Jumanne, 20 Desemba 2011

BAADHI YA WANANCHI WALAUMU KAFULILA KUFUKUZWA UANACHAMA NCCR

Mh. D. Kafulila


Mbunge huyo alionekana anastahili adhabu hiyo baada ya kupitia tuhuma nzito zilizotolewa juu ya Mwenyekiti wa chama hicho, James Mbatia
Wajumbe walipokea na kujadili kina na kura zikapigwa na kuonekana mbunge huyo kutokuwa na imani na mwenyekiti wake na kwenda kinyume na taratibu za chama hicho.

Mbali na kuvuliwa uanachama kwa mbunge huyo pia Hashim Rungwe aliyewahi kuwa mgombea urais katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010 nae amevuliwa uanachama.
Hivyo kwa kuvuliwa uanachama kwa mbunge huyo kwa mujibu wa sheria jimbo hilo litakabiliwa na uchaguzi mdogo kupatikana kwa mbunge

Kufuatia sakata hilo, msajili wa Vyama vya Siasa nchini, John Tendwa amelaani vikali na kukitupia lawama chama hicho kwa kitendo cha kumvua uanachama mbunge huyo na kuita kitendo hicho ni cha kukomoana na kusababisha gharama zisizo za lazima kwa Taifa kugharamia Uchaguzi Mdogo katika jimbo hilo

Kwa upande wa Chama cha Chadema kimemkaribisha mbunge huyo kijana machachari kujiunga na chama hicho baada ya kufukuzwa NCCR-Mageuzi.
"Milango yetu ipo wazi kwa mujibu wa Katiba, Kanuni na taratibu za chama chetu,"kilisema chama hicho

Hata hivyo baadhi ya wananchi nao walilaani kitendo hicho cha kumvua uanachama mbunge huyo ambaye alikubalika jimboni kwake kuokana na harakati zake za kutetea wanaanchi wa jimbo lake na kitendo hicho kimeonekana na sawa na kuwanyanyasa wananchi wa jimbo hilo

Maoni 2 :

  1. Tunampa pole sana, lakini asihamie chama kingine, namshauri: akae tu nyumbani ajishughulishe na mengine ndipo atapata baraka nyingi huenda kijana huyu siku moja akawa Raisi wa Tanzania.



    Mbona kijana waAfrika Kusini Julius Malema amevuliwa madaraka na chama chake kwa miaka 5 ijao lakini ameapa kutokihama chama chake? (Kesho au keshokutwa wale wenye kukufukuza wewe wao wenyewe wanafukuzwa na utaweza kabisa kurejea katika chama chako ukiwa unaheshima zako zote na zaidi pia: kuheshimiwa na vyama vingine kama Mtanzania halisi!)


    Tabia ya kutanga-tanga na vyama wewe Ndugu Yangu ni tabia ya umalaya wa kisiasa na hupati kuheshimika popote pale wala huko ulikotokea wala huko ulikopigia hodi mpya!

    JibuFuta
  2. Kweli kaka Phili umenena, tabia ya kuhamahama ni umalaya hata kama sio ule wa kingono, ukiacha au husipokuwa malaya unaheshimika sana, Kafu tulia home au nenda kasome utulize akili maana unaonekana hata umri una kuruhusu kupanga vizuri maisha yako, Mungu atawaumbua hao wanafiki waliokufukuza hapahapa Duniani, sali sana yatakwisha.

    JibuFuta