Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo HIFADHI. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo HIFADHI. Onyesha machapisho yote

Jumanne, 5 Aprili 2011

KAMUSI YA WAWINDAJI NA MADEREVA PORINI



Neno Rejesta kwa wale watumiaji wazuri wa lugha ya kiswahili lina maana ya matumizi ya lugha au maneno kulingana na muktadha  yaani mahali gani, wakati gani au kundi gani la watu mfano askari au wanafunzi na kadhalika, kwa wale ndugu zetu wawindaji au wasindikizaji wa watalii mbugani hutumia majina kadhaa ya wanyama wanapouliza kwa wenzao wanapokutana ambapo ni vigumu kwa usiye kundi lao kuelewa haraka, mfano SIMBA huitwa SHARUBU, TEMBO huitwa MASIKIO, MAMBA huitwa MKASI, CHUI huitwa WAJUU na TWIGA huitwa MREFU na mengine mengi usiyoyajua.

Jumatano, 30 Machi 2011

UTALII TANZANIA

 Utalii wa maeneo tofauti katika Tanzania unawezekana ukiacha ule wa kuangalia wanyama, hii ni fukwe iliyopo jijini Dar es salaam inayoitwa Coco beach,  wageni na wenyeji hutembelea maeneo haya bila gharama yoyote.(picha zote kwa hisani ya miguelcostales.blogspot.com)
 Mandhari ya jiji la Dar ukiwa baharini upande wa mashariki.
 Fukwe ya Bagamoyo
 Mji mkongwe Zanzibar
 South beach Kigamboni
View point ukiwa katika hifadhi ya Manyara. (Picha kwa hisani ya tembeatz.blogspot.com)