Jumapili, 17 Machi 2013

DEREVA WA DALADALA KAPIGWA RISASI AKIWA KWENYE FOLENI SINZA JUZI


Tukio lilitokea Ijumaa usiku kwenye saa tatu kasoro Sinza Kumekucha Dar es salaam karibu na kanisa la KKKT ambapo ilikua ghafla mlio wa risasi ukasikika ikiwa imelengwa kwa dereva wa daladala.

Watu waliokuwepo karibu wamesema dereva wa hii daladala anadaiwa kumkosea na kumkasirisha mtu wa pikipiki alipokua kwenye foleni.

Ghafla mtu huyo wa pikipiki ambae hakufahamika akiwa amebeba abiria inadaiwa alipita kwa mbele akachomoa bastola na kupiga risasi na kuondoka.

Inadaiwa dereva wa daladala aliepigwa risasi kichwani, alifariki muda mfupi baada ya tukio hilo huku watu wakishuhudia abiria mbalimbali wakitokea madirishani na wengine wakitoa vitu vyao kupitia madirishani.
credits;mpekuzi

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni