Kuna picha ya video inayoonesha jinsi askari saba wa serikali ya Rais Bashar al-Assad wa Syria walivyouawa na waasi wanaopigana kuuondoa utawala huo madarakani, tukio hilo la mauaji lilirekodiwa kwa kamera na waasi hao.
Askari hao walichapwa, kufungwa kamba na kulazwa kifudifudi huku waasi hao wakiwa nyuma yao na silaha zikielekezwa nyuma ya shingo zao, askari hao walikuwa na majeraha ya kuteswa kabla ya kuuawa.
Muda mfupi kabla ya kuuawa, kiongozi wa kundi hilo ajulikanae kama 'The Uncle', alighani shairi la dhihaka kabla ya kupiga risasi ya kwanza.
Inaogofya; askari wa Syria wakiwa wamefungwa na kulazwa kifudifudi kabla ya kuuawa, kulia kabisa ni kiongozi wa kundi la waasi ajulikanae kama'Mjomba Issa'.
Issa alirekodi video hii kwa mujibu wa mtoa habari ili aweze kupata misaada zaidi toka kwa wafadhili wake kifedha na silaha.
Ukatili; Baadaye miili ya askari hao ilitupwa kwenye kisima.
Mkutano wa G20 ukiendelea huko Urusi.