Jumatano, 1 Agosti 2012

TUNDU LISSU AMEWATAJA WABUNGE WALA RUSHWA HADHARANI, NI WA CHAMA TAWALA CCM.


Lissu awataja wabunge wala rushwa hadharani


NewsImages/6551346.jpg
MBUNGE WA SINGIDA Mashariki [Chadema], Tundu Lissu, jana alitaja majina ya wabunge saba wanaohusika na kashfa ya rushwa zinazohusisha Shirika la Umeme Tanzania [TANESCO].
Lissu alitaja majina hayo mbele ya vyombo vya habari katika mkutano wake aliouitisha na wanahabari mjini Dodoma

Katika kikao hicho mbunge huyo alithubutu kwa kujiamini kutaja majina hayo bila hata chembe ya uoga wabunge wote wanaohusika na rushwa kupitia shirika hilo

Aliwataja wabunge hao wa CCM ambao wengi ni wajumbe wa Kamati ya Nishati na Madini bungeni ambayo kamati hiyo tayari imeshavunjwa na Spika. Anne Makinda.

Alianza kwa kutaja Sara Msafiri [VitiMalum], Mariam Kisangi [Viti Maalum], Christopher Ole Sendeka [Simanjiro], Vicky Kamata [Viti Maalum] Bw. Yusuph Nassir [Korogwe Mjini], Bw. Charles Mwijage [Muleba Kaskazini] na Munde Tambwe [Viti Maalum] hao ni ambao kutoka Chama cha Mapinduzi [CCM].

Katika orodha yake hiyo Lissu aliwatetea wabunge wengine kutoka CHADEMA ambao wako katika kamati hiyo kutoka CHADEMA, ambao ni John Mnyika [Ubungo], David Silinde [Mbozi Magharibi] na Mwanamrisho Taratibu Abama [Viti Maalum] kuwa hawahusiki kabisa katika kashfa hiyo.

Katika taarifa yake hiyo alisema wabunge hao ndio chachu ya kuporomoka kwa Tanesco ambapo aliwataja mbunge Sara Msafiri na Munde Tambwe, wamekuwa wakipewa tenda ya kuiuzia matairi TANESCO

Alifafanua mbunge Yusuph Nassir na Mariam Kisangi kuwa wanamiliki vituo vya mafuta hivyo na ndio mana wamekuwa wakipokea rushwa kwa mgongano wa kimasilahi kutoka Wizara ya Nishati.

Alimuelezea Ole Sendeka kuwa, mbunge huyo amekuwa mtetezi namba moja kutetea Kampuni ya Orxy na Camel kwa kukosa tenda ya kuizuia mafuta IPTL kwa kudai ni vituo ambavyo vinafaa

Amesema wabunge hao wote kwa pamoja wamekuwa wakipata manufaa kutoka shirika hilo

Hivyo kupitia taarifa yake hiyo amemuomba Spika wa Bunge avunje kamati zote zinazotiliwa mashaka na utoaji wa rushwa

Leo asubuhi mbunge Ole Sendeka amemuomba Spika ampe muongozo kuhusiana na tuhuma alizopewa na Lissu kuwa athibitishe kauli zake alizozitoa kupitia vyombo vya habari kumchafua kw watanzania

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni