Jumapili, 19 Agosti 2012

TANZANIA NA MALAWI HAZINA MPANGO WA KUINGIA VITANI.

Rais Jakaya akiwa katika mazungumzo na Rais wa Malawi Joyce Banda wakati walipokutana nchini Msumbiji kwenye mkutano wa SADC
Tanzania haina nia wala mpango wa kuingia katika vita na nchi jirani
ya Malawi kufuatia tofauti zao kuhusu mpaka katika Ziwa Nyasa
Rais Jakaya Kikwete amesema hayo leo kufuatia mazungumzo baina yake na
Rais aw Malawi, mheshimiwa Joyce Banda.
“Namhakikishia dada yangu na watu wote wa Malawi kwamba hatuna nia
wala mpango wa kuingia vitani, hatuna matayarisho ya jeshi wala jeshi
halijasogea popote kwani hakuna sababu” amesema na kuongeza kuwa “Mimi
ndiye kamanda Mkuu wa Majeshi na sijapanga wala kutoa maelekezo ya
vita”.
Rais amesema hayo, mbele ya Rais Banda na kuongeza kuwa Kumekuwa na
sintofahamu ya muda mrefu kuhusu suala la mpaka na tayari maafisa aw
pande zote mbili wameshaanza kulizungumzia Kwa nia ya kulitatua Kwa
Amani.
“Tuviachie vyombo vyetu vifanye kazi, hebu tuvipe nafasi, wanasiasa na
waandishi wa habari wajiepushe na maneno haya yanayosababisha taharuki
na chokochoko, hayana maana yeyote tuachie diplomasia ifanye kazi
yake” Rais amesisitiza.
Naye Rais Banda amesema amefurahishwa na kufarijika baada ya
kuhakikishiwa kuwa hakuna vita na Rais Kikwete.
“Nimefarijika sana, swala hili limetusumbua sana, mpaka we Malawi wote
wakaungana na kuwa kitu kimoja na kuzuia tofauti zao” amesema na
kuvishukuru vyombo vya habari vya Malawi Kwa kuonyesha uzalendo na
ukomavu katika suala hili.
Rais Kikwete yuko Maputo, Msumbiji kuhudhuria kikao cha viongozi wa
Jumuiya Ya Maendeleo Kusini Kwa Afrika (SADC) uliofunguliwa tarehe 17
August, 2021 na unatarajiwa kumalizika leo jioni ( tarehe 18.august
2012)
Katika kikao cha Jana Tanzania imechukua uenyekiti wa Kamati ya Siasa,
Ulinzi na Usalama kutoka Afrika ya Kusini ambapo uenyekiti wa SADC
umechukuliwa na Msumbiji kutoka Angola, nafasi hizi ni za mwaka mmoja
mmoja Kwa zamu.
Rais Kikwete anatarajia kurejea nyumbani Mara baada ya kikao hiki.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni