Jumanne, 23 Agosti 2011

AOMBA ANYONGWE MAPEMA.



NewsImages/5893898.jpg
Tariq Aziz
Monday, August 22, 2011 4:37 AMAliyekuwa naibu waziri mkuu wa Iraq enzi za utawala wa rais Saddam Hussein, Tariq Aziz ameitaka serikali ya Iraq imnyonge mapema iwezekanavyo kwa kuwa amechoka kusubiri huku akiteseka kwa magonjwa mbali mbali.
Tariq Aziz, alikuwa naibu waziri mkuu wa Iraq enzi za utawala wa Saddam Hussein na alihukumiwa kunyongwa kama bosi wake mwezi oktoba mwaka jana.

Rais wa Iraq, Jalal Talabani alikataa kutia sahihi adhabu ya kunyongwa kwa Tariq Aziz badala yake alitaka hukumu hiyo hiyo iwe kifungo cha maisha.

Baada ya kutupwa jela akisubiri suluhisho la hukumu yake, Tariq Aziz amemtaka waziri mkuu wa Iraq Nouri al-Maliki afanye mipango ya haraka ili anyongwe kwasababu amechoka kusubiri huku akiteseka kwa magonjwa yanayomkabili.

"Afya yake ni mbaya sana, ameniomba nimwambie Maliki awahishe kunyongwa kwake mapema iwezekanavyo", alisema mwanasheria wa Tariq Aziz, Badie Aref.

"Amesema hili ndio ombi lake kwa sasa kwa kuzingatia afya yake anateseka", alisema Aref.

Aref aliongeza kuwa Tariq Aziz amekuwa akihudumiwa vizuri sana jela lakini amekuwa akisumbuliwa na magonjwa ya kisukari, presha, vidonda vya tumbo na kansa.

Tariq alihukumiwa kunyongwa baada ya kupatikana na hatia ya kufanya mauaji na kuvunja haki za binadamu.

Saddam Hussein ambaye naye alipatikana na hatia ya makosa kama hayo alihukumiwa kunyongwa na alinyongwa disemba 30 mwaka 2006 ambayo ilikuwa ni siku ya kwanza ya sikuu ya Idi

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni