Jumatano, 14 Novemba 2012

KIKWETE ASHINDA KWA KISHINDO UENYEKITI WA CCM TAIFA KWA MSIMU WA HADI 2017, KURA 2 KATI YA 2397 ZASEMA HAPANA.

Rais Jakaya Kikwete amechaguliwa na kushinda kwa kishindo uchaguzi wa nafasi ya Mwenyekiti wa CCM taifa kwa kupata kura 2395.kati ya 2397 zilizopigwa hapo jana mjini Dodoma. Kwa matokeo hayo Ndugu Jakaya Kikwete ameitetea vyema nafasi yake hiyo hadi mwaka 2017. Huku kura za hapana zikiwa 2. Ushindi huo ni sawa na asilimia 99.92.
 
Aidha wagombea wa Nafasi ya Makamu Mwenyekiti ambazo kwa upande wa Bara ilikuwa ikigombewa na Katibu Mkuu wa zamani wa CCM, Philip Mangula naye amechaguliwa kuwa Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara kwa kura 2397,  huku nafasi ya Makamu Mwenyekiti Zanzibar ameshinda Rais wa Zanzibar, Dk.Ali Mohamed Shein kwa kupata kura zote zilizopigwa 2397. Ushindi wa Shein na Mangula ni sawa na asilimia 100.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni