Jumamosi, 31 Agosti 2013

SERIKALI YA MAREKANI YATOA MSAADA WA VIFAA VYA MAWASILIANO KWA JWTZ NA POLISI HAPO JANA.



Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk. Emmanuel Nchimbi akizungumza na viongozi wa Jeshi la Polisi, Jeshi la Wananchi, Marekani pamoja na waandishi wa habari kabla ya kuzindua mitambo ya redio za mawasiliano katika Vituo vya Wanamaji vya Jeshi la Polisi na Jeshi la Wananchi.


Balozi wa Marekani nchini, Alfonso Lenhardt akitoa hotuba yake kabla ya uzinduzi wa mitambo ya redio za mawasiliano katika Vituo vya Wanamaji vya Jeshi la Polisi na Jeshi la Wananchi. Wakwanza kutoka kulia (aliyekaa) ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi. Mitambo hiyo imefungwa kwa hisani ya Serikali ya Marekani ambayo imegharimu Dola za Marekani milioni moja (1,000,000 USD). Redio hizo za mawasiliano zitasaidia kukabiliana na ajali pamoja na makosa yanayofanywa katika maeneo ya baharini na maziwa nchini.


Baadhi ya vifaa vya mawasiliano vilivyozinduliwa leo na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi pamoja na Balozi wa Marekani nchini Alfonso Lenhardt. Vifaa hivyo vya mawasiliano vitasaidia kukabiliana na ajali pamoja na makosa yanayofanywa katika maeneo ya baharini na maziwa nchini. Uzinduzi huo umefanyika katika Kituo cha Kikosi cha Polisi Wanamaji jijini Dar es Salaam leo. Picha na Felix Mwagara wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
 

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni