Jumanne, 3 Septemba 2013

ARSENAL WAMEFANYA MAMBO. OZIL ATUA RASMI IMARATI.

Mjerumani huyo mwenye umri wa miaka 24 anayecheza nafasi ya kati amekamilisha uhamisho uliovunja rekodi kwa Madrid jana jumatatu jioni kwa ada inayoaminika kufikia paundi za Kiingereza £42.5milioni.
Ozil ameweka wazi kuwa kwa sasa hakuwa anapangwa katika kikosi cha kwanza cha Meneja wa Madrid Carlo Ancelotti kufuatia kumsainisha Gareth Bale toka Tottenham, hivyo bila kusita ameamua kuhamia timu mpya ya Arsenal, ambako anajipanga kuwa sehemu ya  timu ya ushindi ya Wenger akiwa sambamba na Jack Wilshere, Theo Walcott na Santi Cazorla.

Stint: Ozil has played 158 times for Real in just over three years
Ozil amecheza mechi 158 akiwa Real Madrid kwa zaidi ya miaka mitatu.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni