Alhamisi, 26 Desemba 2013

JAMES KISAKA AAGWA LEO TAYARI KWA MAZISHI KESHO HUKO MUHEZA, WACHEZAJI WA ZAMANI WAKUTANA.


 Jeneza lenye mwili wa aliyekuwa Kocha wa makipa wa Simba, marehemu James Kisaka likiingizwa kwenye basi la klabu hiyo, baada ya kutolewa heshima za mwisho katika misa iliyofanyika katika Kanisa la Muhimbili, Dar es Salaam. Marehemu Kisaka atasafirishwa kwenda kwao wilayani Muheza, Tanga kwa mazishi yatakayofanyika kesho. 
  Mjane wa marehemu James Kisaka, Teddy Kisaka akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa mumewe
 Mtoto wa mwisho wa marehemu Kisaka, Christopher akitoa heshima za mwisho
  Msanii wa filamu Jacob Steven JB akitoa heshima za mwisho
 Mchezaji wa zamani wa Simba Malota Soma akitoa heshima za mwisho kwa mchezaji mwenzie marehemu Kisaka.
Mshambuliaji hatari wa Simba wa zamani Malota Soma 'Ball Juggler' akitoa heshima zake za mwisho 
 Mwandishi wa habari za michezo wa gazeti la Jambo Leo, Asha Kigundula akitoa heshima za mwisho
Aliyekuwa Kocha Msaidizi wa Simba, Jamhuri Kihwelo 'Julio',akimfariji Benny Kisaka, baada ya kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu James Kisaka.

Mjane wa marehemu James Kisaka, Teddy Kisaka akifarijiana na mtoto wa pili wa marehemu Kisaka, Boniface baada ya kutoa heshima za mwisho.
 Ndugu wa karibu wa marehemu Kisaka akilia alipokuwa akitoa heshima za mwisho
 Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Jambo Concepts Tanzania Limited, Juma Pinto (kushoto), akisalimiana na Mwenyekiti wa zamani wa Klabu ya Simba, Hassan Dalali.
 Wachezaji soka wa zamani wakijadiliana jambo nje ya Kanisa la Muhimbili walipokwenda kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu James Kisaka. Kutoka kushoto ni Madaraka Selemani, Peter Tino, Khamis Kinye, Bakari Malima na Thomas Kipese.
 Aliyekuwa Kocha Msaidizi wa Simba, Jamhuri Kihwelo 'Julio', (kushoto) akijadiliana jambo na baadhi ya wachezaji wa soka waliokwenda kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu James Kisaka.
 Benny Kisaka ambaye ni mdogo wa marehemu James Kisaka akisoma wasifu wa marehemu kakake.
 Credits; michuziblog

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni