Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo SIASA CHAFU. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo SIASA CHAFU. Onyesha machapisho yote

Jumatatu, 4 Juni 2012

PICHA YA LEO; MJUE FARID HADI, KIONGOZI WA KUNDI LA UAMSHO LA ZANZIBAR.


Huyu ndiye Kiongozi wa Kundi linaloitwa UAMSHO la Zanzibar ambalo ni la shughuli za mihadhara ya Kidini hasa ya Kiislam.
Hivi karibuni kumekuwa na matukio ya vurugu huko Zanzibar na habari zilizoenea ni kuwa Kundi hili linahusika  na vurugu hizo, je ni kweli malengo ya kundi hili ni vurugu au kuna propaganda ndani yake ya kulichafua hadhi yake ili lionekane halifai!!!?
Nawaasa Viongozi wa Serikali na Vyombo vya Dola kutotoa majibu ya harakaharaka juu ya vurugu za Zanzibar badala yake ifanye uchunguzi wa kina juu ya matatizo yaliyopo ili yatatuliwe.
 Katiba ya JMT inaruhusu uhuru wa kutoa mawazo lakini uhuru huu usiingilie uhuru wa mwingine.

Jumanne, 29 Mei 2012

WANA UAMSHO ZANZIBAR WAMEPEWA DHAMANA JANA.

Watu thelathini waachiliwa kwa dhamana kufuatia ghasia mjini Zanzibar
Viongozi wawili wa kundi la Uamsho waliokuwa wanashikiliwa na polisi wa Zanzibar kwa zaidi ya siku mbili pamoja na baadhi ya wafuasi wao wameachiwa kwa dhamana katika mahakama ya Mwanakwerekwe huko mjini Zanzibar.
Kwa mujibu wa wachambuzi wa mambo ya kisiasa, kuachiwa kwa viongozi hao ambao walikuwa wanakabiliwa na kosa la kuandamana bila kibali kunaweza kukomesha uhasama wa takriban siku mbili baina ya wafuasi wa kundi hilo na polisi.
Mwandishi wetu Aboubakar Famau aliyekuwa Zanzibar anasema hali ilianza kuwa shwari mjini Zanzibar baada ya kuachiliwa kwa dhamana kwa wafuasi takriban thalathini wa kundi la Uamsho waliokuwa wanashikiliwa na polisi mjini humo kwa tuhuma za kuandamana bila kibali.
Miongoni mwa waliopata dhamana hiyo ni Sheikh Mbaruku Saidi Khalfan na Musa Juma Musa wote wakiwa viongozi wa kundi hilo ambao kukamatwa kwao kumeleta kizazaa mjini humo.
Mbele ya Hakimu wa mahakama ya Mwanakwerekwe majira ya saa nne asubuhi Jumatatu, baada ya kusomewa mashtaka ya kufanya mkusanyika haramu katika maeneo mbalimbali ya Zanzibar, watuhumiwa hao kwa pamoja walikana tuhuma hizo.
Baadaye wakili wa watuhumiwa hao aliwaombea dhamana, ombi ambalo lilikubaliwa bila pingamizi lolote.
Kukamatwa kwa viongozi hawa kumeleta sokomoto kubwa mjini Unguja hasa baada ya wafuasi wa kundihilokuamua kuandamana kwa lengo la kuishinikiza polisi kuwaachia.
Hali iliyosababisha vuta nikuvute baina ya wafuasi hao na polisi ambao wamekuwa wakitumia mabomu ya kutoa machozi na maji ya kuwasha.
Uamsho ni kundi la kidini ambalo limejipa jukumu la kuwaelimisha wazanzibari kuhusu suala la muungano hasa wanapotoa maoniyaokatika Tume ambayo inakusanya maoni ya wananchi kuhusu katiba mpya. Hata hivyo, taarifa zisizothibitishwa zinasema, kundihilolimejikita zaidi katika kuwahamasisha wananchi kuupinga muungano

Ijumaa, 30 Desemba 2011

MBUNGE ASEMA RAIS MUGABE NI SHOGA.

Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe.
Mbunge wa chama cha MDC (Movement for Democratic Change) cha nchini Zimbabwe amejikuta akiingia matatani baada ya kudai rais wa Zimbabwe, Robert Mugabe alifanya mapenzi ya jinsia moja.Mbunge huyo ametupwa jela kwa siku saba.

Mbunge huyo wa kike aliyetajwa kwa jina la Lynette Kareny alisema kuwa Robert Mugabe ambaye pia ni rais wa chama tawala cha Zanu-PF alifanya mapenzi na wanasiasa wawili wa kiume.

"Karenyi anatuhumiwa kutoa kauli hiyo ya kumkashifu kiongozi wa nchi wakati wa mkutano wa hadhara wa chama cha MDC uliofanyika disemba 9 kwenye viwanja vya mpira vya Chimanimani,” limeripoti gazeti la The Herald la nchini Zimbabwe

Jumanne, 20 Septemba 2011

VIONGOZI WA CHADEMA WAWATETEA WAFUASI WAO WALIOMDHIBITI MKUU WA WILAYA YA IGUNGA KUWA WALIKUWA SAHIHI.!!!!!!

Mh. Tundu Lissu akiongea na Waandishi wa habari jana huko Igunga akilaani kitendo cha Wabunge wawili na mfuasi mmoja wa CHADEMA kufikishwa mahakamani Tabora juzi kwa kosa la kumshambulia Mkuu wa Wilaya ya Igunga aliyedaiwa kuingilia mkutano wao wa kampeni, alitaja pia nia yao ya kufanya lolote linalowezekana ili washinde kesi hiyo. Alisema watuhumiwa hao hawana kosa lolote walilotenda zaidi walikuwa wanalinda maslahi ya Chama chao.

Hivi ndio mambo yalivyokuwa hadi kupelekea Lissu kutetea waliopelekwa mahakamani, haya tusubiri tuone mahakama ikionesha haki imetendeka. Nasikia Lissu nae ni mwanasheria.

Jumamosi, 17 Septemba 2011

TIZAMA JINSI DC ALIVYODHALILISHWA NA WATU WANAOSEMEKANA NI CHADEMA, KAMA KWELI HIVI HAO CHADEMA NI NANI NCHI HII HADI WAACHWE WANAFANYA HAYA!!!?

DC wa Igunga Bi. Kimario akiwa na masikitiko makubwa baada ya kushambuliwa na wafuasi wa CHADEMA juzi.

Hivi hawa jamaa wana akili kweli!!? Mkutano wa Ndani wa kiutendaji wa kiongozi wa serikali unawezaje kuathiri Mkutano wa Hadhara wa kampeni. Hapa Mkuu wa Wilaya akitolewa nje toka Ukumbi wa Mikutano, sasa utasemaje kakuingilia kwenye Mkutano wako ikiwa wewe unafanyia nje na wenzio ndani!? Tujifunze siasa za kuvumiliana, hapa sio Libya kwa Wapinzani wasio na staa na viongozi wao hata kama wamewafanyia mazuri, Hawa wachukuliwe hatua kali, haki za binadamu ni lazima zifuatwe, mwanaume unamkamata vipi mwanamke maungoni? Vyombo vya Dola viwajibike hasa kwa hili.

Ubabe mtupu, hapa Diwani wa CCM naye katiwa nguvuni na dola ya Chadema, ni maoni yangu tu na uchambuzi tu, siegemei chama chochote lakini udhalilishaji huu siukubali hata siku moja kwa kulinda heshima ya nchi hii na miaka hamsini ya Uhuru, haikubaliki.