Jumatatu, 29 Agosti 2011

BEI YA MAFUTA YASHUKA TENA.



Akizungumza na waandishi wa habari jana, Mkurugenzi Mkuu wa Ewura, Haruna Masebu alisema hatua hiyo imekuja kutokana na kushuka kwa bei ya bidhaa hiyo katika soko la dunia.


Alisema kuwa bei hiyo ni kutokana na mabadiliko ya bei ya bidhaa za mafuta katika soko la dunia na kushuka kwa thamani ya shilingi ya Tanzania ikilinganishwa na Dola ya Marekani.

Alisema kwa mujibu wa Sheria ya Mafuta ya mwaka 2008, bei ya mafuta zitaendelea kupangwa na soko na kukokotolewa kila baada ya wiki mbili

Hivyo aliwataka wafanyabiashara na wateja wakubaliane na bei hizo zitakazopangwa na Ewura kwa kuwa bidhaa za mafuta zinabadilika mara kwa mara na kuomba kuepukana na migomo isiyo na tija.

Masebu amevitaka vituo vyote vya mafuta kuchapisha bei ya bidhaa hiyo katika mabango yanayoonekana bayana na kuonyesha bei halali iliyotolewa na mamlaka hiyo na wanu uzi kudai stakabadhi halali na tarehe aliyonunulia mafuta

Mkoa wa Dar es Salaam sasa Petrol itakuwa kwa Sh2,070, dizeli ni Sh1,999 na mafuta ya taa Sh1,980.

Bei kikomo Kikanda mikoani inaonyesha kuwa bei ya petroli kwa Mkoa wa Arusha sasa ni Sh 2,154, dizeli ni Sh2,083 na mafuta ya taa Sh2,064. Mkoa wa Dodoma petroli itauzwa kwa Sh2,128, dizeli Sh2,058 na mafuta ya taa Sh2,038.

Mwanza petroli sasa ni Sh2,219, dizeli Sh2,149 na mafuta ya taa Sh2,130. Mkoa wa Mbeya petroli itauzwa kwa Sh2,176 , dizeli Sh2,106 na mafuta ya taa kwa Sh2,087.

Mkoa wa Kigoma petroli itauzwa kwa Sh2,301, dizeli Sh2,230 na mafuta ya taa Sh2,211

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni