Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo MAFURIKO. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo MAFURIKO. Onyesha machapisho yote

Alhamisi, 12 Januari 2012

WAATHIRIKA WA MAFURIKO DAR, BADO WAPO BARABARANI KWA NINI!!!? SERIKALI ICHUKUE HATUA KWANI FEDHA ZA MAAFA ZIPO.

Baadhi ya waathirika wa mafuriko wanaoishi nje ya Shule ya Sekondari Benjamin Mkapa wakiwa na watoto wao kama walivyokutwa kando ya barabara ya Uhuru Dar es Salaam. Kushoto ni Mwanaharusi Abubakari, Zarika Juma, Fatuma Hemedi na Mwajabu Haruna. Kwa mujibu wa Katibu wa Kamati ya Waathirika waliokuwa wapangaji wa maeneo yaliyokumbwa na mafuriko, Eziaka Wema, eneo hilo lina jumla ya waathirika 130 ambao hawana mahali pa kuishi. (Picha na Mohamed Mambo)

Jumapili, 24 Aprili 2011

MAFURIKO DAR

Magari haya yalinaswa na tope wakati yakijaribu kupita kwenye bonde la mto Tegeta kukiwa na maji kidogo yanayotiririka,ghafla maji kutoka maeneo ya juu yalianza kujaza mto ingawa Tegeta  hakukuwa na mvua hali iliyosababisha madereva wayaache magari yao kusubiri maji yapungue,baadae usiku wa jana yaliondolewa.



Ngombe pia huvuka mto huo.

Alhamisi, 14 Aprili 2011

MAFURIKO DAR

Mvua zinazoendelea kunyesha sehemu za miinuko hapa Dar es salaam zinasababisha mito iliyopo jirani na midomo ya bahari kufurika, pichani ni mto Tegeta ukiwa umefurika ingawa katika hali ya kawaida huwa hautiririshi maji.