Jumatano, 23 Machi 2011

VIONGOZI AFRIKA WALAANI UVAMIZI MAGHARIBI LIBYA

Marais wa Uganda, Zimbabwe na Afrika ya Kusini kwa nyakati tofauti wamelaani uvamizi wa kijeshi wa Marekani na marafiki zake kwa Libya na kusema kuwa mashambulizi hayo ni undumilakuwili wa mataifa hayo yanayoacha baadhi ya mambo yaendelee katika mataifa mengine vibaraka kwao na kuishupalia Libya. Mugabe na Museveni wamesema nchi hizo zimevamia Libya wakiwa na nia ya kujipatia mafuta kibabe huku Zuma wa Afrika ya Kusini akiona ni siasa zisizofaa za mataifa hayo kujichagulia viongozi vibaraka kwao. Umoja wa Nchi za Afrika umeyataka mataifa hayo kusitisha mashambulizi hayo mara moja.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni