Jumanne, 1 Januari 2013

FAHAMU MATUMIZI YA ASALI KAMA TIBA YA VIDONDA.

Asali ni tiba ya kidonda  
Kwa nini asali
Asali imetumiwa na jamii nyingi katika katika kutibu kuchomeka, malengelenge, majeraha yatokanayo na kulalia kitanda na majeraha mengine makubwa yanayoudhi.Utafiti umefanyika kote duniani unaoonyesha ya kwamba majeraha yakitibiwa kwa asali halisi hupona kwa haraka na vyema. Majeraha yanayotokana na kuchomeka,majipu,kisukari na kadhalika mara kwa mara huambukizwa na hutoa harufu mbaya.Ukitumia asali kwa majeraha kama haya,harufu hii itaisha katika kipindi cha wiki moja.

 
Majeraha mengi ambayo ni makubwa na yenye kina kirefu ambayo yameambukizwa yanahitaji dakitari ampeleke mgonjwa kwenye chumba cha kupasuliwa ili yasafishwe vizuri. Kutumia asali huondoa haja ya hili na jeraha litapona bila ya kuhitaji kupasuliwa.Mgonjwa mwenye jeraha huhisi uchungu mwingi wakati anapoenda kufungwa jeraha kila siku katika kituo cha afya.Hii ni kwa sababu bendeji hukwama kwenye jeraha.Wakati bendeji inapobadilishwa,hujivuta kutoka kwenye jeraha na kusababisha uchungu na saa zingine hutonesha kidonda upya.
 
Mengi ya dawa zinazotumiwa kutibu majeraha aidha hukausha kidonda ili kuzuia ambukizo ama kulifanya kuwa na unyevu.Jeraha lililokauka huwacha makovu makubwa ilhali jeraha lililo na unyevu huvutia bakteria na inaweza kusababisha ambukizo la mda mrefu. Dawa zilizotengenezwa na binadamu kupigana na bakteria (kiua vijasumu) yana madhara ya kando, huwa kali na hupunguza kasi ya uponaji wa jeraha. Asali kwa upande mwingine, huvuta uoevu kutoka mwilini ambao una seli, virutubishi na vitu vingine ambavyo huongeza kasi ya uponaji wa ngozi. Hii ni njia asili ya kuwezesha uponaji na pia hupunguza ukubwa wa kovu lililoachwa nyuma na jeraha. Hata jeraha lililoathirika hupona haraka ukitumia asali.
 
Asali haswa ni ya manufaa katika kutibu kila aina ya kuchomeka na majeraha ambayo yamekuwa hapo kwa mda mrefu kwa sababu ya magonjwa kwa mfano kisukari,kung’atwa na mdudu,kuumwa na wanyama na magonjwa ya ngozi.Imepatikana kufanya kazi kwa haraka na haina madhara ya kando na madakitari wengi na wauguzi huipendekeza kwa majeraha kama hayo.Haina athari za kando na mara kwa mara sio chungu.Ikitumiwa kwenye macho,kuna mshawasha mdogo ambao huisha.
 
Tahadhari
Ni muhimu kutafuta matibabu kwa jeraha ambalo haliponi vizuri kabla ya kulitibu mwenyewe nyumbani.Hali zingine ambazo ni mbaya kwa mfano saratani zinaweza kufanya jeraha kutopona vyema na ni muhimu kwa dakitari/mwuguzi kukagua jeraha kabla ya kuanza kulifunika kwa asali.
 
Jinsi ya kutumia asali ili kufunika jeraha
  • Osha jeraha kwa kutumia maji yaliyo kavu ama mchanganyiko ambao umewekwa katika matone na kutumiwa katika zahanati/hospitali (myeyusho wa kawaida wa chumvi na maji).
  • Tumia asali halisi ambayo iko katika mfumo wa maji maji ili kuifanya iwe rahisi kuipaka.Ikiwa imekauka kidogo,ipashe joto pole pole lakini sio sana kwani hili litaharibu uwezo wake wa kupambana na maambukizo.
  • Mwaga asali kwenye shashi,bendeji,n.k kisha weka hii kwenye jeraha.
  • Ikiwa una bendeji inayozuia asali kuvuja,hiyo ndiyo nzuri zaidi.Ikiwa hauna tumia tepu ili kushikilia bendeji/shashi na kuizuia kupitisha asali.
  • Kumbuka ya kwamba asali ikiwekwa kwenye ngozi huvutia nzi na wadudu wengine kwa hivyo ni muhimu kuhakikisha ya kwamba haitoki nje ya bendeji.
  • Ikiwa jeraha ni la kina kirefu na haswa lina rusu nyeupe (tishu zilizokufa) chini yake,mwaga asali moja kwa moja kwenye jeraha kisha mwaga nyingine kwenye bendeji na kisha funika jeraha.
  • Tumia asali ya kutosha ili isizimuliwe na uoevu ulioko ndani ya jeraha.Kwa hivyo jinsi jeraha lilivyo kubwa ama lina kina kirefu ndivyo unavyohitajika kutumia asali nyingi zaidi
  • Badilisha bendeji kila siku. Ikiwa asali imevuja sana kwenye bendeji/shashi, badilisha na utumie mpya.
  • Ikiwa jeraha liimeambukizwa,unaweza kubadilisha bendeji ama shashi mara 2-3 kila siku na linapoanza kupona ,ibadilishe mara moja kila siku na kisha baada ya kila siku kadhaa.
  • Hata hivyo,ikiwa hili haliwezekani,kubadilisha bendeji ama shashi kila siku kunatosha.
  • Kunywa vijiko vidogo 6-10 kila siku pia kumepatikana kuongeza kasi ya uponaji.
  • Pindi tuu jeraha linapokauka na linapona vyema, wacha kutumia asali
Chanzo;http://kenya.thebeehive.org

Maoni 23 :

  1. Ni kweli docta , asili ni tiba nzuri katika kutibu vidonda vyenye unyevu ikiwemo vidonda sugu.

    JibuFuta
  2. Asante nimeelewa vyema kuhusu asali na vidonda

    JibuFuta
  3. Asante nimeelewa vyema kuhusu asali na vidonda

    JibuFuta
  4. Ingiza maoni yako...Ahsante Doct Nimeelewa

    JibuFuta
  5. Ingiza maoni yako...Ahsante Doct Nimeelewa

    JibuFuta
  6. Ingiza maoni yako...Ahsante Doct Nimeelewa

    JibuFuta
  7. Ingiza maoni yako...Ahsante Doct Nimeelewa

    JibuFuta
    Majibu
    1. Ivi na kidonda Cha kujikata na kisu au kioo unaweza kupaka asali

      Futa
  8. Ingiza maoni yako...Ahsante Doct Nimeelewa

    JibuFuta
  9. Ingiza maoni yako...Ahsante Doct Nimeelewa

    JibuFuta
  10. Ninashukuru sana doctoor hii imekaa vizuri. Nina kidonda kinanisumbua zaidi ya mwezi mmoja na nusu.

    JibuFuta
  11. nina kidonda cha moto makalioni kinanisumbua mpaka sasa ni mwezi na nusu nitafanya hivyo maana mateso makubwa

    JibuFuta
  12. Kidonda changu nicha exhaust na ni deep ni vizuri kutumia asari.

    JibuFuta
  13. Kindonda cha accident unaweza paka asali

    JibuFuta
  14. Ahsante 🙏

    JibuFuta