni hiyo, Daniel Welwel alisema maombi hayo waliyawasilisha Ijumaa iliyopita chini ya hati ya dharura, kupinga kuvuliwa uanachama.

Kwa mujibu wa Wakili huyo, katika maombi hayo, walidai kwamba uamuzi huo wa NCCR-Mageuzi ukitekelezwa dhidi ya Kafulila atakuwa amekosa sifa za ubunge na jimbo litakosa mbunge.

“Tukasema na kesi ya msingi itakuwa haina maana,” alidai Wakili wa mwanasiasa huyo kijana
aliyewahi pia kuwa mwanachama na kiongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).

Katika kesi ya msingi ambayo itatajwa Februari 21, mwakani, Kafulila kupitia kwa mawakili wake, anadai uamuzi wa NCCR Mageuzi haukuwa halali kwa sababu Katiba ya chama hicho haikufuatwa.

Vile vile anadai hakupewa haki ya kusikilizwa licha ya kwamba ni haki yake ya msingi.

Anadai pia kwamba wajumbe walioshiriki kupitisha uamuzi huo, wengine hawakuwa wajumbe halali.

Watu wanaomuunga mkono pamoja na walio karibu na mbunge huyo, akiwemo Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Kabwe Zitto (Chadema), wameelezea kufurahishwa na uamuzi huo wa Mahakama.

“Kafulila kuendelea na ubunge..... Mahakama Kuu imetoa amri muda mfupi uliopita.

Ataendelea kuwa Mbunge mpaka hapo kesi ya msingi itakapokwisha. Mungu yupo pamoja na wanyonge siku zote,” alisema Zitto kupitia mtandao wa kijamii.
.”

Awali, Katibu wa Bunge, Dk. Thomas Kashilillah alikiri kwamba ofisi imekwishapokea barua ya
NCCR Mageuzi ya kumvua ubunge Kafulila na kwamba inafanyiwa kazi, ingawa hakuna muda maalumu wa kutenda kazi hiyo

PAMOJA NA UTUKUTU WAKE MARIO BALOTELLI ACHANGIA KANISANI KWAKE SHILINGI LAKI TANO WAKATI WA MKESHA WA KRISMASI.

Some footballers enjoy the glitz and glamour of Christmas and are seen attending celebrity parties or enjoying a lavish day at home with the family. But one Manchester City player decided to give something back to his fans this Yuletide - including a charitable church donation and a huge round of drinks.
According to reports today, Mario Balotelli was seen at St John's Church in Chorlton, Manchester, on Christmas Eve to attend the midnight Mass service.
Generous: Manchester City striker Mario Balotelli was full of Christmas cheer as he donated to his local church and bought an expensive round of drinks for patrons at his local pub
Generous: Manchester City striker Mario Balotelli was full of Christmas cheer as he donated to his local church and bought an expensive round of drinks for patrons at his local pub
Accompanied by his girlfriend, they stayed for the carols and after the service, Balotelli put £200 in the collection tray.
A source told The Sun: 'Nobody could believe it when he walked in.
'The last thing anyone expected was a big celebrity like him turning up for the service but he was very polite and charming and didn't draw attention to himself.'
Donation: This is St John's church in Chorlton where Mario put £200 in the collection box after the midnight Mass service
Donation: This is St John's church in Chorlton where Mario put £200 in the collection box after the midnight Mass service

The 21-year-old had been feeling in a generous and festive mood all day as earlier he had visited the Tudor pub in the Manchester suburb of Peel Hall.
He chatted to patrons, had his picture taken with some of them - and then put £1,000 behind the bar.
A source told the paper: 'He was very down to earth. Everyone wanted to talk to him and he took it in his stride.
'It's not a smart pub, so it was a big surprise when he walked in.'
Down to earth: Before the church service, Mario dropped in to the Tudor pub and put £1,000 behind the bar
Down to earth: Before the church service, Mario dropped in to the Tudor pub and put £1,000 behind the bar.

WACHEZAJI YANGA NJAA KALI, PESA HAKUNA.

Wachezaji Yanga walia njaa


Timu ya Yanga
Ikiwa inakabiliwa na ushindani mkali katika kampeni yake ya kutetea ubingwa wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara na pia mashindano ya Klabu Bingwa Afrika, programu za mazoezi ya Yanga inashindwa kutekelezeka kikamilifu kutokana na wachezaji wake kutopata mishahara yao ya miezi miwili.
Mishahara hiyo ambayo wachezaji wanadai ni ya mwezi Novemba na Desemba, ambao umeambatana na sikukuu ya Krismasi na mwaka mpya.
Kwa mujibu wa habari ambazo gazeti hili imezipata ni kwamba mbali na wachezaji hao, pia wafanyakazi wengine walioajiriwa na klabu hiyo hawajalipwa kwa muda wa miezi mitatu sasa.
Chanzo hicho kiliongeza kuwa hali hiyo ya ukata imechangia mambo mengi kutofanyika kama ilivyotarajiwa ikiwemo kuvurugika kwa programu ya mazoezi.
"Hali ni mbaya, klabu haina pesa, mambo mengi hayafanyiki kama ilivyokusudiwa, tunajaribu kufanya kila linalowezekana ili kutatua tatizo hili linalotukabili," alisema mmoja wa viongozi wa Yanga ambaye hakutaka jina lake litajwe.
Aliongeza kuwa kukosekana kwa fedha kutoka kwa aliyekuwa mfadhili wao na mapato madogo ya mlangoni yaliyokuwa yakipatikana katika mechi za mzunguko wa kwanza wa ligi ndio sababu nyingine iliyofanya klabu yao ikose fedha za kujiendesha.

Jumanne, 27 Desemba 2011

MSONDO NA SIKINDE WAPAGAWISHA MASHABIKI MKESHA WA XMASS CHINI YA UDHAMINI WA KONYAGI

Mpambano huo ulivuta mashabiki wengi katika viwanja vya TCC Sigara ambapo bendi ya Sikinde, ilionekana kuwapiku wenzao wa Msondo kutokana na Shamrashamra zilizokuwa zikitawala wakati Msondo wakiimba jukwaani, Onyesho hilo limefanyika usiku wa kuamkia jana ikiwa ni pamoja na kusherehekea sikukuu ya Krismas.
Wanamuziki Shaban Dede na TX Moshi William Junior wa Msondo wakiimba jukwaani huku mashabiki wakiwashangilia kwelikweli wakati wa onyesho hilo lililofanyika TCC Chang'ombe usiku wa kuamkia jana.
TX Moshi William Junior akiimba katikati ya mashabiki , huku mashabiiki hao wakimshangilia.
Kutoka kulia ni mwimbaji wa Bendi ya Sikinde Hassan Kunyata, Yusuph Bernald na Shaban Lendi wapiga Saxaphone wakifanya vitu vyao jukwaani.
Mwimbaji wa bendi ya Sikinde Abdallah Hemba akicheza sambamba na wanenguaji wa bendi hiyo wakati bendi hiyo ilipotupa karata yake ya mwisho usiku wa kuamkia leo

RASHID MATUMLA NA MANENO OSWALD HAKUNA MBABE.

MANENO OSWARD VS RASHIDI MATUMLA HAKUNA MBABE KILA MMOJA ATOKA NA POINTI 99

Bondia Rashidi Matumla (kushoto) akiwa chini baada ya kuteleza uku mpinzani wake Maneno Osward akimsubili kwa ajili ya kumpiga wakati wa mpambano wao uliofanyika Dar es salaam jana wakati wa sikukuu ya Xmasi mpaka mwisho wa pambano point ni 99 kwa 99 hivyo kuwa droo.(Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com)
Bondia Rashidi Matumla (kushoto) na Maneno Osward wakioneshana ufundi wa kutupa masumbwi wakati wa mpambano wao uliofanyika Dar es salaam jana wakati wa sikukuu ya Xmasi mpaka mwisho wa pambano pointi ni 99 kwa 99 hivyo kuwa droo

UKATILI WA AJABU, MJOMBA AMUUNGUZA MTOTO KWA MOTO MAKUSUDI.

Mjomba wa mtoto aliyeunguzwa moto.
 
Mtoto aliyeunguzwa moto.
 
 
Na, Gordon Kalulunga, Mbeya

MTOTO Oscar Oliver (17) mkazi wa Ilemi Jijini Mbeya amechomwa kiganja chake cha mkono wa kushoto na kaa la moto kwa kulazimishwa na mjomba wake akituhumiwa kuwa hana tabia njema.

Tukio hilo la kinyama limetokea usiku wa kuamkia siku ya sikukuu ya Kristmas nyumbani kwa Andendekisye Mwakabubu (30) ambaye ndiye anayedaiwa kufanya unyama huo kwa mpwa wake akimtuhumu kuwa alitaka kumwibia.

Mwakabubu anadaiwa kumlazimisha mtoto huyo kushika kaa la moto na baada ya mtoto huyo kuungua kiganja chake alimpeleka katika kituo kidogo cha polisi cha Mwanjelwa na kumfunmgulia kesi ya wizi wa kuibiwa vitu mbalimbali ili kuweza kuficha unyama wake huo.

Baada ya kufungua kesi hiyo, askari polisi walimshikilia kijana huyo na kumpeleka katika kituo kikuu cha polisi mkoani hapa na kumweleza mlalamikaji huyo bandia kuwa alitakiwa kufika kituoni hapo kwa ajili ya mtoto huyo kupelekwa mahakamani.

Mtoto huyo alipofikishwa katika kituo hicho kikuu alikutana na askari waliopo ndani ya kitengo cha kuelimisha jamii kuhusu unyanyasaji wa kijinsi hususani kwa watoto ambao walimsikiliza mtoto huyo na hatimaye jana walimwita mpwa wake kwa ajili ya kutoa maelezo.

Mwakabubu baada ya kufika kituoni hapo na kutoa maelezo na kuulizwa kuwa nani aliyehusika na tukio hilo alishindwa kubainisha huku akisema kuwa hajui aliyemchoma huku akisahau kuwa katika maelezo yake ya awali yeye ndiye alikuwa mlalamikaji jambo ambalo liliwashawishi askari hao kumakamata na kumpeleka rumande.

Mpwa huyo wa mtoto Oscar akiwa mahabausu ya kituo hicho cha polisi, askari hao wanaunda mtandao huo wa kuelimisha jamii juu ya unyanyasaji wa kijinsia mkoani hapa hususani kwa watoto walimchukua mtoto huyo na kumpeleka Hospitalini kwa ajili ya matibabu.

Mwakabubu alihojiwa na askari wa mtandao huo wakiongozwa na askari aliyefahamika kwa jina la Pudensiana Baito huku mwandishi wa habari hizi akiwa anafuatilia tukio hilo na askari huyo alipotakiwa kueleza kwa undani tukio hilo alisema kuwa yeye si msemaji wa jeshi la polisi.

MCHUNGAJI LUSEKELO AGEUKA HAKIMU, ASEMA JAIRO NA LUHANJO HAWANA MAKOSA!!!!!!!

 
Picture
Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la Maombezi (GRC) lililopo Ubungo Dar es Saama, Mchungaji Antony Lusekelo, ameibuka na kusema kuwa sakata la Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Bw. David Jairo, na Katibu Mkuu Kiongozi Bw. Philemon Luhanjo, ni majungu na haina tatizo.

Bw. Jairo anadaiwa kuchangisha fedha za umma kwa ajili ya kugharamikia kupitisha bajeti ya wizara hiyo kinyume cha utaratibu huku Bw. Luhanjo akidaiwa kumjingia kifua.

Mchungaji Lusekelo maarufu kama Mzee wa Upako amesisitiza kuwa wapo viongozi wengi waliofanya kitendo sawa na ya  Jairo lakini hayajulikani hivyo kutaka Watanzania kuacha tabia ya kuchafuana.

Akizungunza na waandishi wa habari Kanisani kwake jana, Mchungaji Lusekelo alisema haiwezekani mtu mmoja kupanga kuchangisha fedha za wizara bila kuwa na mtandao na viongozi wengine na kudai kuwa kilichotokea ni siri kuvuja na si vinginevyo, "Ninachojua ni kwamba wezi wote wako mahakamani, unapoona mtu analalamikiwa kila siku wala hakamatwi ujue ni majungu tu na mambo hayo hafanyi, angefanya angekuwa selo

Ikumbukwe kwamba kuharibiana na kuchafuana kupo, mfano mimi niliwahi kuambiwa kwamba nimeenda nchini Nigeria kutafuta nguvu za giza wakati sijawai hata kuwaza kufanya kitendo cha namna hiyo,"alisema Mchungaji Lusekelo na kuendelea "Lazima tukiri kwamba watu wanachafuana na ndio maana ninasema hata kwa Bw. Jairo ni siri tu ilivuja na hawezi kufanya peke yake," alisisitiza

Jumapili, 25 Desemba 2011

MTAMBO WA GONGO NA SNAKE MAN KUPANDA ULINGONI LEO

 
Mratibu wa pambano la Ngumi za kulipwa, Shabani Adios 'Mwayamwaya' akiwa katikati ya mabondia,Maneno Osward 'Mtambo wa Gongo' kushoto na Rashidi Matumla 'Snake Man', baada ya kupima uzito leo, kwa ajili ya pambano lao, litakalofanyika kwenye Ukumbi wa Helnken Mtoni Kijichi, Dar es Salaam siku ya Xmasi. (Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com)
Mabondia,Maneno Osward 'Mtambo wa Gongo' kushoto na Rashidi Matumla 'Snake Man', wakipima uzito leo, kwa ajili ya pambano lao, litakalofanyika kwenye Ukumbi wa Helnken Mtoni KIjichi, Dar es Salaam siku ya Xmas

MSONDO NA SIKINDE WAKO KWENYE MPAMBANO MKALI USIKU HUU, NANI ATAIBUKA MKALI!!!?

Nani zaidi kati ya Msondo na Sikinde leo?

Na Mwandishi Wetu
Bendi kongwe nchini Msondo Ngoma Music na Mlimani Park Orchestra “Sikinde Ngoma ya Ukae”
zinatapambana leo (Krismasi) mchana hadi usiku wa manane kwenye viwanja vya TCC Club Chang'ombe jijini Dar es Salaam.
Pambano hilo ambalo tayari limevuta hisia za mashabiki wa muziki wa dansi imeandaliwa na Keen Arts na Bob Entertainment chini ya udhamini wa Konyagi.
Onyesho hilo pia ni maalum kwa ajili ya kusherehekea sikukuu ya Krisimasi ambapo wapenzi wa muziki watajumuika kwa pamoja kwenye viwanja hivyo kufurahia kumalizika kwa mwaka.
Bendi hizo ambazo zina mashabiki wengi nchini kuliko bendi nyingine zozote, zimeahidi kutowaangusha mashabiki wao kwa kila moja ikijinasimu kuwa itaibuka na ushindi.
Mara nyingi bendi hizo zikipambana huwa ni patashika nguo kuchanika, kwani mbali na mashabiki kushangilia bendi wanazozipenda vibweka na vituko kemkem vimekuwa vikitawala.
Sikinde ambayo iliweka kambi jijini Dar es Salaam imejinasibu kuibwaga Msondo na kudai kuwa hivi sasa haitishi kama ile ya miaka kadhaa iliyopita.
Itakuwa ni mara ya kwanza bendi hizo kupambana Wilayani Temeke na pia sikukuu ya Krisimasi tangu zianzishwe