Jumatano, 25 Julai 2012

LEO NI SIKU YA KUWAKUMBUKA MASHUJAA WETU MBALIMBALI WALIOTETEA TAIFA HILI, SHEREHE ZAADHIMISHWA SEHEMU MBALIMBALI TANZANIA.

MAADHIMISHO YA SIKU YA KUMBUKUMBU YA MASHUJAA VIWANJA VYA MNAZI MMOJA JIJINI DAR ES SALAAM LEO

 Rais Dkt. Jakaya Kikwete, akiweka Ngao  na Mkuki kwenye Mnara wa Mashujaa, wakati wa maadhimisho ya siku ya kumbukumbu ya Mashujaa, iliyofanyika kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam, leo.
Mkuu wa Majeshi, Davis Mwamunyange akitoka kuweka silaha ya jadi kwenye Mnara wa Mashujaa, wakati wa maadhimisho ya siku ya kumbukumbu ya Mashujaa, iliyofanyika kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam, leo.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Kikwete, akiwasili kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam leo, kuhudhuria sherehe za maadhimisho ya siku ya kumbukumbu ya Mashujaa, leo.
 Kutoka (kushoto) Rais Dkt. Jakaya Kikwete, Mkuu wa Majeshi, Davis Mwamunyange, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Rais wa Zanzibar, Dkt. Ali Mohamed Shein, Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Idd, Rais Mstaafu wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi,  Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Pandu Ameir Kificho....., Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Shamsi Vuai Nahodha na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Said Meck Sadiq,  wakiwa katika viwanja vya Mnazi  Mmoja wakihudhuria sherehe za maadhimisho ya siku ya kumbukumbu ya Mashujaa, leo.
 Sehemu ya wageni waalikwa na Mabalozi wa nchi mbalimbali waliohudhuria maadhimisho hayo.
 Askari wa Jeshi wakishiriki katika maadhimisho hayo, hapa wakiweka silaha begani.
 Ni ishara ya kutoa heshima kwa Mashujaa wapiganaji.
 Rais Dkt. Jakaya Kikwete, akisalimiana na baadhi ya wazee waliopigana vita mbalimbali vya ukombozi wa nchi ya Tanzania, waliohudhuria katika maadhimisho ya siku ya kumbukumbu ya Mashujaa, iliyofanyika kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam, leo.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na baadhi ya wazee waliopigana vita mbalimbali vya ukombozi wa nchi ya Tanzania, waliohudhuria katika maadhimisho ya siku ya kumbukumbu ya Mashujaa, iliyofanyika kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam, leo.
 Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum, akiomba dua kwa niaba ya waislam wakati wa maadhimisho hayo leo.
 Kiongozi wa dini ya kikristo, Mchungaji Kamoyo, akiomba sala kwa niaba ya wakristo wakati wa maadhimisho hayo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama, wakati akiondoka kwenye uwanja wa Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam leo baada ya kuhudhuria sherehe za maadhimisho ya siku ya kumbukumbu ya Mashujaa.
SHEREHE ZA SIKU YA KUWAKUMBUKA MASHUJAA ZA FANA MKOANI RUVUMA
Jeshi la Wananchi JWTZ wakipita mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said Sabit Mwambungu Kutoa heshima katika Kuadhimisha siku ya Mashujaa kakaka Viwanja vya Maenge Manspaa ya Songea
Gwaride la JWTZ likitoka Nje baada ya Kumaliza shuguli za Siku ya Kuwa kumbuka mashujaa walio kufa wakati wa vita na mashujaa walio nyongwa na wajerumani na kuzikwa katika kaburi moja watu 27 .
Picha ya Askari wa Vita vya Nduli Iddi Amini Dada ikiwa ni ukumbusho kwa asikari walio enda Uganda kuwa komboa waganda pamoja na kuokoa eneo lililo tekwa na Iddi Amini Dada
Askari wa Mawasiliano JWTZ wakiwaburudisha waliofika viwanja vya Mashujaa kuadhimisha siku ya Mashujaa
Mkuu wa mkoa wa Ruvuma akiwa na Bregedia wa kanda ya kusini katika siku ya kuwa kumbuka Mashujaa viwanja vya Mashujaa Mahenge
Meya wa Manispaa ya Songea Charles Mhagama wa pili kutoka kushoto akiwa mmoja wawatu walio hudhuria siku ya Mashujaa
Mkuu wa wilaya ya Songea Joseph Joseph Mkirikiti akiwa katika Viwanja vya Mashujaa Mahenge wakwanza Kulia

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni