Jumapili, 20 Machi 2011

KANISA LA TEGETA STENDI LATEKETEA KWA MOTO

 Mnamo saa 11.10 jioni ya jana jumamosi,bila kutarajia moshi ulionekana ukitoka juu ya paa la kanisa. Eneo hilo ni lenye msongamano wa watu wakiwemo wafanyabiashara wakubwa na wadogo.
 Watu walianza kujikusanya wasijue la kufanya maana dalili za moto mkubwa zilikuwa wazi. Moshi uliongezeka, wafanyabiashara walianza kusalimisha mali zao.
 Moto umekolea, jitihada zangu binafsi za kuwaita zimamoto ziligonga mwamba kwani simu 114 na 112 ya polisi inaonekana hazifanyi kazi kabisa maana haziiti, wahusika mtuelimishe jinsi namba hizi zinavyotumika na jinsi ya kuwapata linapotokea tatizo.
 Kila mtu kataharuki anaokoa maisha yake,hakuna aliyejeruhiwa katika tukio hilo.
 Moto ulivyokolea njia ilibaki nyeupe.

Hapa paa limeshaungua na kuanguka chini,moto umepungua kidogo, hata hivyo natoa pongezi kwa kikosi cha uokoaji cha jiji kufika eneo la tukio saa 11.50 licha ya umbali uliopo kati ya Kariakoo-Fire na Tegeta km25 na msongamano wa magari. Wananchi wachache walionekana kuwabeza  zimamoto kwamba wamechelewa lakini ukichunguza sana si kweli kwa maana ya umbali,polisi wa doria walijitahidi kulinda usalama wa eneo pamoja na wazimamoto waliokuwa wanafanyiwa vurugu. Vikosi vya zimamoto vya binafsi vilichelewa kuja ingawa viko jirani,wajirekebishe.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni