Jumanne, 5 Aprili 2011

KAMUSI YA WAWINDAJI NA MADEREVA PORINI



Neno Rejesta kwa wale watumiaji wazuri wa lugha ya kiswahili lina maana ya matumizi ya lugha au maneno kulingana na muktadha  yaani mahali gani, wakati gani au kundi gani la watu mfano askari au wanafunzi na kadhalika, kwa wale ndugu zetu wawindaji au wasindikizaji wa watalii mbugani hutumia majina kadhaa ya wanyama wanapouliza kwa wenzao wanapokutana ambapo ni vigumu kwa usiye kundi lao kuelewa haraka, mfano SIMBA huitwa SHARUBU, TEMBO huitwa MASIKIO, MAMBA huitwa MKASI, CHUI huitwa WAJUU na TWIGA huitwa MREFU na mengine mengi usiyoyajua.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni