Kama mtoto huzaliwa na kisha baadae kukua na kupitia hatua kadhaa za mabadiliko, basi kijiwe chetu kilianza hivyo mwaka mmoja uliopita kama sehemu binafsi ya kujifurahisha kwa mitundiko ya nyumbani na marafiki zetu, lakini baadae kikakua na kujumuisha mambo mengi ya kijamii.
Shukurani kwenu wote mliobahatika kuona kijiwe hiki kwa njia yoyote ile na kufanya wengi zaidi Duniani kote wakifahamu na kuongeza idadi ya kurasa zinazofunguliwa na kufanya jamii yetu ikue kwa kasi, wachache kati yao si vibaya nikiwataja Kamanda Phili wa Manyanya wa kule bondeni kwa Madiba, Pastor Kalu toka Mbeya, Dada Yasinta(Kapulya Mdadisi) akiwa na shemeji yetu huko Ughaibuni, Simon Kitururu Mzee wa Falsafa ndani ya Neno, Israel Saria wa BBC, Emu Three, Rehema Fussi wa Dar, Flora Talent, Michuzi mkubwa.
Huyu dogo anaitwa Omari, naye ni mdau maana huwa anapenda kushika vifaa vyangu vya kazi na kunifanya nimbembeleze aache ili niendelee na kazi, Maoni yenu ni muhimu ili kuboresha Kijiwe chetu, mwisho tumshukuru Mungu kwa kutupa uwezo wa kuendeleza mambo yetu tunayoyapenda mpaka tukafanikiwa hivi.
Kamanda Hansom Omari akiwa katika pozi anatafakari, nimechelewa kuweka maelezo haya sababu ya shida ya umeme huku kwetu mikoa ya Lindi na Mtwara, tusameheane,tupo pamoja msijali,Tchao.
TUKO pamoja, Mambobado. Endelea tu kutupatia hizo habari zenye msisimuo na picha za kiajabu zikiwa lakini ni habari halisi (na yule jamaa mwenye kulala mbele za magurdumu ya gari la Mbunge kwenye matope alipona kweli? najiuliza hadi leo!)
JibuFutaBinafsi napenda sana habari humo. Ubarikiwe kwa mwaka mwingine wa nyongeza na miaka tena zaidi ya mmoja tu!
Hepi betdeyi!