Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la Maombezi (GRC) lililopo Ubungo Dar es Saama, Mchungaji Antony Lusekelo, ameibuka na kusema kuwa sakata la Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Bw. David Jairo, na Katibu Mkuu Kiongozi Bw. Philemon Luhanjo, ni majungu na haina tatizo.
Bw. Jairo anadaiwa kuchangisha fedha za umma kwa ajili ya kugharamikia kupitisha bajeti ya wizara hiyo kinyume cha utaratibu huku Bw. Luhanjo akidaiwa kumjingia kifua.
Mchungaji Lusekelo maarufu kama Mzee wa Upako amesisitiza kuwa wapo viongozi wengi waliofanya kitendo sawa na ya Jairo lakini hayajulikani hivyo kutaka Watanzania kuacha tabia ya kuchafuana.
Akizungunza na waandishi wa habari Kanisani kwake jana, Mchungaji Lusekelo alisema haiwezekani mtu mmoja kupanga kuchangisha fedha za wizara bila kuwa na mtandao na viongozi wengine na kudai kuwa kilichotokea ni siri kuvuja na si vinginevyo, "Ninachojua ni kwamba wezi wote wako mahakamani, unapoona mtu analalamikiwa kila siku wala hakamatwi ujue ni majungu tu na mambo hayo hafanyi, angefanya angekuwa selo
Ikumbukwe kwamba kuharibiana na kuchafuana kupo, mfano mimi niliwahi kuambiwa kwamba nimeenda nchini Nigeria kutafuta nguvu za giza wakati sijawai hata kuwaza kufanya kitendo cha namna hiyo,"alisema Mchungaji Lusekelo na kuendelea "Lazima tukiri kwamba watu wanachafuana na ndio maana ninasema hata kwa Bw. Jairo ni siri tu ilivuja na hawezi kufanya peke yake," alisisitiza

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni