Jumatano, 21 Machi 2012

JIFUNZE JINSI YA KUONGEZA KIPATO KWA KUBLOG.

Zipo njia mbalimbali za kujiingizia kipato kupitia blogu au tovuti.

Njia hizo ni pamoja na kuuza vitu unavyotengeneza mwenyewe, kuuza vitabu unavyoandika, kuuza makala zako, kutoz kiasi fulani cha malipo kwa kutangaza au kuuza vitu vya watu wanaohitaji kuvitangaza/kuviuza kupitia intaneti, kutengeneza blogu/tovuti za wengine kutokana na ujuzi wako, kuweka matangazo ya makampuni (ndege, hoteli, vinywaji, michezo, benki, nk.) au asasi, chama au Serikali, kuingia mkataba wa kupata malipo kupitia mpango unaofahamika kama "affiliate program" kutoka kwa wenye tovuti wengine wanaohitaji kujitangaza kwenye blogu/tovuti yako, kupokea matangazo kupitia makampuni yanayohusika na biashara ya matangazo kama vile Google Adsense/Adword, AdBrite,  Bidvertiser, Chitika, Infolinks, Kontera, Clicksor, Oxygen, AdBull n.k.

Leo nitazungumzia AdSense ambayo maelezo kwa lugha ya kiingereza yanapatikana: 
google.com/adsense...tour

AdSense ni programu ya Google ambayo mtu yeyote mwenye blogu/tovuti anaweza kutuma maombi ya kujiunga nayo na ikiwa vigezo vitatimizwa, ataruhusiwa kujiunga na kisha kupata maelekezo kutoka kwa watu walio kwenye timu ya AdSense wanaoelekeza hatua za kufanya hadi kufanikisha kuyaweka matangazo kwenye blogu/tovuti.

Ili kujiunga na programu ya AdSense, fuata linki hii: 
google.com/adsense

Baada ya kujiunga utakuwa na fursa ya kuchagua aina ya matangazo unayotaka yaonekane kwenye tovuti yako. Mathalani tovuti yako inahusu mitindo ya mavazi na usingependa kuona habari za mambo ya siasa au dini, basi unao uchaguzi huo.

Vile vile upatapa fursa ya kuchagua ukubwa wa matangazo kulingana na ukubwa wa nafasi kwenye blogu yako. Vipo vipimo mbalimbali kama vile 600 x 200 au 300 x 250 au 120 x 120 ama 728 x 90 n.k kama vilivyoorodheshwa:  
google.com/adsense, na pia utaviona punde unapoandaa matangazo kabla ya kupata "code" kwa ajili yakuweka kwenye blogu yako. Video ya jinsi yakuandaa matangazo hayo imepachikwa hapo chini.

Kielelezo cha picha kifuatacho kinaonesha maeneo muhimu katika uso wa blogu/tovuti ambapo matangazo yakiwekwa huonekana kirahisi na wasomaji. Kielelezo hiki kimetengenezwa kutokana na utafiti uliofanyika kuona macho ya wasomaji huona na kubofya wapi zaidi wanapotembelea blogu/tovuti. Sehemu zilizoandikwa "hot" na "warm" ndizo za kuzingatia.

Pia unaweza kutizama video 
youtube.com/optimization ili kuona mfano halisi wa upangaji unaolipa zaidi.
Picture
picha toka squidoo.com
Kuna video zimeandaliwa na timu ya AdSense kwa ajili ya kukusaidia kujifunza zaidi, video mbili zimepachikwa hapo chini. Ukitaka kutizama video nyingine tumia linki hii:  youtube.com/user/InsideAdSense/videos

Baadhi ya tovuti/blogu zina 'host' ambaye amerahisisha uwezo wa kutumia matangazo ya AdSense hivyo unaweza usihitaji kutengeneza mwenyewe, ila utahitaji kujua ikiwa host wako anahitaji kupata kiasi fulani cha malipo yako kwa kuwa ana-host blogu/tovuti yako bure au kama unaweza kulipia gharama za ku-host na hivyo kumzuia asichukue malipo yako yoyote ya AdSense. Wapo host wengine hawaruhusu kabisa matangazo ya AdSense hadi utakapolipia gharma za ku-host tovuti/blogu. Maelezo hayo mwulize/utayapata kwa kusoma maelezo ya-host wako. 

Watumiaji wa Blogger/Blogspot wamerahisishiwa zoezi hili na host wao (Google Blogger/Blogspot). Baadhi ya wenye blogu kupitia blogger/blogspot tayari wanatumia matangazo haya, baadhi yao wanafahamu sababu ya uwepo wa matangazo hayo, wengine kwa kujua hawayatumii. Wengine wanajua ila kwa haipo njia ya kufanikishiwa malipo yao, wanaona haja ya kuweka Adsense; Mimi ninawashauri wasiokuwa na ufumbuzi wa jinsi ya kufanikishiwa malipo yao, basi wasiache kutangaza, bali waendelee tu na inawezekana siku moja wakapata ufumbuzi kupitia Google AdSense au kupitia rafiki/ndugu/jamaa ambaye atakuwa tayari kuingia nao ubia na kupokea fedha kwa niaba yao. Nitafafanua kuhusu hili kwenye toleo linalofuatia kuhusu malipo (usikose kuperuzi siku zijazo kulisoma).

Ikiwa una blogu na Blogger/Blogspot, tumia linki ifuatayo kufuata maelekezo:  
youtube.com/watch...blogger  
Leo nakomea hapa. Matoleo yanayofuatia nitazungumzia kuhusu mfumo wa malipo yako na miiko ya AdSense


Source: http://www.wavuti.com/

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni