Alhamisi, 14 Machi 2013

JORGE BERGOGLIO TOKA ARGENTINA ACHAGULIWA KUWA KIONGOZI WA KANISA KATOLIKI DUNIANI.ACHAGUA JINA LA PAPA FRANCIS.Jesuit Cardinal Jorge Bergoglio wa Buenos Aires amechaguliwa kuongoza Wakatoliki billioni moja kama Papa Francis I.

Ni Baba Mtakatifu wa kwanza kutoka Amerika ya Kusini. Kwenye hotuba yake ya kwanza amwombea Benedict, aomba Kanisa "litembee pamoja katika imani".

Ametoa baraka yake ya kwanza ya umma saa nne unusu kwa saa za Afrika Mashariki. Awaomba waumini wamwombee.Wachambuzi wasema Francis ni Papa "mnyenyekevu."

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni