Jumamosi, 30 Aprili 2011

HATI ZA MUUNGANO KUMBE ZIPO!!!!!

Mheshimiwa Zuberi Zitto Kabwe amesema uzushi wa watu wanoaminika katika jamii kuwa Hati za Muungano wa Tanganyika na Zanzibar hazionekani na kuwa hazijawahi kuoneshwa kwa watu wegine zaidi ya Nyerere na Karume ni uwongo kwa vile historia inaonesha kuwa baada ya kusainiwa ziliwasilishwa kwenye Bunge la Tanganyika na baadae kwenye Bunge la Tanzania.
Mh. Zuberi Zitto Kabwe.(Mb)
'Wanaosema hazipo hawajafanya utafiti wa kutosha kwa kutembelea Bunge nakuomba kwani mimi binafsi nimewahi kuziona', alisema Mheshimiwa Zitto. Alitoa maneno haya wakati akichangia mada kuhusu nafasi ya Muungano wakati wa mchakato wa marekebisho ya Katiba unaoendelea hapa nchini, mdahalo huo ulirushwa leo mchana na redio Sauti ya Ujerumani idhaa ya Kiswahili ukiongozwa na mtangazaji Osman Miradji. Washiriki wengine walikuwa Hassan Nassoro Moyo toka Zanzibar,Profesa Julius Nyang'oro toka Marekani na Sheikh Malik wa Zanzibar.
Kwa upande wake Nassoro Moyo alisema muungano yapaswa uzungumzwe kwani ni mzuri japo kuna kasoro chache ambazo zinaweza kurekebishwa kuliko kuwa na wazo la kuuvunja muungano ambapo hasara zake ni kubwa zaidi, muungano wetu ni wa asili kabla hata hatujapata uhuru au mapinduzi hayajafanyika.
Kuhusu madai kuwa muungano ni sawa na kaka mkubwa na mdogo ikitanabaishwa kuwa Tanganyika ni kaka mkubwa na Zanzibar kaka mdogo kwa maana wanakandamizwa, Zitto alikataa vikali dhana hiyo ila aliwasifu Wazanzibar kwa uwazi kuzungumzia kero za muungano kuliko wenzao wa bara.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni