Jumatano, 23 Januari 2013

KIFAA CHA SWANSEA MICHU AONGEZA MKATABA NA TIMU HIYO.

Michu asaini mkataba mpya na Swansea

Michu akishangilia bao lake
Mshambuliaji wa Swansea Michu, amesaini mkataba mpya, na kuongeza muda wake na klabu hiyo kwa muda wa miaka minne ijayo.
Mchezaji huyo kutoka Uhispania, ameibuka kuwa miongoni mwa wachezaji bora wa ligi kuu ya Premier ya England tangu aliposajiliwa kwa kitita cha pauni milioni mbili nukta mbili na klabu ya Rayo Vallecano.
Michu mwenye umri wa miaka 26, sasa atasalia katika klabu hiyo hadi mwaka wa 2016.
Akiongea baada ya kusaini mkataba huo, Michu alisema, hakuwa na ugumu wowote kuongeza muda wake na Swansea.
Nyota huyo ambaye ana uwezo wa kucheza kama mcheza kiungo au mshambuliaji, amefunga magoli 16 baada ya kucheza mechi ishirini na nane.
Wachambuzi wa masuala ya soka nchini England wanasema kuwa yeye ni mmoja wa wachezaji bora zaidi kuwahi kusajiliwa na klabu hiyo ya Swansea.
Kocha wa Swansea, Michael Laudrup, amemsifu mchezaji huyo kwa mchango wake katika ufanisi wa klabu hiyo na kumtaja kama kito ya msimu.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni