Jumamosi, 30 Aprili 2011

HATI ZA MUUNGANO KUMBE ZIPO!!!!!

Mheshimiwa Zuberi Zitto Kabwe amesema uzushi wa watu wanoaminika katika jamii kuwa Hati za Muungano wa Tanganyika na Zanzibar hazionekani na kuwa hazijawahi kuoneshwa kwa watu wegine zaidi ya Nyerere na Karume ni uwongo kwa vile historia inaonesha kuwa baada ya kusainiwa ziliwasilishwa kwenye Bunge la Tanganyika na baadae kwenye Bunge la Tanzania.
Mh. Zuberi Zitto Kabwe.(Mb)
'Wanaosema hazipo hawajafanya utafiti wa kutosha kwa kutembelea Bunge nakuomba kwani mimi binafsi nimewahi kuziona', alisema Mheshimiwa Zitto. Alitoa maneno haya wakati akichangia mada kuhusu nafasi ya Muungano wakati wa mchakato wa marekebisho ya Katiba unaoendelea hapa nchini, mdahalo huo ulirushwa leo mchana na redio Sauti ya Ujerumani idhaa ya Kiswahili ukiongozwa na mtangazaji Osman Miradji. Washiriki wengine walikuwa Hassan Nassoro Moyo toka Zanzibar,Profesa Julius Nyang'oro toka Marekani na Sheikh Malik wa Zanzibar.
Kwa upande wake Nassoro Moyo alisema muungano yapaswa uzungumzwe kwani ni mzuri japo kuna kasoro chache ambazo zinaweza kurekebishwa kuliko kuwa na wazo la kuuvunja muungano ambapo hasara zake ni kubwa zaidi, muungano wetu ni wa asili kabla hata hatujapata uhuru au mapinduzi hayajafanyika.
Kuhusu madai kuwa muungano ni sawa na kaka mkubwa na mdogo ikitanabaishwa kuwa Tanganyika ni kaka mkubwa na Zanzibar kaka mdogo kwa maana wanakandamizwa, Zitto alikataa vikali dhana hiyo ila aliwasifu Wazanzibar kwa uwazi kuzungumzia kero za muungano kuliko wenzao wa bara.

MAULID NDANI YA KARIAKOO


Jamaa walikutwa Kariakoo mtaa wa Mafia wakifanya matembezi ya Maulid ya Mtume Muhammad(SAW) huku wakicheza dufu safi sana. 

HATIMAYE MWANAMFALME WILLIAM APATA JIKO. ATAINGIA JIKONI KWELI HUYU KATE?

Mwana mfalme wa Uingereza, Prince William na Kate Middleton wamefunga ndoa katika kanisa la Westminster Abbey jijini London.
Takriban wageni 1,900 walishuhudia tukio hilo ndani ya kanisa, na mamilioni wakifuatilia majumbani mwao kwa njia ya televisheni.
Maharusi hao walishangiliwa na maelfu ya watu waliojipanga barabarani kuelekea kasri ya Buckingham Palace ambako Malkia amewaandalia karamu wageni 650.
Wana ndoa hao wapya walitumia gari liliovutwa na farasi la muundo wa mwaka 1902 ambalo lilitumiwa na wazazi wake Prince William wakati wa ndoa yao mwaka 1981.
Maharusi hao baadaye walijitokeza kwenye roshani ya kasri ya Buckingham na kuwasalimu maelfu ya watu waliokwenda kuwasherehekea.
Baada ya kulishana viapo vya ndoa Askofu mkuu wa Canterbury, Rowan Williams, aliwanadi rasmi kuwa "mume na mke".
Kuanzia sasa maharusi hawa watajulikana rasmi kama Duke na Duchess wa Cambridge.

 Maharusi wakitabasamu
 Bharusi akiingia kanisani

Kushoto mpambe wa Bwana harusi aitwaye Harry ambaye ni mdogo wa kuzaliwa wa Bwana harusi. 

Biharusi na baba yake mzazi.



Wakivishana pete.

Alhamisi, 28 Aprili 2011

Advantages and Disadvantages of Online Degrees

Advantages and Disadvantages of Online Degrees
Today’s lifestyle is quite busy for everybody and hence for reasons like promotion, career advancement, and for learning purpose all of us are in search of online education. Many students are choosing online education for pursuing their degrees. Almost 60 percent of the students complete their courses successfully and that is because they are aware of the advantages of online degrees. Any university that is accredited, awards online degrees to students on various fields. Online degrees are offered for almost all the subjects like Political Science, Finance, Business Administration, Law, Engineering, Accounting, Economics, Mathematics, Graphic Designing, History and Medicine too.

The only difference from an online degree and the traditional degree is the way of teaching. As an online degree student, you will attend classes, will work on projects, will ask questions and discuss with the professors and will also appear for examinations, but only through a virtual environment. Your classroom will have bulletin boards and text chats and at times you may have virtual workgroup for problem solving. Depending on your online degree program, you will have synchronous and asynchronous sessions.

Enrolment for online degrees can be done by filling the online admission forms. You will have the choice to select the cost effective university and the university with more online degree programs.

The main advantage of earning an online degree is the learning environment. Wherever you are, as long as you are connected to the Internet, your online degree follows with you. If you can properly mange your time then your online degree sessions will fit in your busy schedule. Your degree program can also be completed with your pace of study. Online degree offers you the benefit to attend classes from your home or any convenient location of yours. You can also apply to any university of any country that offers online degree programs. With these online degree programs available nobody can use excuses like unable to pursue education. Most of the online degree courses can be completed within the stipulated period or shorter than this when compared with the similar types of degree programs that are campus-based. Only you can delay your course completion, if you did not do time management properly. Even monetarily you can save a lot by opting online degree like the tuition fee will be lesser than campus-based degree and the credit hours will also be comparatively less. Most of your learning materials will be of downloading format and so you can save lot of time and money by studying online degree courses.

There are disadvantages of online education if you don’t fit as a right candidate for the online degree. You have to properly manage your time with family, work and study. Your planning for the sessions are very important and so studying on your pace will increase the duration of online degree completion. Since the learning materials will be in text and downloadable format, you should be comfortable with reading and if your choice is listening, then you have to reconsider the decision of obtaining online degree. Your discussion forums and chats are very important for communication and knowledge of using it is very essential. As the online education’s key channel of communication is Internet, it will be disadvantage to you if you don’t know its usage. You should understand the advantages of online degrees and the important factors that affect your decision in pursuing online degrees.
You can get exhaustive information on various online degree programs offered by world’s reputed institutions on http://www.counselorinternet.info/ . You can also visit http://www.onlineloanhelp.info/ for tips and sources to obtain student loans.

Jumatano, 27 Aprili 2011

UBABE WA MADEREVA WA MAGARI YA SERIKALI USIKU.

Gari hili aina ya Land Cruiser(Mkonga) namba SM 3992 likiwa barabarani maeneo ya Sinza Kamanyola usiku wa tarehe 19-04-2011 lilisababisha ajali kwa makusudi pale dereva wake alipolikwaruza kwa makusudi Daladala(Hiace) namba zimehifadhiwa, hali iliyosababisha vioo vya pembeni kuvunjika na kujeruhi baadhi ya abiria. Alipoulizwa dereva huyo wa Cruiser kulikoni avunje vioo vya daladala lenye abiria ndani, alijibu yeye hana kosa hivyo hakuwa na namna nyingine ya kutovunja vioo, tumlaumu dereva wetu wa daladala. Hata hivyo ukweli ni kuwa dereva wa daladala aliomba apewe nafasi aingize gari lake lakini dereva wa cuiser alibana kwa makusudi.

 HUU NI UBABE USIO NA TIJA  HASA UKIZINGATIA GARI ILIYOHUSIKA NI YA UMMA NA SIJUI KAMA WANA KIBALI CHA KUTUMIA GARI USIKU, PIA WALIONEKANA WAMELEWA DEREVA NA ABIRIA WAKE. WANANCHI WALIOKUWEPO WALIKASIRISHWA SANA NA KITENDO HICHO, ACHENI UBABE NA MPATE VIBALI VYA KUTUMIA MAGARI HAYO KWA MAMBO YENU BINAFSI.

MAN U YAICHAPA SCHALKE MABAO MAWILI.

Manchester United imepiga hatua kubwa kuelekea katika fainali ya Klabu Bingwa Ulaya, baada ya kuifunga Schalke katika nusu fainali ya kwanza nchini Ujerumani.
Giggs
Giggs amekuwa mchezaji mwenye umri mkubwa zaidi kufunga goli katika michuano hii

United wangeweza kufunga mabao mengi kabla ya mapumziko, kama sio uhodari wa kipa wa Schalke, Manuel Neuer.
Hata hivyo United walipata bao la kwanza katika kipindi cha pili, baada ya Wayne Rooney kupenyeza pasi wa Ryan Giggs. Rooney baadaye alipachika bao la pili baada ya kupata pasi kutoka kwa Javier Hernandez.
United itaikaribisha Schalke kwenye uwanja wa Old Trafford, Jumatano tarehe 4 mwezi Mei, kwa ajili ya mchezo wa pili wa nusu fainali.
Iwapo watadhibiti ushindi wao, United itawakilisha soka ya England katika Fainali ya Klabu Bingwa Ulaya itakayochezwa kwenye uwanja wa Wembley.

JK AKAGUA GWARIDE LA MIAKA 47 YA MUUNGANO WETU.


Jumapili, 24 Aprili 2011

MAFURIKO DAR

Magari haya yalinaswa na tope wakati yakijaribu kupita kwenye bonde la mto Tegeta kukiwa na maji kidogo yanayotiririka,ghafla maji kutoka maeneo ya juu yalianza kujaza mto ingawa Tegeta  hakukuwa na mvua hali iliyosababisha madereva wayaache magari yao kusubiri maji yapungue,baadae usiku wa jana yaliondolewa.



Ngombe pia huvuka mto huo.

FILAMU YA YASINTA YAJA


Wasanii wa filamu toka mtaa Mrefu maeneo ya Kigogo Luhanga wapo katika hatua za mwisho kabla ya kutoa filamu yao iitwayo YASINTA. Hapa msanii atakayecheza kama zimwi akipambwa ili afanane na wanachotaka kuonesha.


Jamaa anapambwa bado.


Majaribio ya 'action.'

Zimwi katokea, jamaa mbioo.....
Kwa wale wenye mapenzi mema na kazi hizi za wasanii hawa wanaochipukia kwa kasi ili uwasaidie japo kwa ushauri au fiscal aid unaweza kuwasiliana nao kwa namba hizi;
0659209315 Katibu wa kundi.
0713085713 Mratibu Usafiri



TAIFA STARS YACHAPWA NA BLACK MAMBAS 2-0

Shabiki namba moja wa Taifa Stars

Stars(picha ya maktaba)

Stars mazoezini.
Timu ya Taifa ya Tanzania jana usiku kuamkia Pasaka imechapwa na timu ya Taifa ya Msumbiji mabao 2-0 katika mchezo wa kirafiki wa ufunguzi wa uwanja mpya mkubwa wa soka huko MSUMBIJI. Emmanuel Sithole aliipatia Mambas bao katika kila kipindi na kuifanya Mambas kutoka kifua mbele. Matokeo hayo ni kama Stars imeendekeza kichapo kwani mwaka 2007 katika mchezo wa ufunguzi wa uwanja mpya wa Taifa wa Tanzania Stars ililala dolo mbele ya Mambas. Hureeeee!!!!!! Kichwa cha mwendawazimu!?

MAULID YA OMARI MBELA YAFANA

Dufu ya nguvu toka Kibaoni Tegeta kwa Maalim Kione.

Dua ya Nadhir na Milango ya MAULID ikisomwa.

Dada zake Omari

Mama yake Omar

Omari akitolewa nje

Misosi.

Ijumaa, 22 Aprili 2011

MAULID YA MTOTO OMARI MBELA, JUMAMOSI TAR 23/04/11,SAA 7 MCHANA, WADAU MNAKARIBISHWA.

 Umri siku kumi duniani
 Umri siku ishirini





       
Bibi na wajukuu wake

Siku 38 duniani, karibu sana,shida na raha ndio maisha.
Wanafamilia ya Mnonjela wa Tegeta Salasala wanawakaribisha wote, ndugu , jamaa na marafiki kwenye shughuli ya Maulid ya kuzaliwa mtoto Omari Mbela anayetarajia kutimiza umri wa siku arobaini hapo kesho jumamosi nyumbani Tegeta mchana saa saba.
LLAA ILLAH ILALLAH, INSHAALLAH MUNGU TUKUZIE KIUMBE CHETU,AMIN. 

Alhamisi, 21 Aprili 2011

Waasi wakataa kuweka silaha chini Libya

 

Wapiganaji wa Waasi nchini Libya
Wapiganaji wa Waasi nchini Libya
Upinzani nchini Libya, umekataa pendekezo la hivi punde kutoka kwa serikali ya Kanali Muammar Gaddafi, la kuwataka kuweka silaha chini.
Msemaji wa baraza la mpito linalodhibiti mji wa Benghazi, amesema kuwa wapiganaji wa upinzani wataendelea na vita dhidi ya vikosi vya Kanali Gaddafi.
Msemaji wa kundi hilo la upinzani, Abdul Hafeel Ghoga, amewaambia waandishi wa habari kuwa Kanali Gaddafi, amependekeza mkataba huo wa kusitisha mapigano, kwa sababu wanajeshi wake wanaendelea kuangamizwa kwenye mashambulio ya anga yanayotekelezwa na wanajeshi wa NATO.
Lakini Bwana Ghoga, amesema upinzani hauwezi kusimamisha mashambulio yake dhidi ya wanajeshi wa serikali.
Akizungumzia pendekezo la kuafikiwa kwa mkataba wa kisiasa ambao utaruhusu kiongozi wa Libya, Kanali Gaddafi na familia yake kusalia nchini humo, Ghoga amesema hilo haliwezekani.
Msemaji huyo wa upinzani amesema, kwa sasa hakuna mzozo wa kijeshi nchini humo.
Amesema kuongezwa kwa mashambulio ya anga yanayofanywa na wanajeshi wa NATO, kumeimarisha hali kwa waasi wanaopinga serikali ya Gadaffi.
Huku hayo yakijri, mtengenezaji filamu mmoja aliyeteuliwa kuwania tuzo la filamu maarufu kama Oscars, ameuawa mjini Misrata.
Tim Hetherington
Tim Hetherington
Tim Hetherington, ambaye ana uraia wa Uingereza na Marekani aliuawa kwenye shambulio kati kati mwa mji huo ambao umeendelea kushuhudia mapigano makali kati ya wanajeshi watiifu kwa Kanali Gaddafi na wale wa waasi.
Hetherington alikuwa mmoja wa wasimamzi wa filamu ya Resrepo iliyotengenezwa kuhusu vita vya Afghanistan.
Filamu hiyo iliteuliwa kuwania tuzo la oscar mwaka huu.
Mwandishi mwingine Chris Hondros, raia wa Marekani ambaye alikuwa miongoni mwa waliojeruhiwa kwenye shambulio hilo, aliaga dunia akipokea matibabu hospitalini.
Ripoti zinasema mwandishi mwingine wa habari pia alijeruhiwa kwenye shambulizi hilo.

Jumatano, 20 Aprili 2011

MGENI AJE MWENYEJI ASUMBUKE


Msafara wa marais wa Afrika Mashariki wakitoka kwenyemkutano Mlimani City wakiongozwa na pikipiki za polisi huku......


Wananchi wakiwa wamekwama katika vituo vya daladala kupisha misafara hiyo,abiria wa Ubungo wakiwa Mwenge stendi.

Abiria wanaoenda Tegeta wakiwa stendi ya Shell Mwenge



Wengine walishindwa kuvuka barabara

Hapa wakiwa wamekata tamaa kabisa,ilikuwa tar. 18-04-11 saa 4.00 hadi 4.30 usiku.