Jumatano, 7 Machi 2012

WAFANYAKAZI WA TAZARA WAGOMA

Mwl. Julius Nyerere na Rais kaunda wa Zambia wakati wa uzinduzi wa Reli ya TAZARA miaka ya 70.
WAFANYAKAZI wa Shirika la Reli la Tanzania na Zambia (TAZARA ), jana waligoma kuendelea na kazi.


Wamekitishia kusimamisha huduma ya usafiri wa garimoshi kwa kushinikiza kulipwa mshahara wao wa miezi miwili ya Januari na Februari; anaripoti Lucy Lyatuu.


Hata hivyo, Menejimenti ya Tazara imesema, tayari mshahara wa wafanyakazi hao wa Januari ulishalipwa na uliobakia utalipwa katika ya mwezi huu na hali hiyo inatokana na kushuka kwa uzalishaji wa shirika.


Akizungumza na wafanyakazi wa shirika hilo waliokusanyika katika eneo la kuondokea abiria jijini Dar es Saalam, Mwenyekiti wa Tawi la Chama cha Wafanyakazi wa Reli (TRAWU), Yassin Mleke alisema wafanyakazi wamechukua hatua hiyo kutokana na kutosikilizwa

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni