Leo tar. 7-4-11 ni maadhimisho ya siku ya kumbukumbu ya kifo cha aliyekuwa muasisi na kiongozi wa mapinduzi ya Zanzibar ya mwaka 1964 Ndg Abeid Aman Karume aliyefariki kwa kupigwa risasi na wahaini mwaka 1972 huko makao makuu ya ASP Kisiwandui, Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi, AMIN.
Mheshimiwa Karume akiwa na Marehemu Julius Nyerere wakisheherekea muungano wa Tanganyika na Zanzibar 1964.
Ishara ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar kwa kuchanganya udongo wa nchi zote mbili.Dua ya kumkumbuka marehemu Karume kando ya kaburi lake.
Kushoto ni mjane wa marehemu aitwae Bi. Fatma Karume.
Mtoto mkubwa wa marehemu aitwae Ali Karume
Mtoto mdogo wa marehemu aitwae Amani Karume.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni