Jumapili, 16 Juni 2013

ALSHABAAB WASHINDWA KUSIMAMIA SHARIAH KAMA WANAVYOJINASIBISHA HASA WANACHAMA WAO WANPOHUSIKA NA HUKUMU HIZO.

Uhalifu wa hivi karibuni wa al-Shabaab unaonyesha upuuzaji wa sharia

Na Adnan Hussein, Mogadishu

Wanamgambo wa al-Shabaab wamefanya mfululizo wa mashambulio ya ukatili na uhalifu dhidi ya raia katika wiki za hivi karibuni -- utekaji, kukata vichwa na kupora Wasomali katika kupuuza kabisa sheria za sharia ambazo kundi hilo linadai kuzitetea.
  • Askari polisi wa Somalia akisimamia sheria za barabani kwa shughuli zinazoshukiwa za magaidi kwenye eneo la ukaguzi huko Mogadishu. [Tobin Jones/AU-UN IST/AFP]
    Askari polisi wa Somalia akisimamia sheria za barabani kwa shughuli zinazoshukiwa za magaidi kwenye eneo la ukaguzi huko Mogadishu. [Tobin Jones/AU-UN IST/AFP]
Tarehe 30 Mei, al-Shabaab waliagiza kuachiwa kwa wapiganaji wake sita, waliotuhumiwa kwa kupora dola 6,000 kutoka katika duka la dawa huko Baardheere na kuhukumiwa kukatwa mikono yao ya kuume.
"Nilikusanyika na kundi kubwa kutoka mjini kushuhudia adhabu ambayo ingetolewa kwa wapiganaji sita wa al-Shabaab, kwani tulitarajia mikono yao ya kuume kukatwa," alisema Yusra Nur Abdirahman, mwenye umri wa miaka 28 na mkaazi wa Baardheere. "Cha ajabu, mwakilishi kutoka katika kundi hili [aliyekuwa anahusika kutoa hukumu] Shekhe Aadan Nuh alitangaza kwa kutumia kipaaza sauti kwamba wajahidina hao sita wangepigwa viboko 39 kama adhabu ya kosa lao."
Alisema Nuh aliagiza dola 4,900 kurudishwa kwa mfamasia huyo, ambaye ni muungaji mkono al-Shabaab .
"Uamuzi huu wa aibu na wa kuchekesha ambao kwa hakika ulinishangaza na niliuchukulia kama uliokusudiwa kudanganya na kupotosha watu na kuhimiza wanachama wa kikundi hiki kupora mali binafsi na mali za familia," Abdirahman aliiambia Sabahi.
Huu ni mfano tu wa hivi karibuni wa jinsi adhabu za al-Shabaab zisivyo na msingi maalumu na za kinafiki, kwa kuwa wapiganaji walikutwa na hatia ya makosa hawapaswi kuumia na adhabu zilizoagizwa, alisema, akiongeza kwamba wapiganaji pia wameanzisha ulipizaji kisasi dhidi ya raia wa Somalia, ikiwa ni pamoja na utekaji nyara au kuwakata vichwa ndugu wa viongozi kutoka Gedo na Hiran.
Abdirahman aliviomba vikosi vya serikali ya Somalia kukomesha vitendo vya kutisha vya al-Shabaabvya kuteka nyara, kuua, kutesa na kupiga.

Kukiuka sheria ya sharia

Huko Hiran, al-Shabaab imekuwa ikitoa amri ambazo hazina uhusiano na sharia hivyo wanachama wake wanaweza kuepukana na ujambazi na uasherati, alisema mkuu wa poilisi wa Hiran kanali Isaaq Ali Abdullahi.
Majaji wa Al-Shabaab hawaelewi kikamilifu falsafa ya sheria ya kiislamu na kanuni za msingi za mfumo wa sheria wa haki na usiopendelea, alisema. Uamuzi wao sio halali kwa sababu unachochewa kisiasa, una kisasi na kuzingatia mfumo wa sheria wa kula njama, alisema.
Abdullahi aliishutumu al-Shabaab kwa kumkata kichwa mzee mwanaume na kijana wa kiume tarehe 22 Mei huko Dudumo Qaris, kilometa 45 kaskazini magharibi mwa Beledweyne. Wapiganaji pia waliiba dazeni za ngamia kutoka vijijini, alisema.
"Muda umefika kuwasaka hao wasaliti kutoka al-Shabaab, ambao wanahusiana na al-Qaeda, na kuwaondoa kutoka katika miji mbalimbali na vijiji katika mkoa ili kukomesha uonevu, ukandamizaji, ubaguzi na kudharau [raia]," Abdullahi aliiambia Sabahi.
"Tumefikia katika hali ambapo tunahitaji kutambua matamanio yetu, kwa sababu hivi karibuni utambuzi wa uhuru utakuwa kwetu, ambao watu wetu wanastahili kwa sababu ya kujitoa kwa kiasi kikubwa," alisema.
Ahmed Abdullahi Osman Inji, aliyekuwa kaimu mkuu wa usalama wa Hiran, alisema waathirika wawili walikuwa mjomba wake mwenye miaka 90, Hussein Aadan Toore, na mtoto wa kiume wa Toore. Wauaji waliwakata vichwa kwa kutumia jambia kali na kuwaacha kuvuja damu hadi kifo.
Muda wowote utakaochukua, al-Shabaab siku moja watapigwa na viongozi wao watatakiwa kwenda mbele ya mahakama ya kijeshi kujibu makosa ya gizani, alisema Inji.
"Ulipuaji wa mabomu na ukataji vichwa hauwezi kuendelea," alisema Inji. "Vikosi vya serikali vinachelewa kutekeleza operesheni zao za kijeshi kuzuia njia [za al-Shabaab] zisizo na heshima zinazosababisha maumivu na ugumu kuhusu watu wa Somalia, ambao walilazimishwa kumeza machungu ya mateso na kunyimwa maisha ya kisasa."

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni