Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo TAARAB. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo TAARAB. Onyesha machapisho yote

Jumatatu, 9 Januari 2012

MASHAUZI CLASSIC TAARAB KUTUMBUIZA NDANI YA NACHINGWEA LEO USIKU.

Isha Ramadhan a.k.a Mashauzi Original, ndiye kiongozi wa kundi hilo la Taarab, tayari yupo Nachingwea kwa shoo ya usiku wa leo.
Mtoto anavutia ile mbaya, uongo!!!? Kama kawaida show itafanyika katika ukumbi maarufu wa NR.
Isha Ramadhani. Mkurya wa kwanza kuimba taarabu.

Alhamisi, 29 Desemba 2011

MALKIA WA MIPASHO AL ANISA HADIJA KOPA KUTUMBUIZA NACHINGWEA LINDI MWAKA MPYA TAREHE 02.



Malkia Hadija Kopa.


Kundi zima la TOT Taarab chini ya uongozi wa Al Anisa Khadija Bint Kopa linatarajiwa kutumbuiza mjini Nachingwea siku ya pili baada ya mwaka mpya kuingia yaani tarehe 02/01/2012 ikiwa ni shamrashamra za kuukaribisha mwaka 2012 katika Ukumbi maarufu wa Nachingwea Resort (NR).Wakati wakazi wa Nachingwea wakisubiri kwa hamu kumuona Malkia na kundi lake la TOT, kwa sasa Hadija yupo katika ziara ya nchi kadhaa za Ulaya, lakini kwa mujibu wa waandaaji wa ziara hiyo,wamesema hilo lisiwatishe na wana uhakika kuwa Hadija atakuwepo siku hiyo ili kuwaburudisha.

Jumapili, 6 Novemba 2011

HADIJA KOPA ALIVYOWAPAGAWISHA MASHABIKI WA TAARAB UINGEREZA.


Khadija Kopa nguli wa muziki wa taarabu alikuja Uingereza kwa shoo moja tu ambayo aliifanya mwishoni mwa wiki iliyopita.

Khadija Kopa aliondoka Uingereza kuelekea Nairobi nchini Kenya kwa shoo nyingine ya taarabu huku nyuma akiacha gumzo jinsi alivyoweza kulitawala jukwaa na kufanya manjonjo mengi ambayo yaliwafanya watu wapagawe.

Hadija Kopa akipokelewa na wenyeji wake Uingereza katika Uwanja wa Earthrow mwezi uliopita mwishoni.

 Khadija Kopa aliimba zaidi ya nyimbo 10 zikiwemo nyimbo zake zinazotamba nchini Tanzania pamoja na nyimbo mpya toka kwenye albamu yake mpya ya "Full Stop


Mashabiki wakifurahi.


Alhamisi, 3 Novemba 2011

OMARI TEGO NA KUNDI ZIMA LA COAST MODERN TAARAB WAPAGAWISHA NACHINGWEA JANA.

Kiongozi wa kundi Omari Tego.
Kundi likiwa kazini. 
Shabiki akipiga picha na muimbaji wa kike wa kundi hilo.
Kundi la Taarab la Coast toka Dar es salaam lipo katika ziara maalum ya mikoa ya kusini ya Lindi na Mtwara. Juzi walikuwa wilayani Liwale, jana Nachingwea katika ukumbi wa NR ambapo umati wa watu ulifurika kuburudika na kundi hilo linaloongozwa na Al-Ustaadh Omari Tego, leo jioni kundi hilo litakuwa wilayani Rwangwa.




Jumapili, 1 Mei 2011

TOT TAARAB IKIFANYA VITU VYAKE JUMATATU YA PASAKA DECCA INN BOKO

Bibie Rukia Juma akiimba na kundi lake la TOT, utu uzima dawa kweli, huyu ni mama mzazi wa mwimbaji mwingine maarufu wa taarab aitwae Isha Ramadhan.(Mashauzi)