Ijumaa, 16 Machi 2012

JK ATEUA WAKUU WA MIKOA WAPYA.

WAKUU wa mikoa mipya ambayo hivi karibuni ilitangazwa katika gazeti la serikali wameteuliwa jana na wanatarajiwa kuapishwa wiki ijayo, Machi 21 mwaka huu.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka Ikulu walioteuliwa ni Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Dk. Rajab Rutengwe ambaye sasa atakuwa mkuu wa mkoa wa Katavi na Magalula Saidi Magalula atakayekuwa mkuu wa mkoa wa Geita.

Awali Magalula alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Lindi. Wengine ni Paschal Mabiti atakayekuwa Mkuu wa Mkoa wa SIMIYU na Asery Msangi mkoa wa Njombe.

Kabla ya hapo Mabiti alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Singida na Msangi Mkuu wa Wilaya ya Iringa.

Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais imesema kwamba uteuzi huu umeanza jana Machi 15, 2012

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni