Ijumaa, 3 Agosti 2012

MRISHO NGASSA AMEPOKELEWA KWA KISHINDO LEO HUKO MTAA WA MSIMBAZI.

Mrisho Ngassa akikabidhiwa vifaa vya michezo kutoka kwa wanachama wa Simba SC.
Ngassa akionyesha jezi aliyokabidhiwa na Simba SC.
...Akiwa katika pozi na wanachama wa Simba.…


Mrisho Ngassa akikabidhiwa vifaa vya michezo kutoka kwa wanachama wa Simba SC.

Ngassa akionyesha jezi aliyokabidhiwa na Simba SC.
...Akiwa katika pozi na wanachama wa Simba.
Mashabiki wa Simba waliofika kumkaribisha Ngassa wakiwa na bango la kuwakejeli watani wao,mwenye bango ni shabiki maarufu wa Simba SC Hamis Kapopo wa Songea.

Mashabiki wakimshangilia Ngassa anayeingia kwenye gari.

...Wakilisonga gari lake.

Mashabiki wakimsindikiza Ngassa wakati akiondoka Makao Makuu ya Simba.
MCHEZAJI mpya wa Simba, Mrisho Ngassa, leo amekabidhiwa jezi namba 16 atakayokuwa akiitumia kwenye klabu yake msimu huu.
Ngassa alikabidhiwa jezi yake hiyo katika makao makuu ya Simba Mtaa wa Msimbazi jijini Dar es Salaam na Makamu Mwenyekiti wa Simba, Geofrey Nyange Kaburu.
Kaburu alisema Simba inamkaribisha Ngassa kwa moyo mmoja na kwamba wapenzi wote wa Wekundu wa Msimbazi wana imani kubwa naye kwani uwezo wake mkubwa wa soka unafahamika ndani na nje ya nchi.
"Tunashukuru kwamba tumekidhi vigezo vyote vilivyohitajika kwa ajili ya usajili wa mchezaji huyu. Tumeingia naye mkataba wa mwaka mmoja baada ya kumaliza muda wa mkopo wake kutoka Azam na ni imani yetu kwamba ujio wa Ngassa utaimarisha zaidi timu kwani yeye ni miongoni mwa wachezaji ambao Kocha Mkuu wa Simba, Milovan Cirkovic, anawapenda," alisema. 
Akizungumza katika tukio hilo, Ngassa alisema amefurahi kusajiliwa na Simba kwani ni sawa na historia kujirudia, akikumbusha kwamba baba yake mzazi, Khalfan Ngassa, aliwahi kuwa mchezaji wa klabu katika miaka ya 1990.
Kabla ya mkutano huo na waandishi wa habari, Ngassa alifanya mazoezi na wachezaji wenzake wa Simba katika ufukwe wa Coco, jijini Dar es Salaam ambako Simba inaendelea na mazoezi yake chini ya makocha Amatre Richard na James Kisaka.

(PICHA NA RICHARD BUKOS / GPL)

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni