KARIBU KATIKA BLOGU HII YA KUELIMISHA, KUBURUDISHA NA KUONYA KUPITIA MADA MBALIMBALI NA HATA PICHA. ONGEZA MAHUSIANO KWA KUJUMUIKA NA WENZIO HAPA.UNAWEZA TUMA PICHA NA MAELEZO KWA ANUANI HII;mkuu74@gmail.com
Alhamisi, 31 Machi 2011
Jumatano, 30 Machi 2011
Hapa Kwetu: SUPER MUHOGO: Unga Safi wa Muhogo
SUPER MUHOGO: Unga Safi wa Muhogo: "Katika pita pita zangu, nimeona tangazo kwenye blogu ya Profesa Mbelle la wajasiriamali wa Chanika, Dar es Salaam, wanaouza unga wa muhogo. Uzuri ni kwamba unga huu wa muhogo mimi nimeutumia na bado nina kilo kama nne katika stock yangu,ni mzuri ukila pia wametusaidia kupata vyakula vyetu vya asili ambavyo ni nadra kuvipata hapa mjini,kiafya unga wa muhogo una virutubisho vyote. Hongera Bw. Joram na kundi lake Mungu awazidishie muendelee kutoa lishe bora kwa watu wote.
UTALII TANZANIA
Utalii wa maeneo tofauti katika Tanzania unawezekana ukiacha ule wa kuangalia wanyama, hii ni fukwe iliyopo jijini Dar es salaam inayoitwa Coco beach, wageni na wenyeji hutembelea maeneo haya bila gharama yoyote.(picha zote kwa hisani ya miguelcostales.blogspot.com)
Mandhari ya jiji la Dar ukiwa baharini upande wa mashariki.
Fukwe ya Bagamoyo
Mji mkongwe Zanzibar
South beach Kigamboni
View point ukiwa katika hifadhi ya Manyara. (Picha kwa hisani ya tembeatz.blogspot.com)
Jumanne, 29 Machi 2011
KABUMBU LA WATANI WA JADI
WADAU WOTE WA MICHEZO MNAKUMBUSHWA KUWA ULE MPAMBANO WA MCHEZO WA KANDANDA KATI YA WATANI WA JADI TIMU YA INVESTIGATORS DHIDI YA ASSISTANTS INVESTIGATORS UPO PALE PALE. MCHUANO MKALI UNATARAJIWA SIKU YA JUMAMOSI TAREHE 2/4/2011 KATIKA VIWANJA VYA SHULE YA MSINGI MUHIMBILI KUANZIA SAA MOJA ASUBUHI. MRATIBU WA MCHEZO HUO BW. VICTOR SWELLA AMEWATAKA WACHEZAJI WA TIMU ZOTE MBILI KUENDELEA NA MAZOEZI ILI KULETA MCHEZO SAFI WENYE USHINDANI SIKU HIYO,TARATIBU ZA USAFIRI MTAJULISHWA.
MICHEZO KWA AFYA.
MICHEZO KWA AFYA.
NANI MFALME WA NYIKA?
Naomba niulize swali nipewe jibu maana kuuliza si ujinga, haya yanayoonekana mbele ya mnyama Tembo ni meno yake au pembe zake?
Hivi kati ya Simba na Tembo yupi ndiye mfalme wa huko mwituni? Please naomba majibu toka kwenu wadau, ni katika kuelimishana tu.
Jumatano, 23 Machi 2011
AJALI YA WANAMUZIKI WA TAARAB
Waombolezi wakiwa nje ya ukumb wa Equator Grill wakisubiri maelkezo ya shughuli ya msiba ya wanamuziki 13 wa five star taarab. Huo ndio ukumbi wao wa nyumbani wanamuziki hao.
Lori lililosheheni mzigo wa mbao ndilo linasemekana limesababisha ajali hiyo. Kamanda wa kikosi cha usalama barabarani mkoani Morogoro amesema chanzo cha ajali hiyo ni mwendokasi aliokuwa nao dereva wa basi dogo aina ya coaster iliyowabeba wanamuziki hao alipojaribu kulipita lori hilo bila ya mafanikio.
Askari Wanyamapori wa Mikumi Mbuga ya Wanyama wakilinda usalama wa eneo la ajali.
Lori lililosheheni mzigo wa mbao ndilo linasemekana limesababisha ajali hiyo. Kamanda wa kikosi cha usalama barabarani mkoani Morogoro amesema chanzo cha ajali hiyo ni mwendokasi aliokuwa nao dereva wa basi dogo aina ya coaster iliyowabeba wanamuziki hao alipojaribu kulipita lori hilo bila ya mafanikio.
Waombolezaji wakiangalia bango lenye picha ya baadhi ya wanamuziki wa kundi hilo.
Walionusurika katika ajali wakiwa ukumbini Equator baada ya kuruhusiwa kutoka hospitali Morogoro. Hadija Kopa akiwa na mmoja wa majeruhi wa ajali hiyo.
Mwenye baraghashia ni mwanamuziki wa coast modern taarab Omari Tego akimsindikiza kwenda nyumbani kupumzika mmoja wa majeruhi wa ajali hiyo.
Eneo la tukio
Mwanahawa Alli akiwa hospitali MOROGORO
Mtangazaji Startv akiwahoji baadhi ya waombolezaji
Askari Wanyamapori wa Mikumi Mbuga ya Wanyama wakilinda usalama wa eneo la ajali.
VIONGOZI AFRIKA WALAANI UVAMIZI MAGHARIBI LIBYA
Marais wa Uganda, Zimbabwe na Afrika ya Kusini kwa nyakati tofauti wamelaani uvamizi wa kijeshi wa Marekani na marafiki zake kwa Libya na kusema kuwa mashambulizi hayo ni undumilakuwili wa mataifa hayo yanayoacha baadhi ya mambo yaendelee katika mataifa mengine vibaraka kwao na kuishupalia Libya. Mugabe na Museveni wamesema nchi hizo zimevamia Libya wakiwa na nia ya kujipatia mafuta kibabe huku Zuma wa Afrika ya Kusini akiona ni siasa zisizofaa za mataifa hayo kujichagulia viongozi vibaraka kwao. Umoja wa Nchi za Afrika umeyataka mataifa hayo kusitisha mashambulizi hayo mara moja.
Jumatatu, 21 Machi 2011
MUNGU MKUBWA
Kijana anayefahamika kwa jina la Hassan wa Tanga ni mlemavu wa mtindio wa ubongo anaishi kwa mateso makubwa kwa kufungwa kamba kama ng'ombe wa maziwa muda wote. Wazazi wake wanasema wamechukua hatua hiyo ili kumnusuru na kipigo toka kwa wananchi kwa vile akiachwa huru ni mkorofi kwa kuharibu mali za watu na anatembea kwenda mbali bila kukumbuka kurudi nyumbani.
Mbunge wa viti maalumu mkoa wa Tanga CUF Amina Mwidau akisalimiana kwa furaha na Hassan pale alipoenda kumtembelea nyumbani kwao Tanga mjini.
Jumapili, 20 Machi 2011
KANISA LA TEGETA STENDI LATEKETEA KWA MOTO
Mnamo saa 11.10 jioni ya jana jumamosi,bila kutarajia moshi ulionekana ukitoka juu ya paa la kanisa. Eneo hilo ni lenye msongamano wa watu wakiwemo wafanyabiashara wakubwa na wadogo.
Hapa paa limeshaungua na kuanguka chini,moto umepungua kidogo, hata hivyo natoa pongezi kwa kikosi cha uokoaji cha jiji kufika eneo la tukio saa 11.50 licha ya umbali uliopo kati ya Kariakoo-Fire na Tegeta km25 na msongamano wa magari. Wananchi wachache walionekana kuwabeza zimamoto kwamba wamechelewa lakini ukichunguza sana si kweli kwa maana ya umbali,polisi wa doria walijitahidi kulinda usalama wa eneo pamoja na wazimamoto waliokuwa wanafanyiwa vurugu. Vikosi vya zimamoto vya binafsi vilichelewa kuja ingawa viko jirani,wajirekebishe.
Watu walianza kujikusanya wasijue la kufanya maana dalili za moto mkubwa zilikuwa wazi. Moshi uliongezeka, wafanyabiashara walianza kusalimisha mali zao.
Moto umekolea, jitihada zangu binafsi za kuwaita zimamoto ziligonga mwamba kwani simu 114 na 112 ya polisi inaonekana hazifanyi kazi kabisa maana haziiti, wahusika mtuelimishe jinsi namba hizi zinavyotumika na jinsi ya kuwapata linapotokea tatizo.
Kila mtu kataharuki anaokoa maisha yake,hakuna aliyejeruhiwa katika tukio hilo.
Moto ulivyokolea njia ilibaki nyeupe.
Hapa paa limeshaungua na kuanguka chini,moto umepungua kidogo, hata hivyo natoa pongezi kwa kikosi cha uokoaji cha jiji kufika eneo la tukio saa 11.50 licha ya umbali uliopo kati ya Kariakoo-Fire na Tegeta km25 na msongamano wa magari. Wananchi wachache walionekana kuwabeza zimamoto kwamba wamechelewa lakini ukichunguza sana si kweli kwa maana ya umbali,polisi wa doria walijitahidi kulinda usalama wa eneo pamoja na wazimamoto waliokuwa wanafanyiwa vurugu. Vikosi vya zimamoto vya binafsi vilichelewa kuja ingawa viko jirani,wajirekebishe.
Jumamosi, 19 Machi 2011
MAMBO YA FEDHA
Mfanyabiashara Hans Macha pamoja na familia yake amekodi Helikopta na kutua jirani kabisa na nyumbani kwa mchungaji Mwasapile kijiji cha Samunge kwa ajili ya kupata kikombe cha dawa.
Jisajili kwenye:
Machapisho (Atom)