Jumamosi, 31 Machi 2012

PICHA YA LEO; KABURI LA MBWA HUKO NACHINGWEA.

Hili linaloonekana hapa ni kaburi la Mbwa wa Mzungu mmoja aliyejulikana kwa jina la Phills aliyewahi kuishi hapa Tanzania wilayani Nachingwea akifanya shuguli zake za kilimo cha karanga miaka ya 1950. Kaburi hili lipo maeneo ya Boma  Airport Road hapa mjini Nachingwea na limejengewa vizuri kwa zege imara ingawa limeanza kuhujumiwa kwa kuondolea kibao cha shaba kilichokuwa kinaelezea jina la mbwa huyo na uzio mdogo kubomolewa. 
Kwa nini mbwa ajengewe kaburi zuri la kudumu kama binadamu!!?
Mbwa huyu alikuwa maarufu enzi hizo kwani alikuwa msaidizi mkubwa kwa kazi za nyumbani za Mzungu Phills ikiwemo ulinzi wa makazi pia kutumwa sehemu mbalimbali ikiwemo sokoni kununua bidhaa.
Mbwa huyo marehemu alikuwa na akili za kuweza kwenda sokoni akiwa na kikapu na pesa na maelekezo ya maandishi ya bidhaa za kununua na duka au kibanda husika cha sokoni, muuzaji husoma maelekezo na kumpatia mbwa bidhaa kwenye kikapu shingoni hata kama ni nyama na huzifikisha kwa mwenyewe aliyemtuma ambaye ni Mzungu Phills. Baada ya kifo chake mzungu alihudhunika sana na kuamua kujenga kaburi zuri la kumbukumbu ya Mbwa wake ambalo lipo hadi leo maeneo ya Kilimani Boma Nachingwea. 

Maoni 1 :